Jiwe la msingi lililowekwa na mchezaji wa soka mashuhuri Lionel Messi pamoja na rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon katika uzinduzi wa uwanja wa mpira utakaotumika kuchezwa mechi za fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017, limepotea na halijulikani lilipo hadi sasa.
Jiwe hilo la msingi liliwekwa Jumamosi iliyopita na mshindi huyo wa tuzo la mchezaji bora duniani, akiwa na rais Bongo katika mji wa kusini mwa Gabon Port-Gentil
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.