Noah Voxy zina uimara kiasi gani?

Noah Voxy zina uimara kiasi gani?

Vp salama wakuu.

Kuna mtu flan anataka kuniuzia Voxy 2006 kwa 7mil,

Me siyo mtaalam sana wa magari,so naomba wenye uelewa wanipe elimu kidogo kuhusu Voxy.
Matumizi yangu ni kubeba abiria na njia ni rough road na mahali pengine ni lami.

Sasa naomba kufahamu uimara wa hii gari na changamoto zake.
Hamna kitu ni laini hatari mabati yake ni kama ya kopo la reblue
 
Barabara yetu ni full mkeka tarakea -moshi
Kwa barabara ya vumbi anunue gari za kazi e. g. Tata.
Huko kweli tena kunahitaji gari za petrol zaidi maana kupanda nako mtihani, Moshi / Marangu kumenoga sana kwakweli.
 
Kama ina engine ya D4 jiandae kuzijua garage zote.

Ugonjwa wake mkubwa ni kwenye sensors na kuwasha taa ya "Check Engine"
 
Ila kwenye magari Wabongo tunatishana sana. Kuna wakati nilipitia uzi fulani wa kuhusu magari, kuna watu walisema gari zenye injini ya D4 hazifai na zinasumbua sana!

Cha kushangaza hapa nilipo nina gari ya Muingereza! Tena ni ya kumvua mtu, injini yake ni D4 hiyo hiyo!! Gari haijawahi kunisumbua kwa chochote! Popote inafika! Haichemshi! Haina sijui mis! Yaani maelezo ya baadhi ya watu na uhalisia, ni vitu viwili tofauti.
 
Vox jamaa mmoja alikua anabeba wanafunzi tena wa darasa la kwanza wachache tu alifanya hiyo kazi asubuhi na mchana mwezi tu gari ikawa inagonga kila sehemu kama excavator hela kachukua punda kagoma kwenda ikabidi akaazime Noah Sr 40 kwa mwana mmoja nae hivyo hivyo nimepigiwa simu gari ipo moro wanataka 5m sasa hivi hataki hata kuiangalia..
 
Kama hujanunua
Udhauri wa bure achana nayo
Unless the deal is good ukaweza kupotezea comments
Ntaongelea kwenye engine pekee
Voxy zina 1AZ
Hii engine ina challenge za kutosha
Fuatilia reviews online
Then fanya maamuzi on it.
 
Back
Top Bottom