Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,323
- 67
Nadhani hii mada ni pana sana.Ila naona 50/50 representation bado ni ngumu kwa sababu kadhaa, lakini nitadokeza mojawapo ya sababu ambayo naona ni kubwa...50/50 gender balance?...sounds like affirmative action!
..kitu cha muhimu ni kwa wakina mama wenyewe kujibidiisha kuondoa tabia iliyopo miongoni mwa wengi wao ya kungoja kupokea!watafute!watapata!hasa katika nyanja za shughuli za maendeleo!
..tukilenga kufanya mlinganisho wa lazima tutakuwa tunakosea!kitu sahihi ni kushawishi,kusomesha,na kuwawezesha kina mama kujitegemea zaidi!
..it must be a cultural revolution!
1.Majukumu/matazamo wa familia
Akina mama ndiyo wana reproductive potential.Hili ni jukumu muhimu sana na linachukua sehemu kubwa ya muda wa akina mama katika ujauzito na malezi,hivyo kubaki nyuma katika masuala ya kazini, particularly kwa zile office ambazo ni labor intensive.At the end of the day wanabaki nyuma katika promotion pia.
Kuna evidence kwamba good number ya wanawake wanaogangamaa na ofisi, wanajikuta nyumba zao zinayumba kwa namna moja au nyingine au kusambaratika kabisa. Hivyo inabidi waegemee zaidi upande wa pili..kama mama lao alivyoiweka kwamba cv wanazo "lakini wanazilalia".
Nadhani wengi wamenafuatilia ktk nchi za wenzetu ambapo kuna declining population growth, sababu kubwa ni kazi.Kwamba mtu anasacrifice familia kwa kazi, maana viwili hivyo vinakinzana na kwamwe haviendi pamoja.Baadhi ya nchi zilizoathirika zaidi kwa hili ni ujerumani na sasa hivi japan.
Labda kwa nchi kama yetu,yaya anaweza kuchukua nafasi ya mama,hivyo akajizatiti zaidi kazini. Lakini sina uhakika akina mama wanalichuliaje hili la yaya kuchukua jukumu la malezi ya familia.
Kabla ya kuendelea na sababu nyingine ningependelea mama lao et al mtupe mwanga kwenye hili kwanza.