Nlimwomba Mke wangu anilishe Limbwata...

Nlimwomba Mke wangu anilishe Limbwata...

Hongera sana familia ni kitu muhimu sana hii hata Mungu anajua. Shetani siku zote anataka kuharibu familia kwa sababu anajua Mungu anapenda watu waishi kwenye familia. So jihadhari na mashetani. Sisi baba yetu wakati wa ujana wake alikuwa kama hao marafiki zako. Siku ya siku akapata ajali akitoka kijiweni na marafiki. Watu waliyemuuguza na kuhangaika nae ni sisi watoto na mke wake na tena watoto tulikuwa bado wadogo. Lakini aliona ni jinsi gani tulivyompenda na kuhangaika nae mpk apone. Hao marafiki zake walikuwa wanakuja kimjulia hali tu lakini kuanzia kuogeshwa kula kuvalishwa kupewa dawa yote hayo alifanya mke wake.. Na uzuri bibi yetu alikuja kumuona mwanae alimwambia ushawahi sikia MTU akifa watu wanasema marehemu Ka acha marafiki zake wa bar? Huwa wanasema marehemu Ka acha mke, watoto, au wajukuu. So ipe familia yako kipaumbele. Toka hiyo siku alijifunza kama kunywa atakunywa Na mkewe nyumbani, kama kutoka atatoka na mkewe kwa sababu huyo ndio best friend wake. Leo wanazeeka pamoja hakuna anayeweza watenganisha. Hao marafiki zake wengi walishakufa yeye baba kabaki na mkewe.
Khaaa ahsante. Kwa kweli sijawahi kusikia marehemu kaacha marafiki zake wa bar
C.c espy Nalendwa MBITIYAZA
 
Hongera sana familia ni kitu muhimu sana hii hata Mungu anajua. Shetani siku zote anataka kuharibu familia kwa sababu anajua Mungu anapenda watu waishi kwenye familia. So jihadhari na mashetani. Sisi baba yetu wakati wa ujana wake alikuwa kama hao marafiki zako. Siku ya siku akapata ajali akitoka kijiweni na marafiki. Watu waliyemuuguza na kuhangaika nae ni sisi watoto na mke wake na tena watoto tulikuwa bado wadogo. Lakini aliona ni jinsi gani tulivyompenda na kuhangaika nae mpk apone. Hao marafiki zake walikuwa wanakuja kimjulia hali tu lakini kuanzia kuogeshwa kula kuvalishwa kupewa dawa yote hayo alifanya mke wake.. Na uzuri bibi yetu alikuja kumuona mwanae alimwambia ushawahi sikia MTU akifa watu wanasema marehemu Ka acha marafiki zake wa bar? Huwa wanasema marehemu Ka acha mke, watoto, au wajukuu. So ipe familia yako kipaumbele. Toka hiyo siku alijifunza kama kunywa atakunywa Na mkewe nyumbani, kama kutoka atatoka na mkewe kwa sababu huyo ndio best friend wake. Leo wanazeeka pamoja hakuna anayeweza watenganisha. Hao marafiki zake wengi walishakufa yeye baba kabaki na mkewe.


aiseee safi sana kwa mzeee dorrlyn kujitambua ! mie nakosa cha kuandika
 
Sodoku hongera kwa kujitambua ! jaman hivi una miaka mingapi? yaan unarange kati ya wapi na wapi!
mie ukiniona mume amewah home hana ht 100 !chefu
 
Nyinyi ndio mnatutukanisha wanaume wa Dsm
 
Khaaa ahsante. Kwa kweli sijawahi kusikia marehemu kaacha marafiki zake wa bar
C.c espy Nalendwa MBITIYAZA


Mh!, hongera zake mbona!
Haya mambo yao ya kutumia muda mwingi huko wanasahau hata kama kuna dating after marriage pia kudumisha upendo na ndoa. Wao wakishaweka mtu ndani ki halali basi anaachwa hivyo na muda mwingi unaishia kwa marafiki.
 
dada weka tuweze kushirikiana.. la msingi hutaji jina lake na sisi hatutaki kumfaham mhusika ila hapa tuna share uzoefu nasi tujifunze.
Siwezi yaanika waweza chefuka
 
Yote uliyoainisha ni sawa labda tu
SUALA LA MKEO KUMUOMBA RUHUSA YA KUTOKA SIO VIZURI LABDA KAMA UNAMTAARIFU
 
Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.

nlikuwa na marafik kabla ya ndoa na baada ya ndoa. popote pale wanapokusanyika binadamu kunakuwa na changamoto zake. ukiwa ofisini ukawa unafanya kazi kwa bidii na unafuata sheria na taratibu zote kuna watu watakuchukia na kukuona unajipendekeza au una shida sana hivyo unaogopa kuvukuzwa kazi. hali kadhalika ......

kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.

kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.

imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k

wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.
Nimelisoma andiko lako nami nimeona nichangie kile nilichojifunza kutoka kwenye ndoa.
Ni kweli kuwa kama mwanaume familia ndio kipaumbele chako cha kwanza. Ni kweli pia unahtaj kumsikiliza mkeo au kuwa na mipangalio inayomshirikisha mama kama mwenza wa maisha yako.
Sasa ngoja nikufundishe wewe na wengineo.
1] kwanza kabisa ndoa ni ile miaka mitatu ya kwanza so unapoanza ndoa kuanzia honeymoon uclete zile cjui beib cjui honey cjui maisha ya kwenye tv ya kimarekan yale. Uwe na kias tu ucpitilize maana unakokwenda ni mbali bado na humkin kutakuwepo muda mbaya na mzur unatakiwa ucmwonyeshe mkeo fake life ambayo hutaweza kuendelea kuionyesha kwake. Onyesha uhalisia wako maana ukija kurud kwenye uhalisia atakwambia zaman hukuwa hiv ndio ugomvi unaanzia hapo mara umebadilika nk.
2) mwanamke ucmwonyeshe mda maalum wa kurud nyumban. Leo ukirud saa moja kesho rud saa tano keshokutwa rud mapema kabisa asikusome kwenye muda hii ina faida nyingi na anatakiwa kukujua hilo ndio mipangilio yako.
3) kunatakiwa kuwepo na kikao cha familia cha mipango mikakati na utaratibu wa kifamilia wa kiuchumi, kijamii, kidini, kusahihishana, kusamehana na kukumbushana mipango yenu kufaulu au kufeli kwa mipango mliyojiwekea. kila mwanzo wa mwaka na kila baada ya miez mitatu.
4) kuwekeana mipaka, hapa namaanisha baba na mama wanatakiwa kuwa na sehem katika hiyo mipango wanaisimamia moja kwa moja bila ili kuruhusu mtu binafs kuonyesha uwezo wake, hii inampa mmoja wenu uwezo wa kujiamin na kuamin mawazo yake yaan mwisho wa cku kila mtu ajihc ni mshirika katika maendeleo ya nyumba.
4) ukitaka maendeleo ya ukweli msikilize sana mkeo hata anapongea ujinga lakin fuata nusu ya yale anayokuambia. Sasa namna ya kuyakataa mawazo yake sio moja kwa moja unakuwa na maneno ya kumshawish njia nyingine kwa maneno lain amin mwanamke anapenda mwanaume anaemsikiliza so unamsikiliza lakin unacheza na akili yake. Kumbuka mwanamke ni kama jin kila cku linatakiwa kupuliziwa uban kulituliza na uclitoe kwenye chupa ghafla ,kila unapopiga hatua ruhusu vitu flan vya kumfurahisha, kama ni gar mnunulie, out kidogo nk hii ni kwa kadir mipango nauchumi enu unavyppiga hatua. .
5) ucruhusu kuish na ndugu yeyote iwe kwao au kwenu utakuwasalama.ukiweza wasaidie kwa kias kule waliko.
6)kumbuka mwanamke anakuheshim sana maana wewe ni insurance yake na watoto wake lakin kumbuka mtoto wa kwanza wa kiume akifikisha miaka 25 wewe kwake sio inshu sana so pambana sana uwekeze b4 miaka hiyo ya ndoa maana kuanzia wakat huo mama na watoto wanakuwa pamoja kukuatak maana wakat huo huna nguvu ndio unakuta wazee wengi wanakufa kwenye miaka 60-75 coz mategemeo yao yamechukuliwa na mama. So jiwekee utaratibu wa kuwekeza ili wakibadilika ukute unapakuponea.
7) weka utaratibu wa sala nyumban kwako wa kudum,
8)kumbuka mwanamke anabadilika muda wowote ucmwamin sana kuwa na kias. Kumbuka hata huyo aliyewaumba alishatuasa tuish nao kwa akili hii ni ushahd waz kuwa ni mitambo kaa nayo kwa tahadhar kubwa.
9) mpende mkeo ila kuwa na kias.
10) kumbuka kuwa na marafiki hasa wa bar maana watu wakilewa ndio wanaongeaga ukweli na dili nyingi zipo bar japo ucwe mlevi, jitahd kuwa marafiki wazee pia ili kitu flan unapotaka ushaur unapata fasta. Mwisho. Kila levo ya uchumi na umri una marafiki zake so ucnga'ang'anie marafiki wa historia coz kila uchumi una watu wake.
 
dada weka tuweze kushirikiana.. la msingi hutaji jina lake na sisi hatutaki kumfaham mhusika ila hapa tuna share uzoefu nasi tujifunze.
Mkuu nitake radhi, nina ndevu, Gegedulio pamoja na makende.
How come you identify me as FE
 
OTE="Sodoku, post: 23809386, member: 351185"]kuna jamaa anaitwa GuDume alikuwa anatafuta mke nadhan ana sifa hizo
pia yupo @gagadudu
Majina yao tu hata na billion siwataki[/QUOTE]
Hahahaaaa.....Bora ukutane na gagadudu kuliku huyo jamaa anaitwa Gudume
 
Promo jipigie mwenyewe ukingoja kupigiwa utalala Dolo.

Mjomba kwa promo hili mboni utawachapa sana wakizani wewe ni mfano wa mume bora.
 
Dahhh hongera sana mpo wachache sana namshukuru Mungu mume wangu ana character kama zako na ww ulisoma Seminari nini mkuu "sodoku"
 
monanost: 23875066 said:
Majina yao tu hata na billion siwataki
Hahahaaaa.....Bora ukutane na gagadudu kuliku huyo jamaa anaitwa Gudume[/QUOTE]
Hahahahaaaa majina yao nahc yanasadifu yaliyomo........
 
nashukuru ndugu cajojo.... hapana sikusoma seminari ila napenda tu kuwa na nidhamu binafsi. maisha yangu yamejikita katika kuwa na kanuni...
Dahhh hongera sana mpo wachache sana namshukuru Mungu mume wangu ana character kama zako na ww ulisoma Seminari nini mkuu "sodoku"
 
Back
Top Bottom