Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

sitasahau Shulen Tanga kuna jamaa alikurupuka kitandan bukta iko magotin usiku akatoka mbio had nje huku anatukana.. tulijua kapandisha mashetan.. kutoka nje tunamkuta ameshika fimbo anatukana kumuuliza akasema kuwa kuna binti mwanafunzi alikuwq anambaka.. na amemfanyia hivyo mara mbili..

sasa alikuwa amemtime amdake sema binti kamchomoka.. tukajiuliza mbona hatujaona mtu aliekuwa anamkimbiza akasema alikuja kichawi.. watu wakabisha akasema kweli ninusen kuna msela akanusa akasema dah kweli unanuka ****
na jamaa dushe lilikuwa limesimama..

masela kuona hivyo eti wengine wakawa usiku wanavua bukta wamelala uchi wanamuomba mariam aje awabake.. dem alikuwa anaitwa mariam eti hawatambishia watatoa ushirikiano

kisa cha pili siku hiyo tunatoka kuangalia mpira UEFA kijijini.. tulikuwa na kaka mkuu pamoja na Patron ambaye alikuwa mshakaj tu.. sasa tunakatiza mabwen ya wavulana ambayo yako
umbali wa kiwanja cha mpira kutoka majengo mengine ya shule ikiwemo bwen la
wasichana tukaona mtu kachutama kimuibukia kumbe binti wa pale shule alikuwa anawanga ndo ameweka ungo chini anajiandaa kuanza ushirikina sijui alikuwa anaenda wapi.. basi Patron kuona hivyo akachagua masela watatu akasema mpelekea mabwen ya wasichana muwambie walinzi wamuamshe matron ili mumkabidhi matron kesho tutalizingumzia na matron

Asubuh Patron anaenda kwa matron Kumuuliza ishu ya jana usiku matron anashangaa hana taarifa.. Ikabidi Patron awaite masela aliowakabidhi binti kuwauliza kulikon wakasema wakati wanamrudisha aliwaloga wakamsamehe

kumbe masela wameona binti yuko
uchi kaumbika wakamwambia awape mzigo wamwachie dem akawapa mzigo wakapiga mtungo wakamwachia

na ikawa kila siku usiku wanavizia maeneo yale eti wakamate mabinti wachawi wawale
mtungo

maisha ya boarding school shule tosha ilitakiwa tupewe vyeti nje ya vyeti vya taaluma..
Hiki kiss sio mahala pake hapa, ungekipeleka kule kwenye Kula tunda kimasihara
 
Acha nami nishee story yangu japo si mzuri sana katka uandishi.
Ilikua 2010 Dar es salam enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapo. Ukweli sikukutana nakiumbe cha kutisha bali ni binaadam alienifanya nibaki na sintofaham na maono tofauti ktk maisha.
Sikubahatika kupata chumba ktk hostel za chuo ikanibidi nipange kitaa flan uswahilini karibu na mwenge hapo. Maisha yalikua fresh tu fadha house alikua na wake wawili na watoto kadhaa hapo kijana mkubwa wa mwenye nyumba alitokea kua mwanangu sana story za hapa na pale, jamaa alikua mstaalabu sana na anasura ya upole by that time alikua kama ana 30 yrs nakuendelea.
Tukio lilotokea lilinifanya nibaki mdomo wazi ni siku moja mida ya saa tisa kasoro huyo bro aliniamsha kwa kugonga mlango nlisita kuitika lkn mwisho nilifunua nakumkuta amemkamata kijana mmoja wa makamo. Jamaa akanambia kwamba huyu ni mwizi na huwa anaibia watu hapo mtaani. Nikamuuliza vp ushahidi unao akadai hana ila amemkuta na kisu mfukoni. Nilitaka kuacha kumpa ushirikiano ila nikaona nimsaidie huyo kijana asijedhurika kwani hakukua na ushahidi wowote. Nilimshauri jamaa kua tuamshe majirani au ndg zake jamaa akawa mbogo. Ilibidi nimfate kwanyuma akiwa amemkamata yule kijana shingoni tukielekea nyumba iliokua opposite na hii tunayokaa. Nilipata bahati ya kumuuliza jamaa akakubali ni kweli hapo aliwahi iba shati na sendoz. Nilijua itakua kesi ndogo lkn tulipofika kwa huyu jirani aligonga mlango mara mbili tatu huyo mzee akafungua na kuelezwa dhumuni la sie kuwepo hapo. Alimtazama yule kijana kwa macho ya dharau na kuulizia mimi kwani hakuwahi niona maeneo hayo ndo jamaa akanitambulisha kama mpangaji wao. Yule mzee haraka bila uoga alitupa jukumu tumuue huyo dogo then tukimaliza tumchome moto hapo hapo. Nilihisi kuogopa nikaona ni kama mzaha vile kwani tulikua wawili tunaopewa jukum hilo. Alipomaliza kufunga mlango wake mzee yule nilimwambia huyu mshkaj kwanini tusimteme tu dogo coz vitu alivyoiba nividogo sana. Msela alinifokea sana na kunipolomoshea matusi makali. Ilibidi niwe mtazamaji asikwambie mtu kifo ni kitu rahisi sana, dogo alishushiwa kipigo hevy ngumi na mateke mpaka akazimia ndipo jamaa alipoanza kutumia mawe yaliyokua pembeni . Ilifika muda dogo alipiga mayowe maskini it was too late, jamaa alihitaji kuua siku hiyo. Baada yakama dakika saba dogo alivuta nikimshuhudia alimsihi yule jamaa akimtaja kwa jina kua unaniua bure bro mimi ni mdogo wako, haikusaidia kitu dogo alipigwa taili mbili na kumwagiwa mafuta ya taa. Aliwaka mpaka mwisho. Niliogopa sana na usiku huo sikulala tena taswira ya kile kipigo ilikua ikinijia kichwani. Niliogopa sababu dogo alouwawa na huyu jamaa ni wa pale mtaani vp mimi mgeni. Nakwanini jamaa hakutaka watu waamshwe na dogo mbona hakua amemuibia huyu jamaa kitu.
Ilibidi iwe siri yangu mpaka nilpokuja kufahamishwa na majirani wengine juu ya kuokotwa mara kwa mara maiti zisizo julikana mtaani. Ilibidi nihame kimya kmya na kujiapiza kua sintokuja kupanga uswahilini tena na hawa binadam wenye sura nzuri za upole niishinao kwa tahadhari kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah.. inasikitisha sana
 
