Nobel ya Amani 2019 yaenda Ethiopia huku Tanzania ya Magufuli ikiambulia patupu!!!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Juzi Kamati ya Uteuzi ya Washindi wa Nobel ikiwemo Tuzo ya Amani kutoka Sweden imemtangaza Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Abiy Ahmed kuwa ndiyo mshindi.

Nilitegemea Rais Mhe. Daktari John Joseph Pombe Magufuli angelitunukiwa moja ya Tuzo hizo kwa Sifa alizojizoelea kulingana na Wana CCM. Kwamba angeambulia hata ya Uchumi kwa kutamba kwamba ameiweka Tanzania kwenye Ramani kwa sera zake za Ufisadi, Ujenzi wa Viwanda na Sera za madini,ujenzi wa SGR na Bwawa la Stieglers lakini kwa masikitiko si Magufuli wala Waziri wake Mkuu au Waziri yeyote. Wote wameangukia pua...!!

Ukiwauliza CCM watadai hizo Tuzo zinztolewa na Mabeberu. Ni ile hadithi ya Sungura ya SIZITAKI MBICHI HIZI.
Karibuni kwa mjadala



1570872342901.png

https://www.nobelprize.org/nomination/peace/
 

Attachments

  • 1570871250695.png
    1570871250695.png
    13.7 KB · Views: 1
JPM atapewa tuzo mwakani mwezi wa kumi wakati wa uchaguzi, anachoendelea kukifanya nchi nzima ni kuweka sawa mazingira ya kuibeba hiyo tuzo.
 
Hata kumfikiria kwenye tuzo hiyo hawathubutu, huyu huyu anaewaita mabeberu wampe tuzo? Apewe tuzo kwa kugawa hela barabarani labda.
 
Hatuhitaji akili za mabeberu kujua ubora wa Magufuli
Sisi tutampa tuzo Wananchi tutampa tuzo kwa sababu anafanya Kazi kubwa sana

Mwalimu Nyerere once said,'' Tanzania is not an Island.."
Tanzania siyo Kisiwa maana yake ni kwamba Tanzania lazima iwe na utangamano(Intergration) na nchi zingine. Hilo ni pamoja na Rais wake na nchi kuwa na mahusiano na Marais wa nchi zingine zikiwemo Taasisi za Kimataifa kama UN, WHO,UNESCO,nk.

Kuna faida gani kuwa na Rais anasifika nchini kwake tu ilhali dunia nzima inamwona kituko na mwendawazimu fulani aliyejitenga na Jumuia ya Kimataifa? Rais bora ni yule ambaye ana EXPOSURE katika Mataifa na Taazisi za nje. Ndiyo maana tunasema Magufuli siyo saizi ya Mwalimu Nyerere maana Baba wa Taifa dunia nzima ilikuwa inamtambua kiasi cha kumsikiliza hoja zake za kupigania Uhuru Kusini mwa Afrika. Mwalimu alikuwa akienda UN kutetea hoja za Uhuru wa Afrika Kiuchumi, Kisiasa na Kijeshi. Huyu Magufuli atajulikana wapi sanasana ni kutoka Chato, Dar, Kigali na Kampala kwa maswahiba zake..!!!
 
Mwaka gan iliambulia chochote ?

Huyu Magufuli wenu si ndo mnasema aliyoyafanya kwa MIAKA 4 ni makubwa kuliko yaliyofanywa na Marais wanne(4)ndani ya MIAKA 55? Kama kweli amefanya wonders(vi-wonders) kuliko wote kwanini basi asipewe Tuzo mojawapo ya Nobel?
 
Wasiojurikana kutopatikana na lissu kukayangia huko kwa mabeberu ndivyo vilivyo muondolea sifa mwamba wa chato
 
Nani ampe magu nobel,? Labda zitoke nobel za udikteta awekwe kundi moja na Kagame, Nkurunzinza na Mu7 na Asad wa syria
 
Huyu Magufuli wenu si ndo mnasema aliyoyafanya kwa MIAKA 4 ni makubwa kuliko yaliyofanywa na Marais wanne(4)ndani ya MIAKA 55? Kama kweli amefanya wonders(vi-wonders) kuliko wote kwanini basi asipewe Tuzo mojawapo ya Nobel?
Unaelewa maana ya"TUZO YA AMANI" ?
 
Nadhani kilichotuangusha ni lile sakata fujo nchini South Africa...

Tanzania kama mwenyeketi wa SADC hatujafanya lolote wala kushawishi chochote...



Cc: mahondaw
 
Hatuhitaji akili za mabeberu kujua ubora wa Magufuli
Sisi tutampa tuzo Wananchi tutampa tuzo kwa sababu anafanya Kazi kubwa sana
Mleta mada alishatabiri...



Ukiwauliza CCM watadai hizo Tuzo zinztolewa na Mabeberu. Ni ile hadithi ya Sungura ya SIZITAKI MBICHI HIZI.
Karibuni kwa mjadala
 
Lengo lako ni nini hasa. Yani JF inanifanya muda mwingine nione siasa ni upuuzi. Ni kivipi Tanzania ilitakiwa kuhusika na Nobel peace prize kwa miaka hii ya karibuni. Kwamba tumesuruhisha mgogoro mkubwa,tumeokoa jamii flani iliyokuwa kwenye vita au nini hasa. Mkiwa mnapenda siasa msiwe mnaacha akili na kutumia ushabiki
 
Back
Top Bottom