NMB acheni uzembe, mnachefua sana

NMB acheni uzembe, mnachefua sana

Stavros Myles

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2020
Posts
350
Reaction score
390
Hi kwa wana jeiefu wote natumaini tuwazima wa afya, kwa wagonjwa na wenye shida mbalimbali m/Mungu awasaidie na kuwaonekea kwenye maisha yenu.

Moja kwa moja bila kupoteza muda nimeamua kuwapandia hewani NMB Bank, hii ni benki inayojinasibu kumiliki matawi mengi hapa nchini Tanzania na blah blah kibao, lakini nimekuja kugundua IT experts wao ni watu wa ovyo sana mshahara wanakula bure tu,bora hata waongezewe kazi ya ku "repair" hata bulb kuliko ujinga wanaoufanya.

Leo majira ya jioni mida ya saa 1 nikiwa nimetuliza kichwa baada ya kutoka kwenye majukumu mara gliii gliii kuangalia ni meseji kutoka Nmb, nikaifungua na kuanza kuisoma la haula! kwa mbwembwe za kiwango cha ndege ya concorde wameanza kuandika mtejaSOPHIA sasa nikajiuliza hii makusudi au kusema mimi taarifa zangu hawana hawajui ninaitwa nani mpaka ninaitwa jina la kike, uandishi wao mbovu unaweza ukayumbisha hadi ndoa yangu.

Mke atadhani ni jina la kampango ka kando kumbe wapi, sasa kama taarifa ndogo kama hiyo mnakosea itakuwaje kuhusu fweza zetu ambazo mna "deduct" kila baada ya mda, hivi kweli nikiamua niwe serious kupiga calculations na mhasibu wenu kuhusu pesa za account yangu mnadhani mtaepuka makosa.

Mnapoteza uaminifu kwa kuwa incorrect kwenye vitu vidogo tu, ukipiga simu huduma kwa wateja mnanisubirisha zaidi ya dk 15 kweli tutafika? 😥😥😥😥😥😥😥😥.

Screenshot_20200723-232708.png
Screenshot_20200723-232708.png
 
Pole sana Mzee.Na Mimi pia nimepokea Sms Kama iyo.Jamaa awapo Serious kabisa na Majukumu yao.
 
Hivi imekuaje majina yote ni ya kike, japo nimepata meseji ya kuombwa radhi. Ni sio NMB tu hata wiki iliyopita CRDB walikuwa na issue kama hii.
 
Hivi imekuaje majina yote ni ya kike, japo nimepata meseji ya kuombwa radhi. Ni sio NMB tu hata wiki iliyopita CRDB walikuwa na issue kama hii.
Wanajikombakomba kwa herufi kubwa, mistakes zao za kizembe mno😖😖😖
 
Mi nimechoka na app yao ya Nmb mkononi, siku hizi kila uki log in inatumia confirmation codes via sms , ndipo uendelee,

Hivi hao It experts wao wameshindwa kabisa kujua sababu ya hizi bank apps? kwamba zikusaidie wakati hata upo mbali na nchi husika ? maana nmb mkononi huwezi kutumia kama sim card haipo hewani maana hutapata confirmation sms, hata kama kuna internet.
 
Back
Top Bottom