Nmekutana nae tsaap group tukapendana haswa.

Tushfutshtar

Senior Member
Joined
Dec 30, 2017
Posts
117
Reaction score
112
Habari zenu wadau!

Kama kichwa kisemavyo, nilikutana na binti kwenye group la WhatsApp tukaahidiana kukutana na ikawa hivo,nilijikuta nampenda sana na yeye mwanzo alionesha ana nipenda sana lakini baadae akawa MTU mwenye ratiba zisizoeleweka hadi mawasiliano yakaingia DOA na nikawa MTU wa kulalamika sana hadi nikataka kukata tamaa!

Nikaamua kumpima imani na UPENDO wake kwa kutumia namba nyingine kwa ujumbe uliosema "wewe achana na mpenzi wangu venegrade" (sio jina halisi) daaahh siamini vile mwenye namba ile alivyosumbuliwa na huyu dada kwa kweli ,kumbe ananipenda sana hadi juzi nimetoka kwake aliniita kwa kesi hiyo nikamwambia ukweli kwamba nilikuwa nampima ila tukayamaliza baada ya yeye kujiridhisha!

Kuanzia juzi simu na text zake hazikatiki hadi nmeanza kuona impacts za ule mtego wangu japo nilikuwa na wasiwasi angeniona mm sio mwanminifu na kuniacha, nampenda nimeamini kupendana ni popote asee!

Naomba kufahamu nje na uelewa wangu na uzoefu pia, kuna nini kinaweza tokea endapo nitaamua kuwa nae hata kumuoa kabisa ikiwa tumekutana mtandaoni?

Mawazo yenu wadau!
 
sio issue
 
Ni sawa pia nani kama kwa wanaokutana mashuleni, ofisini, kanisani, mtaani na sehemu yoyote maadam sio ndugu yako
 
Sawa mkuu !

Bad au Good kivipi labda maana kwa mwonekano yuko poa tu ananifaa mm nimeridhika ila kitabia ndo bado Nina % chache tu maana tuna mda mfupi kiasi
OK kwanza vzuri ,, nahongera kwakumkubali maana iko ndo muhimu.

Sasa Basi kuoa nimtu unayempa maisha yako yote ,atajua madhaifu yako na mazuri ..kwaufupi nimtu unayempa yote yaliyoyako.

Sijui nimuda gan toka muwe pamoja..... Ila Wenda ulimtongoza nakumwambia *Nitakuoa* ndo maana ameamua kua mwemaaaaaa kwako..

Ivo embu jipe Muda ,jiridhishe ,kisha muoe.. Achana na *Mwonekano tuu mkuu* soma moyo wake.

Utaoa sababu ya mwonekano ,,mwezi mmojw unagundua demu ni kiguu nanjiaaa ,hataki kukosa singeli mtaani ,,madela haishiii.

UTAANZA KUJIONGELESHA HATA CHOONI KM KICHAA!!.
 
Sasa unataka sisi tukwambie nini mkuu!! Wewe ndio unamfahamu huyo binti, na ndio unajua kama mnapendana au la!! Kuanza kuhangaika na ushauri kwa vitu ambavyo havihitaji ushauri tena kwa mwanaume ni kuonyesha ni jinsi gani haujui nini unataka.

Jiulize moyo na nafsi yako vinakwambia nini then go for it.
 
Maisha hayana user manual kwamba mahusiano yakianzia nyumba ya ibada itakuwa hivi au yakianzia mtandaoni itakuwa vile.

Weka viwango vyako jiridhishe vimefikiwa/vitafikiwa basi baada ya hapo endelea na hatua zingine.
 
Nikiwa na jambo nitakuwa napitisha kwako kwanza mkuu ili uchambue kama lafaa kwa kuomba au kutoomba ushauri!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…