Huyo jamaa alikuwa ni muuaji tu
 
sitasahau Shulen Tanga kuna jamaa alikurupuka kitandan bukta iko magotin usiku akatoka mbio had nje huku anatukana.. tulijua kapandisha mashetan.. kutoka nje tunamkuta ameshika fimbo anatukana kumuuliza akasema kuwa kuna binti mwanafunzi alikuwq anambaka.. na amemfanyia hivyo mara mbili..

sasa alikuwa amemtime amdake sema binti kamchomoka.. tukajiuliza mbona hatujaona mtu aliekuwa anamkimbiza akasema alikuja kichawi.. watu wakabisha akasema kweli ninusen kuna msela akanusa akasema dah kweli unanuka ****
na jamaa dushe lilikuwa limesimama..

masela kuona hivyo eti wengine wakawa usiku wanavua bukta wamelala uchi wanamuomba mariam aje awabake.. dem alikuwa anaitwa mariam eti hawatambishia watatoa ushirikiano

kisa cha pili siku hiyo tunatoka kuangalia mpira UEFA kijijini.. tulikuwa na kaka mkuu pamoja na Patron ambaye alikuwa mshakaj tu.. sasa tunakatiza mabwen ya wavulana ambayo yako
umbali wa kiwanja cha mpira kutoka majengo mengine ya shule ikiwemo bwen la
wasichana tukaona mtu kachutama kimuibukia kumbe binti wa pale shule alikuwa anawanga ndo ameweka ungo chini anajiandaa kuanza ushirikina sijui alikuwa anaenda wapi.. basi Patron kuona hivyo akachagua masela watatu akasema mpelekea mabwen ya wasichana muwambie walinzi wamuamshe matron ili mumkabidhi matron kesho tutalizingumzia na matron

Asubuh Patron anaenda kwa matron Kumuuliza ishu ya jana usiku matron anashangaa hana taarifa.. Ikabidi Patron awaite masela aliowakabidhi binti kuwauliza kulikon wakasema wakati wanamrudisha aliwaloga wakamsamehe

kumbe masela wameona binti yuko
uchi kaumbika wakamwambia awape mzigo wamwachie dem akawapa mzigo wakapiga mtungo wakamwachia

na ikawa kila siku usiku wanavizia maeneo yale eti wakamate mabinti wachawi wawale
mtungo

maisha ya boarding school shule tosha ilitakiwa tupewe vyeti nje ya vyeti vya taaluma..
Hata ningekuwa mie sikubali mbusus ilivo ile tena za wachawi zinakuwaga zimeumuka flani hivi mweee!! inajaa kwa kiganja! hapo hata mie niroge tu yaishe!! !

kwa hiyo madogo wakapanga kabisaaa! tuseme tumerogwaaa!? yaani Duniani kuna mamboo!! ........angekuwa Discpline master wetu hao wange koma kwa fimbo!!! yaani mume mwachia mchawiiiiiii! why?? rara chini! kuchimba visiki!! tena na

mkamrete tena mchawi wangu km alivo kuwa paree uchi!! si munamujua jina!
 
