Noti moja feki kutoka benki ya posta. Chukua tahadhari

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Huu sasa umekuwa ubazazi. Jana nimepokea noti kadhaa kutoka benki ya posta zenye thamani ya sh 10000 kila moja. Bila ya wasiwasi nikazitumbukiza mfukoni nikiamini kwa kuwa zinatoka benki hakuna wasi wasi. Nikaendelea na mambo yangu. Noti hiyo imegunduliwa kuwa ni feke pale Mlimani City baada ya kununua vitu kadhaa na kufanya malipo. Tahadhari, hata benki nao wanaingizwa mkenge, kuweni makini.
 
Noti zote mpya ni FAKE! Ukienda kufanya Manunuzi ukaambiwa ni FAKE irudishe Benki yoyote iliyo karibu nawe na utabadilishiwa bila kuulizwa maswali!
 
Haya pia yalitaka kunikuta nilipokuwa nikichukua hela toka kwa wakala wa M-pesa.Uzuri hela hiyo haikuwa kubwa hivyo ikanirahisishia kazi ya kuchunguza noti moja baada ya nyingine.Zilikuwa noti kumi za 5,000 na ndipo nilipogundua kuwa noti moja ina muonekano tofauti na nyinginezo.Uzuri nilikuwa sijatoka eneo hilo.
Angalizo: Tujenge tabia ya kuchunguza hela tunazopewa.
 
mabazazi sana kujifanya wanazo kumbe majizi makubwa
Sio majizi, hio unaweza ukakuta imetoka bank nyengine au hata imetoka kwa mteja alivofanya deposit. Mbona hata benki hupata loss kwa hela feki za wateja, kwani hakuna bank inayotengeneza hela feki ni watu mabazazi ndio wanaochakachua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom