Nmechanganyikiwa sielewi nifanye nini.

Nmechanganyikiwa sielewi nifanye nini.

Habali zenu,
Mimi ni mwanamke mwenye miaka hiyo wakati nipo chuo nilikuwa na boyfrend baadae tukawa kama tunamis understantanding fulani hivi sijui ni kwasababu ya umbali anyway, basi mimi nikapata boy mwingine akaja home na akafata taratibu zote bahati mbaya kabla ya ndoa nikashika mimba kabla ya kufunga ndoa kuna mambo yakatokea katikati ikabidi nijifungue kwanza ndo tufunge ndoa.

Nikajifungua salama na maisha yakaendelea kama kawaida,ikiwa tunafanya process za ndoa sielewi nini kiliingilia kati yetu ukweli nashindwa hata kuelewa tulitofautina kwenye simu kama mnavojua mapenzi ya mbali basi yule bwana akakomoa kuwa basi na uhusiano uishie hapo kwa kweli sikuamini kilichotokea wazazi pande zote waliingilia kati wala hakutaka kunielew nilijitahidi kumpembeleza alikataa kata kata fikiria hapo na mtoto mdogo, basi ndugu zake wakawa wananifariji hatimaye nikawa normal.

Nikaendelea kulea mwanangu ila hakuacha kumjulia hali mtoto na kutoa support zote kama kunatatizo hata ndungu zake pia hasa wazazi wake hawa kuwa mbali na mimi kunijulia hali,basi nikazoea.

Sasa yule boyfrend wangu wa mwanzo kama 4yrs imepita akaanza kunitafuta nikamwambia kila kitu kinachoendelea baada ya kuniuliza social life yangu ya mapenzi nikamwambia kuwa na mtoto na blal blah nyingine alisikitika sana ila akakubali hali halisi baadae akawa ananiuliza vipi mbona upo home hujaenda kwako ikabidi nimwambie ukweli wote, akakaa kama miezi 6 then akanambia ooohh tuludie na nini na nin nikakataa badae akanisisitiza akaniambia usijari kuhusu mtoto siwezi kumuhukumu kutokana na historia yetu nikaona isiwe shida nikakubali ila nikamuuliza vipi kuhusu yeye akadai toka tulivoacha 4yrs ago hajaoa wala hana mtoto nikaacha kama yalivo.

Kweli nikaenda kwake hakukuwa kama siku mbili nikarudi alikuwa anaishi mwenyewe, sasa yupo kwenye process za kutaka kuja home ndo hapo utata ulipo nikapata habali ana mtoto nikamuuliza akasema ndiyo ila hakutaka kuniambia sababu ananipenda ningekataa kuoana naye.
nipo njia panda nataka kusitisha zoezi lake la kuja home kwanini hakuniambia hapo mwanzo hadi wengine wanambie?
Ushauri jamani tafadhali

nimekutukana we huna haya,,,,,tusi,,,hv huo wivu wann we mbn umetaga?,,,,,,,,tusi,,,,,,,,ujinga wako mpelekee mama yako ,,,,,,,tusi
 
dah hii yote inatokana na tamaa ya kutaka kuolewa !!!!hapo inaonyesha hujachagua mwanaume wa aina ipi unamtaka bf wako wa mwanzo alipropose twende huyu wa pili twende wa mwanzo karudi tena twende mhh akirudi tena huyu wa pili nahisi utachanganyikiwa zaidi.... ushauri wangu angalia moyo wako inataka nini,ukiona humuamini achana nae ukiona bado uuna feelings nae na unampenda mkaribishe home
 
mhhn!
hiki ni kituko kingine kwa kuwaleo lunch siendi kwa ajili ya mfuko ngoja nijaribu kama naweza kusema chochote wakati napunguza njaa.
kwa harakaharaka wewe ndiwe mwenye matatizo zaidi kuliko wanaume wote wawili. unaonekana ni mtu unahisi kuumizwa na unasikia raha kulialia kwa kuwapa wengine lawama. lakini lililobaya zaidi ni mwepesi kujiachia na kumwamini mwanaume kwa haraka sana.
katika simanzi hii ya kulalamika kudanganywa nauhakika akitokea mwanaume aliyepanga mistari vizuri na akahaidi kukuoa basi na wewe unahama kwa huyo mwanaume wako.
huna maamuzi katika mambo yako mwenyewe na hasa mahusiano ki ukweli unahitaji kujifunza zaidi.
lakini kumbuka kunatofauti kubwa sana kati ya boyfriend na mchumba. boy friend huwa hajajiandaa kuwa mme na ndio maana uhusiano unaweza kufa wakati wote kwa kuwa hajaweka mawazo yake kwako kwa kiasi kikubwa ni mechi za mchangani zisizo na ligi.
sasa nini ufanye
kwanza kubali kuwa unamapungufu katika hili
jua mahitaji yako nini unataka mme/boyfriend
tazama asilia yako umelelewaje, nafsi ya familia katika kuolewa ikoje na mapungufu yako yakoje
kipi unaweza kurekebisha kipi uwezi na unafikiri unaweza kujifunzaje ili uweze kikusaidie uwe mke mzuri
ukiweza mshirikishe huyo uliezaa naye aliona nini mpaka akaghaili ili urekebishe upokuwa na mwanaume mwingine haya yasitokee ili uweze kulea mtoto wenu vizuri.
la muhimu zaidi mshirikishe MUNGU zaidi katika kukusaidia katika hili.
pole maneno ni makali njaa nayo inachangia
lakini huu ndio mchango wangu

nashukuru kwa ushauri
 
Subiri nikwambie kitu mpenzi, do u knw that shetani yupo kazini eeh!ss hapo alipokuacha bila sbb ndo ujue there s somthing,trust mi its satan,kuna kitu kwny hyo couple yenu, ndo maana satan ameharibu bcoz satan anachofanya ni ku-hold u a destiny/future, na njia anazotumia ni nyingi, ss km sio mtu wa rohoni/imani ni ngumu kuelewa nachokwambia,coz unaenenda kwa jinsi ya mwili
Na always anachofanya ni kuku-kupush kwa mtu mwingine ambae siyo God s will!!...yaani i wish nikukuwekee hii akili yangu!ingekusaidia kung'amua kitu.
nashukuru kwa ushauri wako
 
usikurupuke hapo kukubali, ebu anza naye tena mahusiano kama boy na girl friend ili kuendelea kuchunguza mienendo yake, najua unapenda kuwa na familia ila wakuwa naye ndo shughuli, pili msipende kuzaa kabla ya ndoa endapo yanatoke kama hayo wachache ambao wanakubali kuoa mtu wa hivyo. mchunguze huyo mpk uridhike naye usitumie historia kwani mambo yanabadilika.
 
usikurupuke hapo kukubali, ebu anza naye tena mahusiano kama boy na girl friend ili kuendelea kuchunguza mienendo yake, najua unapenda kuwa na familia ila wakuwa naye ndo shughuli, pili msipende kuzaa kabla ya ndoa endapo yanatoke kama hayo wachache ambao wanakubali kuoa mtu wa hivyo. mchunguze huyo mpk uridhike naye usitumie historia kwani mambo yanabadilika.
unamaanisha nini?
 
Yan huyo ndo mzuri akikuoa analeta yule mtoto na wa kwako wanakuwa watoto wawl hakuna kuzaa tena . Wanatosha hao enough is enough
 
Back
Top Bottom