Nlimwomba Mke wangu anilishe Limbwata...

Nlimwomba Mke wangu anilishe Limbwata...

ha ha ha.. sawa dada nmekuelewa kweli yana ukakasi sana. utapata mwanaume anayekufaa ikiwa kweli hauna..ingawa najua pia huwezi kosa mwanaume
OTE="Sodoku, post: 23809386, member: 351185"]kuna jamaa anaitwa GuDume alikuwa anatafuta mke nadhan ana sifa hizo
pia yupo @gagadudu
Majina yao tu hata na billion siwataki[/QUOTE]
 
Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.

nlikuwa na marafik kabla ya ndoa na baada ya ndoa. popote pale wanapokusanyika binadamu kunakuwa na changamoto zake. ukiwa ofisini ukawa unafanya kazi kwa bidii na unafuata sheria na taratibu zote kuna watu watakuchukia na kukuona unajipendekeza au una shida sana hivyo unaogopa kuvukuzwa kazi. hali kadhalika ......

kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.

kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.

imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k

wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.
Ukikua utakuja kuelewa
 
[QUOTE="Sodoku, post: 23809549, member: 351185"ha ha.. sawa dada nmekuelewa kweli yana ukakasi sana. utapata mwanaume anayekufaa ikiwa kweli hauna..ingawa najua pia huwezi kosa mwanaume

Majina yao tu hata na billion siwataki[/QUOTE][/QUOTE]
Ahsante kaka.......nakosaje ila hali moyo u mzima huna tobo wala tundu.sema ngempata mwny kasifa hako mweeeeh mbona ngeona dunia yote yng
 
Badilisha aina ya marafiki ulionao si lazima uwaridhishe follow your heart
 
Achana na hao fools, watakuja kujuta uzeeni.....Your a gentleman, teach ur sons how to be a gentleman lyk u. For they shall enjoy God's blessings. A married woman has the POWER to break her husband's blessings/success. I have seen real lyf situations of husbands with no more success in lyf because of her wife's curses & lamentations .
 
siku ukitendwa na huyi mkeo...akili itakukaaa!!
 
Jaman kama kuna mwanaume anayepatikana Wa namna hii,nipo teyari ata ndoa ya mkeka.

Au kaka huna mpango wa kuongeza mke wa pili?
Mimi nipo tyr
hakika hii dunia yote utahisi yako
 
Hongera sana familia ni kitu muhimu sana hii hata Mungu anajua. Shetani siku zote anataka kuharibu familia kwa sababu anajua Mungu anapenda watu waishi kwenye familia. So jihadhari na mashetani. Sisi baba yetu wakati wa ujana wake alikuwa kama hao marafiki zako. Siku ya siku akapata ajali akitoka kijiweni na marafiki. Watu waliyemuuguza na kuhangaika nae ni sisi watoto na mke wake na tena watoto tulikuwa bado wadogo. Lakini aliona ni jinsi gani tulivyompenda na kuhangaika nae mpk apone. Hao marafiki zake walikuwa wanakuja kimjulia hali tu lakini kuanzia kuogeshwa kula kuvalishwa kupewa dawa yote hayo alifanya mke wake.. Na uzuri bibi yetu alikuja kumuona mwanae alimwambia ushawahi sikia MTU akifa watu wanasema marehemu Ka acha marafiki zake wa bar? Huwa wanasema marehemu Ka acha mke, watoto, au wajukuu. So ipe familia yako kipaumbele. Toka hiyo siku alijifunza kama kunywa atakunywa Na mkewe nyumbani, kama kutoka atatoka na mkewe kwa sababu huyo ndio best friend wake. Leo wanazeeka pamoja hakuna anayeweza watenganisha. Hao marafiki zake wengi walishakufa yeye baba kabaki na mkewe.
 
Back
Top Bottom