Tanzania ya viwanda ilikuwa ya CCM au Magufuli binafsi?

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau wakati utawala wa awamu ya 5 unaingia tena kwa mbwembwe nyingi tuliambiwa awamu ya 5 ni ya kujenga viwanda 100 kila mkoa. CCM nayo ililipigia kelele nchi nzima na kuliweka kwenye ilani yake na kuagiza viongozi wake nchi nzima walisimamie.

Baada ya tangazo hilo waziri wa Tamisemi wa wakati huo mh. Jaffo alizunguka nchi zima kuhakikisha viwanja vya viwanda vinatengwa na ujenzi kuanza ili kutengeneza ajira kwa wasomi wetu na kuinua uchumi. Lakini mpaka leo hatujawahi kutangaziwa ni viwanja vingapi vimepimwa na viwanda vingapi vimejengwa kwa kila mkoa na ni viwanda vya nini. Kelele za Tanzania ya viwanda zilianza kupungua kila siku mpaka leo ni awamu ya 6 hazisikiki kabisa utadhani hakujawahi kuwa na tangazo hilo.

Tunawaomba wahusika watuambie iwapo ile sera ya Tanzania ya viwanda je ilikuwa ya mtu binafsi ambaye ni Magufuli au ya CCM na kama ni ya CCM mbona CCM ipo lakini Tanzania ya viwanda haisikiki tena?
 
Back
Top Bottom