Nkurunziza atangazwa kuwa kiongozi wa maisha CNDD/FDD

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,383
33,041
nkurusinza.jpg

Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.

Tangazo hili la chama tawala CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kama Kiongozi Mkuu wa Kudumu linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu Marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Kati ya mambo mengi katiba hiyo ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.

Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Lakini pia uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.

Isitoshe kwa Wachanganuzi wa siasa za bado wanaiona hatua hii ya Rais Nkurunziza kutangazwa Kiongozi wa maisha kama dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama cha CNDD/FDD.

Chanzo: BBC Swahili
 
Acha na yeye aongoze tu milele mbona Jirani take hapo Rwanda kapiga sarakasi kwenye katiba mpaka akawa Wa milele? Burundi na Rwanda ni mataifa identical. Tofauti ni kuwa Rwanda yenye majority ya Hutu na minority Tutsi inaongozwa na Tutsi wakati Burundi yenye majority ya Hutu na minority Tutsi inaongozwa na Hutu.
 
Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

_100371438_cf9451c3-e2e6-4642-985c-59b959bacfa7.jpg

Alinusurika kupinduliwa mwaka 2015
Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.

Tangazo hili la chama tawala CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kama Kiongozi Mkuu wa Kudumu linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu Marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Kati ya mambo mengi katiba hiyo ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.

_100370936_87b95fef-d06d-48e4-9194-9e9737ccafdb.jpg

Nkurunzinza ni mcheza soka mashuhuri pia nchini Burundi
Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Lakini pia uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.

Isitoshe kwa Wachanganuzi wa siasa za bado wanaiona hatua hii ya Rais Nkurunziza kutangazwa Kiongozi wa maisha kama dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama cha CNDD/FDD.

Kwa hisani ya BBC Swahili
 
Bado hapa kwetu nao wataenda CHATTLE kujadili hilo
Inakuja haya ni mabadililko ya kidunia tunaita wind of change, urusi wako mbioni. Ujamaa wetu tunautaka kwa speed kali.Mungu alisema na Ayubu kuwa hakuna kipya yote yalishatokea ni marudio
 
Hiii ndo afrika kiongozi wa maisha kwa maaanaya kwamba hatokuja mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza zaidi yake sma ina maana ata wanachama wake wakimchoka hawawezi kumtoa kwa maana katiba ya chama itakuwa ina mlinda daaaaah afrika yangu ivi ni kwanini haya yote yanatokea afrika???????
 
Madaraka ni matamu sana.
Hofu tu ndiyo imemtawala.

Ngoja tusubirie upande mwingine wa nchi jirani zinazoizunguka Burundi.
 
Mambo haya yanahitaji msaada wa Mungu kwa kweli.! Maana upeo wetu wa kutatua changamoto tunaujua wenyewe.!
 
Back
Top Bottom