Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,094
538
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA



NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.


Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.
Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -


MKOAWILAYA ZAKEMKOA ZINAKOTOKAMAKAO MAKUU
1.GeitaGeitaMwanzaGeita


Nyang'hwale(Mpya)Mwanza


ChatoKagera


BukombeShinyanga


Mpya/MbogweShinyanga





2.SimiyuBariadiShinyangaBariadi


Itilima (Mpya)Shinyanga


MaswaShinyanga


MeatuShinyanga


Busega (Mpya)Mwanza





3.NjombeNjombeIringaNjombe


Wanging'ombe(Mpya)Iringa


LudewaIringa


Makete Iringa





4.KataviMpandaRukwaMpanda


Mlele(Mpya) Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYAWILAYA MAMAMKOAMAKAO MAKUU
1. BuhigweKasuluKigomaBuhigwe
2. BusegaMagu MwanzaIgalukilo
3. ButiamaMusomaMaraNyamisisi
4. ChembaKondoaDodomaChemba
5. GairoKilosa MorogoroGairo
6. IkungiSingidaSingidaIkungi
7. Itilima BariadiShinyangaItilima
8. KakonkoKibondoKigomaKakonko
9. KalamboSumbwangaRukwaKalambo
10. KaliuaUramboTaboraKalua
11. KyerwaKaragweKageraRubwera
12. MbogweBukombeShinyangaMbogwe
13. MkalamaIrambaSingidaNduguti
14. MleleMpanda RukwaInyonga
15. MombaMboziMbeyaNdalambo
16Nyang'hwaleGeitaMwanzaNyang'hwale
17. NyasaMbinga RuvumaMbamba Bay
18. UvinzaKigomaKigomaLugufu
19. Wanging'ombeNjombeIringaWaging'ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116

Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
9 Septemba, 2011

*************************************************
Wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania kwa sasa na jinsi Taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (Mikoa MINNE na Wilaya KUMI NA TISA).

Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa?

Swali la kujiuliza, Mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu Marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya JK ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama Baraza la Mawaziri, Uteuzi wa majaji, na hata Mikoa pamoja na Wilaya Mpya.

Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.

Source: Pmoralg - Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government | Tanzania

 
Morogoro na Mbeya ni Mikoa Mikubwa sana... naona hawawezi kuigawanya sababu ya Ardhi wamegawana hao wakubwa wa CCM

Wanaimaliza Mwanza sababu ya Upinzani, Wanaigawa gawa - vipi Majimbo yamekufa kabisa?
 
Sasa jamani matatizo hapa Tanzania bado ni mengi badala ya kupunguza mianya ya upotevu wa pesa(ufisadi/wizi)wao wanawaza kuongeza mikoa mipya isiyokuwa na tija!!!!?.Hiii iliyopo kwa sasa imeboreshwa kwa kiwango gani?Vipi suala la elimu bora,afya,miundombinu na mengine mengi!!?.Chonde chonde wakuu wa nchi sisi(wananchi)ndio maboss wenu pls tusikilizeni.
 
Chunya na Sikonge ni mawilaya makuwa sana unaweza kuanzisha mkoa plae.....sijui Chuny iliwakosea nini wakubwa wetu.....miaka mingi wanazuiwa kul;ma Pamba japo inamea vizuri tu....gold kibao
 
iliyopo hata kuunganishwa kwa umeme wa grid ya taifa bado, barabara ndo usiseme, huduma za afya ni kitendawili bado tunaongeza nafasi ya watu kutafuna kwenye ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa na vyeo utitiri kuanzia mkuu wa polisi wilaya, Das, Ras, Ded< maafisa ardhi, maafisa misitu, wanyamapori na utitiri wa watumishi kibao
Na mianya ya kula kw awatakaojenga ofisi za wakuu wa wilaya na mikoa na makao makuu ya polisi wilaya na mkoa na hospitali za mikoa na wilaya duh kweli Tzania zaidi ya uijuavyo
 
Mie nilitegemea mdau utakuja na orodha ya wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa maana tetesi zilizopo ni kwamba JK anatarajia kuwatangaza wateule hao wapya jioni ya leo!
 
Hata wakitangazwa hakuna atakachobadilisha wala kubadilika maana umaskini ndo unazidi na hao jamaa wamekalia tuu kuendesha maV* yao kututimulia vumbi
Bora hata tubaki na waliopo maana ufanisi wao hauonekani
 
Kwa afya ya uchumi tulionao kwa sasa hatuhitaji kuongeza mkoa au wilaya hata moja, na kwa mchakato wa katiba mpya upo mbioni wangeacha hii ije ijadiliwe na kuwekwa idadi maalumu mikoa na wilaya itakayojulikana kikatiba
 
Natarajia kutangazwa mkuu wa wilaya ya Ikungi.....sijui nami nitakuwa mmoja wa mfaisadi...au watanitosa nikikendelea kuwa mwaminifu?
 
