No dancing girls for the election?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Mnamo tarehe 27 mwezi Mei magari ya kikundi cha TOT ambacho hutumbuiza wakati wa kampeni kwa upande wa CCM (chama tawala) yalikamatwa an Majembe Auction Mart kufuatia order kutoka mahakamani.

Mtafaruku huo ulikuja baada ya Benki ya wananchi wa Dar es Salaam (Dar es Salaam Community Bank) kuwafikisha TOT mahakamani kudai deni lao ambalo limechukuliwa muda mrefu sasa la Tshs Milioni 30.

Mkurugenzi Mtendaji wa Dar es Salaam Community Bank ndugu Edmund Mkwawa alikiri kuwepo kwa kesi hiyo na kuwa benki inajaribu kurejesha madeni ambayo yamekaa muda mrefu bila kulipwa ambayo alikopeshwa Mkurugenzi wa TOT Kapt. Komba rafiki wa karibu na rais mstaafu Benjamin Mkapa na kuwa anawachezesha danadana.

Suala hili lilienda mbali na kumfikia Mzee Makamba ambaye ni katibu mkuu wa CCM ambaye hakuchukua hatua madhubuti kusuluhisha hivyo DCB kulazimika kulipeleka kortini ambako ndiko kulitolewa ruksa ya DCB kuyakamata magari ya TOT kupitia Majembe Auction Mart.

Sasa, suala hili limefikia wapi? Naamini tuna waandishi ambao wana access ya information hii ambao wanaweza kutujuza; maana endapo magari ya TOT yataendelea kushikiliwa kuna uwezekano kampeni za JK zikakosa wanenguaji wa TOT kama ilivyozoeleka (na huisaidia sana CCM).

Ikumbukwe kuwa; miaka mitatu iliyopita (mwaka 2007 mwezi Novemba) viongozi wa ndani wa CCM waliwahi kumjia juu Kapt. Komba kwa madeni ambayo aliwaingiza bila kutarajia (US$ 30,000.00) ambayo wao (CCM) walilipia mwezi huo wa Novemba kuweza kufunika kombe. Kapt. Komba alidai zilikuwa ni njama za kumchafua kisiasa!
 
Mhhh .........hapo pia litafunikwa tena, au kwenye hiyo auction ya magari wanaweza kuyanunua tena hao hao ccm.

makelele ya komba kwenye kampeni wenyewe wanayajua kuwa ni ya lazima katika ku brainwash vichwa vya watanzania
 
CCM wana mkono mrefu unaoweza kuisagasaga MAJEMBE na DCB kirahisi kabisa!...Time will tell!..

Lets keep our ears wide open pindi kampeni zikianza utaliona mtaani hata kama watakuwa hawajalipa deni la watu!....Na kipindi hicho kutokana na jinsi watu wanavyojipendekeza utastukia roSTAmu mmoja akalipia deni lote!
 
hehehe!invisible hiyo taito ulivyoiweka dah!ibedilishe kidogo bwana!imekaa ki-uchokozi zaidi(naongea kama mpiga solo wa T.O.T)
ningekuwa painkiller ningekupa ban ya siku mbili
 
CCM wana mkono mrefu unaoweza kuisagasaga MAJEMBE na DCB kirahisi kabisa!...Time will tell!..

Lets keep our ears wide open pindi kampeni zikianza utaliona mtaani hata kama watakuwa hawajalipa deni la watu!....Na kipindi hicho kutokana na jinsi watu wanavyojipendekeza utastukia roSTAmu mmoja akalipia deni lote!
You know what? Hapo kwenye RED ndipo watanzania mnapoharibu,,, hakuna chama cha kujigamba kuwa na mkono mrefu! Watanzania ndio wanatakiwa kubadilika na kuweza kuchukua maamuzi ya kumwadhibu yeyote anayejifanya kuwa na mkono mrefu, aidha kwa amani au .......
 
Kwa bahati mbaya sana sisi Watanzania hatuna muono mmoja kuhusu mustakabali wetu hasa wa muda wa kati na mrefu. Bado wengi wetu tuna hulka ya kuwaabudu badala ya kuwadhibiti walioshikilia nyenzo za uchumi.
 
You know what? Hapo kwenye RED ndipo watanzania mnapoharibu,,, hakuna chama cha kujigamba kuwa na mkono mrefu! Watanzania ndio wanatakiwa kubadilika na kuweza kuchukua maamuzi ya kumwadhibu yeyote anayejifanya kuwa na mkono mrefu, aidha kwa amani au .......

And fun enough huu the so called 'mkono mrefu' siku zote uko too selective!
 
Back
Top Bottom