Kuna binadamu wamepewa uwezo wa kung'amua vitu na kuna wengine katika ulimwengu wa kiroho ni vipofu wasioona kitu chochote. Macho yao yamefungwa. Sikumbuki vizuri ila katika biblia kuna mtume mmoja walizingirwa na maadui lakini hakuonesha wasi wasi wowote. msaidizi wake akamwambia sasa tunauwawa. Yeye akajibu ondoa wasiwasi tunaulinzi yule akashangaa ulinzi u wapi. Ndipo yule mtume akamfungua macho yule mtumishi akaona jeshi kubwa la malaika limewazunguka. Ndipo wasiwasi ukaondoka. wanaojua Biblia watasema ni nani. Nilitaka tu kukwambia haya mambo ni ktk roho. uwezi yaona mpaka uwe katika ulimwengu wa rohoni. Majini, Malaika uwezi waona kwa macho ya nyama. Kuna watu wanazaliwa wananguvu maalum za kiroho. Haya mambo yapo!
Elijah mtume na gerhaz mtumishi wake
 
Mwaka 2012 nilienda wilaya ya rungwe kukusanya data, sasa katika harakati za kuzunguka nikafika kijiji fulani kinaitwa malalika sijui kama nimeandika sahihi, kipo 15km kutoka kiwila na 7km kutoka hospitali ya igogwe, nyumba niliyofikia ilijengwa mlimani hivi katikati ya shamba la chai, ilikua na vyumba viwili vya kulala nikapewa chumba kimoja kingine alilala mhudumu wa lile shamba, nyumba ilijengwa kwa tofali za tope ila ndani wamebandika magazeti chumba kizima ndio plasta na juu wameweka shuka ndio ceiling board, usiku nilipokua nimelala nilianza kusikia kishindo kikubwa juu ya bati kama mtu anatembea kutoka upande mmoja wa nyumba kwenda mwingine, mwanzoni nilihisi kama ndoto ila niliposhtuka usingizini niloendelea kusikia kama mtu anatembea juu ya bati, ile hali iliendelea kwa muda mrefu, niliinua kichwa kuchungulia dilishani nje sikuona kitu palikua na ukungu mkali ikabidi nirudi kujifubika branket langu huku moyo ukienda mbio sana nikajua leo kazi ninayo, baada ya muda ile sauti iliacha ghafla kikaja kitu kama kimbunga mle chumbani upepo mkali ukabandua yale magazeti yote ukutani mavumbi ya tofali yakawa yananiangukia kitandi mimi nimejifunika hadi kichwa nimekaza miguu shuka lisitoke, ule upepo ulipoisha nikaita alexxxx kwa sauti kubwa ambaye ni yule mwenyej wangu aliyelala chumba kingine alipoitika sikujua nimefikaje chumbani kwake, maana niliruka kitandani nikapiga teke kile kimlango cha chumbani nikavamia na mlango wake hadi chumbani kwake, nikamuuliza kama amesikia ivo vitu licha ya kuwa na baridi ila jasho lilikua linanitoka, jamaa alichonijibu ni tulia acha papara. Nikawa nimekaa kwenye kistuli pembeni ya kitanda chake huku tumewasha kibatali, jamaa akaniambia pametulia rudi ukalale nikakataa nikamwambia silali nakaa hapa hapa wewe lala, nilikaa pale hadi alfajiri nilipoona nje pameanza kupambazuka nikaenda mle chumbani palikua hovyo sana vumbi kila mahali nikachukua kibegi changu nikamwambia yule jamaa mimi nasepa badae njoo kiwira tuongee, nikatoka nikadandia magari yanayobeba ndizi na maparachichi kwenda mnandani, saa nne yule jamaa akikuja kiwira nikampa elfu ishirini nikamwambia ikitokea siku mabosi wangu wakija kijijini kuuliza kama nilifika awambie kuwa nilikuja na nikafanya kazi ila kiukweli nilikimbia huwa sisahau lilie tukio, kuna lingine nililiona wilaya ya mbogwe mkoa wa simiyu, ni vijijini huko ndani kabisa hata barabara hakuna mnapaki gari mnatembea 4km huko tulizinguana na mwenyekiti wa kijiji akatutumia kundi la fisi tukakimbilia kwenye nyumba ya mwanakijiji tukapiga simu kwa mtendaji akaja kutuokoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fisi? Dah
 
Hata ningekuwa mie sikubali mbusus ilivo ile tena za wachawi zinakuwaga zimeumuka flani hivi mweee!! inajaa kwa kiganja! hapo hata mie niroge tu yaishe!! !

