Sakata la Burundi ni mgogoro usioweza kupata ufumbuzi wa kina kwa sasa hivi. Ni nchi ambayo watu wake wamezoea kuuana na kupinduana kana kwamba hakuna sheria zinazotawala taifa lile. Kwa sakata la Nkurunziza, mi simfahamu sana ila niliwahi kuwa Bujumbura miaka ya nyuma nikashtuka asubuhi nilipoona jiji zima likifanya mazoezi ya viungo. Nilipoulizia nikaambiwa hiyo ndo field ya rais wa nchi hii kwa hiyo wengi wanamfuata katika kujijenga kiafya. Pale niliona mwanya wa watu wenye nia mbaya kukusanyika asubuhi na hatimaye kumwingiza matatizoni....ndo nimeona katika vyombo vya habari kuwa mazoezi yale hatimaye yalipigwa marufuku...wapinzani wake walipaona na wakajua atatolewa kwa sheria yake mwenyewe...naye akafunga uwazi ule. Uhalali wa muhula wa tatu....hapa ndo sipaelewi kabisaa...sakata hili linataka kuwa kama la Ukrain na Cremia...wakati Ghorbacheiv anatangaza Perestroika...iliyoisambaratisha Urusi alishangiliwa sana kuwa demokrasia imetawala na watu wamepata haki yao ya kutangaza kuwa sisi ni Chechen, Ukrain, n.k na dunia ilisema hii ndiyo demodrasi. Ilipotokea kuwa Ukrain watu wanataka kujiunga na magharibi na wakamtoa kwa maandamao rais aliyekuwa madarakani, nayo ilionekana ni demokrasia nzuri tu hakukuwa na shida. Pundi si punde katika nchi changa ya Ukrain sehemu yake Cremia ikasema inataka kujitenga...minong'ono ikaanza si vema ni njama za Urusi. Wakafanya referundum ambayo ndiyo njia ya kidemokrasia hata inatumika kwa Scotland na Ireland lakini Cremia ilipoonekana wanaunga mkono kujitenga wakaambiwa hii si sahihi. Putin akaona 'double standards' zinazotumika katika vyombo vikuu vya maamuzi ya kimataifa akasema watu wameamua wapeni walichotaka....hadi leo sidhani kama anaonekaa vema mbele ya mataifa...vikwazo zikawa kama ndiyo lazima kwake. Hakuna mahakama iliyosema tangazo la Ukrain au kura yao ilikuwa na wizi...ila tu hawakupaswa kupiga kura hiyo.
Sakata la Burundi mi naona limelala hapo. Kwamba kambi ya Nkurunziza inasema huu ndo muhula wake wa pili, wapinzani wanasema huu ni muhula wa tatu. Tafsiri itoke wapi? Mahakama ya katiba (naona hapa haijadiliwi hii), mahakama ikasema apewe ndo muhula wake wa pili naye akasema utakuwa wa mwisho kwake. Mataifa yakasema zoezi la kupiga kura liahirishwe kwanza ili tutoe nafasi sawa kwa wapinzani kufanya kampeni...hiki sikielewi katika muktadha wa demokrasia na utendaji wa serekali kwamba kila watu wakiandamana tutakuwa tunaahirisha mipango yetu. Akina bwana mkubwa wakamnyima pesa za uchaguzi...baada ya hapo mapinduzi....ukiunganisha unajua nini kiko nyuma ya mapinduzi.
Bado siamini siasa za kupendwa na wananchi kuliko misingi na taasisi za demokrasia. Katika dola ya kirumi kulikuwepo na uchaguzi wa mtu akitokea watu wanakushangilia halafu unakuwa ndiyo kiongozi wao. Tunajua dola ile watu walinunua watu na wakashangiliwa na wakawa viongozi. Lakini ndo walikuwa viongozi wabaya na ni sababu kati ya nyingi zilizosababisha dola hiyo kuanguka. Kwa suala la Burundi mi naamini bado tafsiri ya mahakama ndilo suluhisho kuliko maandamano barabarani kwa nchi ambayo tayari ina nyufa zaidi ya nyingi tunazozitarajia. Kama kuna kukiukwa kwa misingi ya mahakama, jamaa zetu wapo pia katika jumuiya ya afrika mashariki, wanaweza kupeleka malalamiko ya kisheria katika mahakama hizo pia...si mwanasheria sijui nguvu za sheria za mahaka hizo...ila najua kuna kesi tena toka Burundi ilipata suluhisho toka mahakama za Afrika Mashariki. Waandamanaji wanazo haki zao, lakini misingi ya sheria inapaswa kuheshimiwa si tu kuangalia upande wa haki bila wajibu kama raia na mwanadamu ambaye unapenda na wenzio waishi. Nimeona clip ya kumpiga anayedhaniwa ni 'imbonerakure' kwa mawe na vingine...hali hii ni chaotic na nchi ikiendeshwa kwa chaotic democracy itakuwa pia chaotic country na lawlessness ikitawala haki huwa imeshatangulia kaburini miaka mingi nyuma.
Ushauri wangu tafsiri ya muhula wa tatu iangaliwe kwa makini, na kama hakuna suluhisho la kisheria, basi maana yake ni kusubiri hiyo mitano ipite tuone movie itakayofuata ni nini kuliko kuingiza nchi katika hali ya 'anarchy' kwa sababu tu wapo wanaotaka pia kuwa marais. Afrika imewavumilia wengi naona kwa sababu tusizozijua maana hata kama magharibi wanasema lakini hadi leo Mugabe bado ni rais pamoja na kuwa na zaidi ya miaka 90 na miaka huenda karibu 40 ya kuwa madarakani. Tujifunze kukomaza taasisi kuliko kukomaza 'anarchy'. Kanuni iliyotumika mahakama za Burundi ni kanuni hiyo hiyo ya kupiga kura inatumika hadi leo Marekani wanapofanya maamuzi magumu kama ya ushoga na vinginevyo na haijaonekana kama ni tatizo...maana ndiyo mfumo wa mahakama za kibinadamu, zaweza kukosea na hata kuhongeka na hata kutumika na wenye nia zao...!!!! Ni mawazo na maoni yangu na wala mi si msuluhishi wa migogoro ya wao kwa wao huko Burundi