charrote
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 1,988
- 4,413
Habari ya uzima,
Naomba niwasilishe hoja yangu kama ifuatavyo...
Nakumbuka nikiwa shule ya msingi darasa la sita ndipo yale masomo ya ukuaji wa binaadamu ndipo yalianza kuzungumzwa kwa upana katika somo la Sayansi. Nikiwa sekondari mada za ukuaji na mahusiano ya kimapenzi mpaka kufikia kuzaliana zilikua zikifundishwa kwa upana sana.
Kadri unavyoendelea kuongeza elimu unaweza kugundua kuwa suala zima la mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume ni muhimu sana. Hata tukirejea katika maandiko matakatifu wakati wa uumbaji Mwenyezi Mungu baada ya kumuumba Adam(mwanaume) akaona si vyema awe peke yake hivyo hakumuacha peke yake akamletea msaidizi Eva (mwanamke).
Naomba tujadiliane kwa kina suala hili kwa upande wa ndugu zetu walioko magerezani(wafungwa). Je kuwa mfungwa tayari unakuwa umepoteza haki yako ya kuwa na mwenza wako kama ilivyoagizwa na Muumba?
Kwanini usiwekwe utaratibu walau mara moja kwa mwezi na wao waweze kutendea haki hisia zao? Ikiwa wewe huwezi kumaliza wiki bila kushiriki mapenzi inakuwaje kwa mwenzio ambaye anatumikia kifungo miaka 25 au maisha yote? Au kuna kipengele katika katiba kinakataza? Kwanini?
Mwenye majibu anakaribishwa.