Hati fungani za NMB

m.agape

Senior Member
Dec 7, 2012
141
79
Habari wanajamvi. Penye wengi hapakosi neno. Nimepata hiyo meseji hapo chini kutoka NMB.

NAOMBA YEYOTE ANAEJUA KUHUSU HATI FUNGANI, ANIPE DARASA KIDOGO.

Ndugu Mteja, faidika na gawio la 9.5% kila baada ya miezi 3 kwa kununua hati fungani (Jamii Bond) kupitia benki ya NMB. Dirisha litafungwa tarehe 27/10/2023
 
Hiyo rate ya 9.5% ni kwa mwaka. Ila unapewa kila baada ya miezi 3

Kwa mfano umeweka 1000,000
Gawio kwa mwaka = 0.95*1000,000=95,000
Gawio kwa miezi 3 = 95,000/3 = 31,600
Ina maana kila mwezi unapata wastani wa Tshs 10,533?
31,600/3 = 10,533
 
Nmekatwa sh 50,000 kwenye account yangu imeomba statement imeandikwa SI IFO then jina nn maana yake? Naomba msaada
 
Ukichukua hati fungani huwezi kutoa pesa zako mpaka muda wa makubaliano ufike. Ukiamua kutoa kabla kuna makato au faida yote itakatwa.
 
Hiyo rate ya 9.5% ni kwa mwaka. Ila unapewa kila baada ya miezi 3

Kwa mfano umeweka 1000,000
Gawio kwa mwaka = 0.95*1000,000=95,000
Gawio kwa miezi 3 = 95,000/3 = 31,600
Gawio kwa kila miezi 3 maana yake wanalipa quarterly..
Yaani 95,000/4 = 23,750

Hicho ndo kiasi atapokea kila baada ya miezi 3..

i.e Tsh 7,917 kwa mwezi.
 
Hati fungani Tanzania uwe na mtaji mkubwa kuanzia milioni 500 ama zaidi.

Imagine ukiweka milioni 100, utapata faida kwa mwaka milioni 9.5 sawa na shilingi laki 790 kwa mwezi.

Fikiria, je ukifingua hardware store ya milioni 100, kwa mwezi utapata faida ya laki 790 tu?

Ama ukiweka milioni 50 Mpesa, kwa mwezi utapata faida ya laki 790 tu?

Kwa msingi huo, hati fungani ni kwa wenye mtaji mkubwa tu.
 
Back
Top Bottom