Hongera jk, wacha wapinzani wa maendeleo waseme au wabeze, kusogeza mamlaka jirani zaidi na wananchi ni muhimu sana. Hata hivyo tangu lini? Wapinzani wakapongeza kazi ya serikali iliopo itakuwa ajabu.
 
Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail hakattanga@yahoo.comFax- 026-2322116

Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


9 Septemba, 2011

*************************************************

Hivi kweli serikali hawana mfumo rasmi wa e-mail zao hadi mtu antuwekea @yahoo.com ????!!!! Ubabaishaji mkubwa!
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIa
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA


NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
MKOA
WILAYA ZAKE
MKOA ZINAKOTOKA
MAKAO MAKUU
1.
Geita
Geita
Mwanza
Geita
Nyang’hwale(Mpya)
Mwanza
Chato
Kagera
Bukombe
Shinyanga
Mpya/Mbogwe
Shinyanga
2.
Simiyu
Bariadi
Shinyanga
Bariadi
Itilima (Mpya)
Shinyanga
Maswa
Shinyanga
Meatu
Shinyanga
Busega (Mpya)
Mwanza
3.
Njombe
Njombe
Iringa
Njombe
Wanging’ombe(Mpya)
Iringa
Ludewa
Iringa
Makete
Iringa
4.
Katavi
Mpanda
Rukwa
Mpanda
Mlele(Mpya)
Rukwa


Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
WILAYA MPYA
WILAYA MAMA
MKOA
MAKAO MAKUU
1.
Buhigwe
Kasulu
Kigoma
Buhigwe
2.
Busega
Magu
Mwanza
Igalukilo
3.
Butiama
Musoma
Mara
Nyamisisi
4.
Chemba
Kondoa
Dodoma
Chemba
5.
Gairo
Kilosa
Morogoro
Gairo
6.
Ikungi
Singida
Singida
Ikungi
7.
Itilima
Bariadi
Shinyanga
Itilima
8.
Kakonko
Kibondo
Kigoma
Kakonko
9.
Kalambo
Sumbwanga
Rukwa
Kalambo
10.
Kaliua
Urambo
Tabora
Kalua
11.
Kyerwa
Karagwe
Kagera
Rubwera
12.
Mbogwe
Bukombe
Shinyanga
Mbogwe
13.
Mkalama
Iramba
Singida
Nduguti
14.
Mlele
Mpanda
Rukwa
Inyonga
15.
Momba
Mbozi
Mbeya
Ndalambo
16
Nyang’hwale
Geita
Mwanza
Nyang’hwale
17.
Nyasa
Mbinga
Ruvuma
Mbamba Bay
18.
Uvinza
Kigoma
Kigoma
Lugufu
19.
Wanging’ombe
Njombe
Iringa
Waging’ombe


Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116
Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


9 Septemba, 2011

*************************************************
Wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania kwa sasa na jinsi Taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (Mikoa MINNE na Wilaya KUMI NA TISA).

Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa?

Swali la kujiuliza, Mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu Marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya JK ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama Baraza la Mawaziri, Uteuzi wa majaji, na hata Mikoa pamoja na Wilaya Mpya.

Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.
hivi.Du hii mikoa mingine,mfano kamkoa ka Pinda kana wilaya mbili tu,haiingii akilini,kupoteza hela ya walipa kodi kwa ajili ya kuanzisha mkoa wenye wilaya 2 tu heti tu kwasababu waziri mkuu anatoka mkoa huo,huo ni utumiaji mbaya wa madaraka,kama kila atakaye pata uwaziri mkuu atataka tarafa yake iwe wilaya na wilaya yake iwe mkoa ili wapate fungu kubwa basi kufikia 2050 Tanzania itakuwa na wilaya kama 130

Source: PMORALG - Home -
Du hii mikoa mingine,mfano kamkoa ka Pinda kana wilaya mbili tu,haiingii akilini,kupoteza hela ya walipa kodi kwa ajili ya kuanzisha mkoa wenye wilaya 2 tu heti tu kwasababu waziri mkuu anatoka mkoa huo,huo ni utumiaji mbaya wa madaraka,kama kila atakaye pata uwaziri mkuu atataka tarafa yake iwe wilaya na wilaya yake iwe mkoa ili wapate fungu kubwa basi kufikia 2050 Tanzania itakuwa na wilaya kama 130
 
Nipo kuwa mkuu wa mkoa au Wilaya nitajua hizi nafasi ni za kulipa fadhila..kwa watu fulani
 
Back
Top Bottom