NMB Bado hawajatii maelekezo ya BoT ya kupunguza Riba kwenye Mikopo

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,132
7,711
Tarehe 27 Julai 2021 BOT ilitoa maelekezo kwa Benki zote nchini kupunguza viwango vya riba kwenye mikopo kutokana na Janga la UVIKO 19.

Benki ya NMB ambayo kwa asilimia kubwa wateja wake ni watumishi wa umma ambao ndio walio pigika kiuchumi Je mpaka leo hii trh 17/9/2021 NMB wamepunguza viwango vya riba ktk mikopo ya wateja wake?

Ieleweke kuwa viwango vya riba vilipaswa vipunguzwe kwenye mikopo ambayo tayari ilikuwepo na pia kwa mikopo ambayo itakopwa baada ya maelekezo hayo ya BOT.

NMB nia yenu ni kuwakwamua wateja wenu au ni kuwadidimiza?

NMB ndio Benki yenye ukwasi nchini kutokana na watumishi wa umma lkn bado haijarudisha fadhila kwao, riba kwa watumishi wa umma ilipaswa ishushwe mara dufu tofauti na wafanyabiashara.

Kazi iendelee.
 
NMB Bank kwa Ukwasi wake ilio upata kutokana na mishahara ya watumishi wa umma kupitia ktk Bank hiyo ilipaswa iwakwamue kiuchumi haswa ktk kipindi hiki cha janga la Uviko19 ambapo kipato kimeyumba.
NMB chukueni hatua maalum.
 
financial institutions haziingiliwi kinyume nyume, BoT, IMF na WB zinakontrol kiasi cha pesa kwenye mzunguko kupitia riba, hisa na hifadhi ya pesa.

crdb walianza kutii maagizo ya ovyo si kwa sababu walitaka bali mkurugenzi mkuu aliahidiwa uwaziri.

upumbavu huo usijirudie tena.

unaetegemea riba kushuka kwa uliefunga mkataba sahau kabisa.

serikali yako imegoma kupunguza loan bodi toka 15 iwe 8 sembuse mwekezaji.

kwa masuali yote ya fedha niulize kifedha na uchumi, sio kisiasa
 
NMB ilipaswa iwe Bank ya kwanza kutekeleza masharti ya BOT kwa sababu ya kuhudumia makabwela.....lkn bila hata aibu nao wamegoma!
 
financial institutions haziingiliwi kinyume nyume, BoT, IMF na WB zinakontrol kiasi cha pesa kwenye mzunguko kupitia riba, hisa na hifadhi ya pesa.

crdb walianza kutii maagizo ya ovyo si kwa sababu walitaka bali mkurugenzi mkuu aliahidiwa uwaziri.

upumbavu huo usijirudie tena.

unaetegemea riba kushuka kwa uliefunga mkataba sahau kabisa.

serikali yako imegoma kupunguza loan bodi toka 15 iwe 8 sembuse mwekezaji.

kwa masuali yote ya fedha niulize kifedha na uchumi, sio kisiasa
kwa hiyo BOT walitoa maelekezo bila kujiridhisha kwanza?!
 
BOT inapaswa ifuatilie na ijiridhishe kuona kama maelekezo waliyo yatoa yametekelezeka.
 
Nilitegemea hii trillion 1.3 iliyotolewa na IMF kupambana na athari za UVIKO kiasi kingekuwa injected kwenye mabenki ili kutoa relief kwenye mikopo ambayo wafanyakazi, wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali wanadaiwa kwenye mabenki na pia kutoa fursa ya mikopo yenye riba nafuu zaidi kama ilivyopendekezwa na BOT, lakini kwa hii nchi ya danganyika ninavyoijua hakuna mtu yupo interested na welfare ya watu wengine......wapo kwa ajili ya kuangalia matumbo yao waendelee kuneemeka wao tu.
 
hii benki ina ukwasi wa kutisha ila wateja wake wamebaki hoi.
 
NMB Bank kwa Ukwasi wake ilio upata kutokana na mishahara ya watumishi wa umma kupitia ktk Bank hiyo ilipaswa iwakwamue kiuchumi haswa ktk kipindi hiki cha janga la Uviko19 ambapo kipato kimeyumba.
NMB chukueni hatua maalum.
Mkuu siyo NMB pekee, hata CRDB watumishi wapo wengi tu na mikopo yao imekaba palepale........miaka inaenda na makato hayapungui, pesa inayokatwa mwanzo mwa deni inabaki palepale hadi deni linapoisha hata kama ni miaka 7. Hizi benki za kibongo zimekaa kinyonyaji sana na hazipo kwa ajili ya kujenga jamii.
 
sawa lkn NMB ndio Benki pekee iliyo ingia Mkataba na Serikali.
 
kwa nini Serikali isiingie Mkataba na Benki ya Kizalendo ya POSTA? kisha wakaachana na NMB.
 
Back
Top Bottom