Watu walishakula 10% kitambo!Ndio Tanzania ya leo, Uchumi unaendeshwa kwa kujaza mihela mitaani maanake kama utajiri ni fedha basi chapisha nyingi kwa mabillioni kila mtu atatajirika.. Hesabu za Idd Amin na JK.
jamani nyie acheni tu, mie sasa hivi nimetoka kuvuta noti za zamani kwenye ATM, halafu juzi kwa macho yangu nilikuwa azania benki nikaona jamaa wa back desk anazipanga noti za zamani zikiwa mpyaaaaaaaa tena mafundo mafundo, niliguna tu na kujisemea moyoni tunaenda wapi Tanzania.
Walituambia hela mpya inayofiti kwenye wallet maajabu waleti yangu nikiziweka utadhani hazimo hasa kile cha miatano.
no wonder you can breakNchi nyingine wale the two stooges wa Benki Huu na Hazina wangejiuzulu
Kuna habari za kuaminika kuwa noti mpya ambazo zilitengenezwa kwa gharama kubwa na kuwa launched kwa mbwembwe nyingi zimeondolewa kinyemela kwenye mzunguko kwa sababu zilichakachuliwa,
nashawishika kuamini kwa sababu benki zote kwa sasa hazina noti mpya ni za zamani tu. Naomba mwenye undani zaidi atufungue macho ni nini kinaendelea!
Kwa hiyo uchakachuaji uko kwenye utepe?
mh! hii nchi hii??Wahusika wa Ma-Benki, wanakwambia wakienda huko BOT kuchukua hizo noti, wanapewa za zamani, na nimarufuku kuoji! hivyo basi kama huna supply ya kuweka kwenye ATMs, ni lazima urudishe noti zinazopatikana, ambazo ni za zamani.
BOT hovyo kabisa, unajua walikuwa kama wanawalaumi mabenki kwa kutoweka hizo pesa mpya, walipoanza kufanya hivyo mara wanapewa za zamani.