Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Simu mpya za Nokia zinazotumia dainamo ya baiskeli kuchaji Friday, June 04, 2010 3:27 AM
  Kampuni kongwe ya simu duniani, Nokia imezitambulisha simu zake mpya za bei chee zenye laini (SIM card) mbili ambazo betri zake huchajiwa na dainamo ya baiskeli. Simu hizo zilitambulishwa kwa watu jana nchini Kenya ambapo Nokia imesema kuwa imelenga kuziuza kwa bei chee ingawa simu hizo ndio zitakuwa simu za kwanza za Nokia kutumia laini mbili.

  Simu hizo pia zina radio na tochi na vionjo vingine vya kawaida.

  Simu hizo zinazoitwa Nokia C1-00 zitauzwa kati ya Tsh. 50,000 na Tsh. 90,000 wakati chaja yake itakayotumika kwenye baiskeli itauzwa kuanzia Tsh. 15,000.

  Chaja ya simu hiyo inatumia dainamo ya baiskeli hivyo spidi ya mtu kuendesha baiskeli ndivyo betri litakavyojaa chaja nyingi.

  Safari ya dakika 10 kwa spidi ya kilomita 10 kwa saa italichaji betri na kukuwezesha kuongea mfululizo dakika 28 au masaa ya 37 ya simu kuwa ON.

  Nokia imesema kuwa simu hizo zimelenga zaidi maeneo ya Afrika ambako umeme unapatikana kwa tabu.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani wamelenga na kwa kukubali kutoa cm za line mbili kweli ushindani ni mkubwa au ni za kichina kwani nokia aligoma kutoa line 2
   
Loading...