kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,247
- 16,169
Usalama kwanza
Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.
Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.
Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.
Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.