No Doubt HG wangu ana ujauzito! Nishaurini

No Doubt HG wangu ana ujauzito! Nishaurini

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
486
Dah WanaJF
Yaani haka kasafari ka siku chache tu nimerudi nimekuta balaa!
Tulikuwa na kasafari kadogo na mamsap! Juzi kati nimerudi home nikapokelewa na malalamiko kibao!
Wa kwanza Sijui nimwite HOUSE BOY anyway mmenielewa! Eti dada siku hizi hapiki na akiuliza chakula tu atatukanwa ile mbaya. Mbaya zaidi anatematema mate hovyo na hii inampa kazi kubwa sana ya kufanya usafi! Huyu mvulana ndo kazi yake kufanya usafi! Pia HG analala mida yote!
Wa pili ni binti yangu mdogo wa miaka 11. Ananambia kuwa anapewa kichapo karibia kila siku tena na makovu akanionyesha. Kisa dada (HG) hataki usumbufu!
Tukaanza kufanya uchunguzi. Taarifa za ma- informers wetu zinawahusisha mdogo wangu mmoja na vijana (Watoto wangu) 2! Kila mmoja baada ya kubanwa kivyake bila kujua kuwa tulisha wahoji na wengine wamekiri kuwa wameshawahi mara kadhaa kuonjeshana na HG wetu. Kwa hiyo hapa kuna vidume 3.
House Girl tulivyomhoji hakubisha wala kukubali alibakia kimya. Alipoambiwa ana MIMBA akang'aka kwa ukali kuwa hana mimba! Leo hii saa hii my waifu wangu kamtoa kwa dakitari na ni confirmed kuwa ana mimba ya miezi 2. Sasa ni ya nani ndo kasheshe!
Hebu nishaurini sasa tufanyeje.
Ni ushauri tu unahitajika!
 
Sasa tukushauri nini mama mjamzito si anaelekezwa clinic au
 
Hapo kazi ipo! Ngoja aje mtaalamu wa mambo hayo @lara1 akupe mpango mzima! Duh ila kiukweli kazi unayo mkuu.
 
Mpe matunzo mazuri huku ukijiandaa kupokea mjukuu
 
shemeji @Lara1 ukuye huku. , .platinum advice highly needed.
 
Subiri mtoto azaliwe hilo zigo umkabidhi mhusika maana inaoneka huyo HG alikua tetee wa kuazima, hadi mtaa wa jirani anapelekwa ili mradi akaatamie tu mayai ya kuku wenzie....
 
Mkuu umetaka ushauri na mi nakupa kama ifuatavyo:
Muite mketishe chini mumweleweshe kua mmeshampima na ana ujauzito wa miezi 2. Kwa hiyo suala la yeye kukataa ukweli mwambie aachane nalo.
Pili aelezee kinagaubaga amelala na watu wangapi. Hapo ndani kwako katika kipindi chote tangu ameanza kuujua mpipi. Cha msingi umjue mhusika ambae ni mkuu aliyekua analala nae mara kwa mara ili muestablish a coincidental likelihood of a father.
Kinyume cha kusema ukweli huo mumwambie safari yake ya kurudi kwao kijijini inaiva hapo hapo.
Na akikataa mpaka ukamilifu wa dahari huna budi ya kumpeleka mguu kwa mguu hadi kijijini kwao uklipomchukua (kama ulimchukua kweli)
Anza na hayo machache kisha leta mlishombele.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Umeonae? Yanini kuumizana vichwa na mkubwa mwenzio?

Si ndo hapo sasa, kangekuwa katoto ka praimare hapo sawa!
Hataki . . . basi akasemee kwao.

Mitu mingine bana,
Mpaka hapo anatarajia labda ni tofali ataenda kuuza kwa wajenzi?
 
Si ndo hapo sasa, kangekuwa katoto ka praimare hapo sawa!
Hataki . . . basi akasemee kwao.

Mitu mingine bana,
Mpaka hapo anatarajia labda ni tofali ataenda kuuza kwa wajenzi?

Dah kweli mkuu sijaona mtu mbishi ka huyu. Tumemwambia tunamrejesha kwao na hivi niongeavyo safari ni kesho. Ifikapo saa saba mchana atakuwa pale Singida stendi.
 
Dah kweli mkuu sijaona mtu mbishi ka huyu. Tumemwambia tunamrejesha kwao na hivi niongeavyo safari ni kesho. Ifikapo saa saba mchana atakuwa pale Singida stendi.

kumbe wa singida!!!!!!!
 
Back
Top Bottom