Noandoka Tanzania

Noandoka Tanzania

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,265
Reaction score
4,452
Naondoka Tanzania,

Hivi sasa naelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yangu hii. Nimeacha mke na watoto pamoja na wazazi ambao natarajia watanifuata baada ya mwezi mmoja kwani naenda kuwaweka sehemu salama zaidi na ambayo wanangu watakuwa na haki ya kuota ndoto.

Nirudi kwenye sababu za kuondoka;

Kwanza niseme sababu ya kwanza ya kuondoka na kwasababu ninao uwezo wa kuondoka, pili kwa kweli uzalendo unanishinda na naona kabisa kuwa kadiri siku zinavyoendaelea nazidi kuichukia nchi yangu, kuwachukia viongozi wangu, kuwachukia aia wenzangu na hata kujichukia mwenyewe.

Najisikia vibaya kwani sasa nina mashaka na wasi wasi wakati wote, naona aibu kuwa Mtanzania.

Ubaya mkubwa ni ukweli kwamba tayari nchi yetu imeshapiga magoti, wananchi wamekata tamaa, taifa limepoteza mwelekeo na hata sasa ukimuuliza hata Rais wetu ni wapi anakopeleka nchi yetu hana hata jibu dogo analoweza kukupa bila kujiuma uma na kuchanganya mambo.

Sijui tulikosea wapi, sijui turekebisheje ila kwa wale ambao tunaweza kuondoka basi tuondoka, nyumba na mali zangu zote nimeweka kwa madalali waziuze ili pesa hiyo itusaidie kwenda kuanza maisha mapya mimi na familia yangu.


Ee Mungu utusaidie
 
hongera mkuu,ila kuuza nyumba sikushauri,usidhanie ukiuza utaishi peponi,hela shilling haina thamani mbele ya dollar au pound,unacheza pata potea mkuu unless ni hela nyingi utapata ukiuza hizo nyumba kiasi cha kukuwezesha kuinvest huko uendako...............
 
hongera mkuu,ila kuuza nyumba sikushauri,usidhanie ukiuza utaishi peponi,hela shilling haina thamani mbele ya dollar au pound,unacheza pata potea mkuu unless ni hela nyingi utapata ukiuza hizo nyumba kiasi cha kukuwezesha kuinvest huko uendako...............
Naedna kuanza maisha mapya at any cost,N itabakiza nyumba ya urithi kwa sababu za kiutamaduni ila nilivochuma kwa hela yangu vyote nauza niende nikabebe maboksi na kusafisha choo ng'ambo nikiwa na amani moyoni sio kukaa kwenye nchi ambayo inatia kichefuchefu na kuhara wakati wote
 
umetumiwa nauli na mange?? husubiri hiyo trh 26??
Sijaona sababu ya kuandama kwenye nchi ambayo haina maana sana sana wataniudhi halafu nitaharibu maisha yangu na watoto wangu wakati dunia ina nafasi sehemu zingine.Waandamane wale ambao hawana pa kwenda ili wahakikishe nchi inaenda sawa.Wasipoandamana wataandamanishwa
 
ubongokid
Ndio maana ukawa expert member jf kwa uhodari wa kutunga uonga!Ungeweka ticket ya safari ungeaminika kidogo
 
Back
Top Bottom