No rush on graft cases, says JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

No rush on graft cases, says JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invisible, Dec 17, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  The Daily News
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  No rush.....no rush..... no rush. Now the projection is that all these graft cases will end after 2010 when all the defendats will enter nolo contendere.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mama hapo juu kasema kweli, hii ni janja ya nyani kwani kesi hizi za hawa mafisadi watazivuta mpaka uchaguzi wa 2010 halafu kila mmoja wao ataachiwa!! Hawa jamaa wanatupiga madongo ya macho watawapandisha kizimbani wengi tu halafu watawaachia; hata GOLDENBERG ya Kamlesh Pattni aliyetumiwa na moribund KANU kuiba Benki kuu Kenya Kesi yake ilivutwa mpaka mwisho ikafutwa. Muungwana ajue tu kuwa tunajua mbini zake asitufanye mabwege.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna mengi yanaonekana kuwa bado yanafichwa. Kwanini Mramba, Yona na Mgonja wanafunguliwa mashitaka ya kulitia hasara taifa tu. Mbona EPA hawasemwi? Mramba, Mgonja wanaconnection nzuri sana na EPA. Mashitaka waliyofunguliwa hukumu yake itakuwa ni ya kuchekesha sana, tutapigwa bao mpaka tutajicheka kesi yao inaweza kuendeshwa kwa miaka 20 na hukumu inatolewa wakiwa na matatizo ya kiafya, halafu wanatumikia kifungo cha nje.
  Trick yote ya kuwafikisha hawa jamaa mahakamni zaidi ni kuwa-fool international community ili wazidi ku-pump hela Tanzania halafu walaji waendelee kuila, na dalili zinaonesha kuwa wameingia mkenge ni kama wanataka kuendelea kutoa hela, hao ndio audi zetu kwa sasa.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Rais wa nchi anasema watu maarufu wachukuliwe kwa uangalifu zaidi mbele ya vyombo vya sheria ili wasije kuchafuliwa!

  Ni Tanzania tu ndio unaweza kusema hicho kitu, lakini nchi za wengine ungetoa tamko hilo watu wangeandama na mabango mpaka jumba la Rais kumtaka awapishe!

  Haelewi misingi ya "equal protection" na "due process" of law.

  Mtu yeyote yule anaeingizwa katika mkondo wa sheria na kuanza kuchunguzwa, kushitakiwa, kutwikwa gharama za kujitetea, kulazimika kujitafutia njia za dhamana, kuanikwa nyeti zake mahakamani, kupoteza kazi kabla hata ya matokeo ya kesi, haya yote ni mzigo ambao hakuna anaetaka kuubeba. Uwe mstaafu waziri au mshutumiwa wizi wa ng'ombe, hakuna anaependa.

  Kwa sababu ya kuhakikisha kwamba mtu hata sokomezwa katika mkondo wa sheria bila hiana, na bila vidhibiti, na bila haki, na bila nafasi ya kujitetea, watu wa jamii zote zilizo staarabika wakajiwekea msingi wa uendeshaji sheria unaoitwa, kwa lugha ya common law ya mwingereza, "due process of law." Katika katiba yetu msingi huo umesimikwa katika Ibara ya 15, kwamba huwezi kukamatwa kamatwa ovyo tu bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo shuku ya msingi iliyotokana na uchunguzi yakinifu kutafuta vidhibiti vya makosa. Ni vizuri Kikwete anakiongelea hiki kitu manake siku zote kimekuwa kikidharauliwa, toka enzi za watawala wa nyuma, za vinara wa uasisi wa nchi yetu. Maana watu waliswekwaswekwa kwenye vyumba vya giza na hewa isiyotosha bila sheria. Siku wakitolewa baada ya miaka wanakuwa tayari wana magonjwa ya vifua, wanakaa kidogo wanakufa. Humo kizuizini hakuna cha kupewa daktari, achilia mbali "due process."

  Lakini muhimu ni kwamba pembeni ya "due process" kuna msingi-dada wake mwingine unaofuatwa na jamii zote zilizopevukia haki, na katika katiba yetu unaoitwa, kwa lugha ya common law "equal protection" of law, ambao katika katiba yetu umechimbiwa katika Ibara ya kumi na tatu:

  ``Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria...Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.``

  Huwezi - ni dhambi ya asili katika misingi ya haki - kusema kwamba tunapotaka kumchunguza waziri mstaafu Andrew Chenge, au mwanasiasa mfadhili Rostam Aziz, au mstaafu mkuu wa wakuu, Benjamin Mkapa, basi hawa uwachukulie kwa makini zaidi ili wasije chafuliwa jina. Lahasha!

  "Due Process" inaenda sambamba na, na inajumuisha, "Equal Protection."

  Unaposema utakuwa mwangalifu zaidi unapomchunguka kiongozi eti usimchafulie jina kuliko unapomchunguka mwizi wa mtaani ina maana mtu wa kawaida yuko chini ya mfumo tofauti wa sheria.

  Sasa kama tunataka kuwa na mifumo miwili ya sheria basi ingeleta mantiki kama tungepindua mambo juu chini tukafanya huyu kiongozi msadikiwa wizi huyu ndie tungemburuza ovyo ovyo kumharakisha kumpatia adhabu bila umakini wa uchunguzi maana huyu ndie alipewa dhamana ya wananchi na taadhima ya jamii, uwaziri mkuu, ukatibu mkuu, uamiri jeshi mkuu. Isitoshe, huyu anasadikiwa kuiba mabilioni wakati mwenzake ana kesi mbuzi ya kuiba kuku!
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikwete kashawahi kusikia the concept of "equal protection under the law"? Mimi nilifikiri kila mtu anatakiwa kuhukumiwa kwa umakini, au ndiyo mambo ya the Orwellian equality kwamba "everybody is equal, but some are more equal"?

  Rais anahitaji msaada wa kupigwa msasa on some basics za civics and governance.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  What happened to Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!?
   
Loading...