kwa hiyo madogo wakapanga kabisaaa! tuseme tumerogwaaa!? yaani Duniani kuna mamboo!! ........angekuwa Discpline master wetu hao wange koma kwa fimbo!!! yaani mume mwachia mchawiiiiiii! why?? rara chini! kuchimba visiki!! tena na

mkamrete tena mchawi wangu km alivo kuwa paree uchi!! si munamujua jina!
Dah umenikumbusha habari za kuchimba visiki vya mnazi... Academic master a.k.a tulikuaa tunamuita " kihotpot" mkaksi adhabu zake push up mia na kuchimba Visiki anaweza akakupa hata visiki vitano.. Sema wana tulikuwa tunapigana tafu jion kuchimba visiki maana hujui kesho unaweza ukapewa wewe kisiki

Ana msemo.wake anasema mitoto ya siku hiz imekuwa kama mazezeta unamgombeza anakuangalia tu wala hasemi samahan sababu wamemzulumu ndama maziwa yake.. Wamekulia maziwa ya ng'ombe badala maziwa ya mama zao wamekuwa na akili za ndama
 
Miaka ya nyuma baada ya kumtibu ndugu yetu mmoja ikashindikana kupona ndipo mganga aliposema inabidi tuwaite wachawi waliomroga ili watuonyeshe dawa mana kwangu imeshindikana tukaa kama wanafamilia tukakubaliana na maneno ya mganga siku ya siku imefika tukabeba mgonjwa mpk makabulini na mganga nakumbuka ilikuwa saa 8 usiku tumefika pale mganga akaanza mambo yake mara akachukua filimbi akapiga mara 3 tukaanza kuona mauza mauza mganga akatwambia mnapaswa msiogope hiyo dawa niliyowapaka ni ya kuona wachawi ambao wamefanya hili jambo ila iwe siri yenu na watakachotaka muwatimizie ili tusijenge vita mimi na wao kweli bana akaanza kutokea paka anageuka kuwa mtu mara ndege anakuja pale anageuka na kuwa mtu yani siku hiyo niliona kila aina ya vitwimbwi ghafla wakawa watu kama 10 hivi na kila mmoja amekuja kwa style yake wakatuuliza tumewaitia nini mganga akawaeleza shida yetu watuonyeshe dawa ya kumtibu fulani tyliye naye pale dah ila wachawi wana maneno ya kejeli yani tulitumia kama lisaa mpk kuelewana na kiasi walichokitka tukawapa nusu siku hiyo wakamuonyesha mganga dawa ya hilo tatizo ndio kupona kwa ndugu yetu ila nilipomuuliza yule mganga kwanini imetubidi tuwaite wale wachawi alisema mchawi hata uwe mganga wa aina au mtu wa aina gani wakikuamulia wakumalize hawashindwi bila kujali una imani au huna.Nyingine ni ktk utafutaji ridhiki hapo ndio nilikuja kuona duniani kuna viumbe tunaishi navyo bila sisi kujua
Weka na hiyo nyingine Ngulukizi
 
Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Na kwa Bahati nzuri akaweka kizuizi kwa kupitia uwezo wake wa kiungu hili tusiweze kushuhudia viumbe hivyo ambavyo havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu isipokua kwa utaalamu flani wa mambo ya kiroho.

Viumbe hivyo vikiwemo , Malaika, Majini , Wachawi pamoja na viumbe vingine vya kutisha sana, ikiwemo wanyama wa ajabu wenye ukubwa wenye kutetemesha na kuogofya kwa wanadamu wa kawaida.

Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”

Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”

Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Wengi tukisoma Habari kama hizi za kuona simba mwenye vichwa vinne na miguu kama ya binadamu, beberu mwenye pembe kumi, nyoka mwenye vichwa saba na wanyama wengine wa kutisha, tunajipa moyo na kusema hiyo ni lugha tu ya biblia/ lugha ya picha hakuna viumbe kama hivyo. Ila ukweli ni kuwa viumbe hivyo vipo na vinaishi kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu wetu unaonekana. Na kuna binadamu wenzetu wameshashuhudia kabisa kwa macho yao.

Tuachane na hayo na turudi kwenye maada yetu ya leo . Tuzungumzie kuhusu mikasa ya kutisha ambayo tumewahi kukutana nayo kwenye ulimwengu huu ambayo kwa namna moja au nyingine vimekuacha midomo wazi na kukufanya uwe traumatized.

Ngoja nianze na mikasa / mambo ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani ambayo mpaka sasa hivi bado najiuliza kama ni viini macho au ni kweli , lakini ukweli unabaki kuwa ni kweli .

1. Jini kuchomoza baharini na kuelea hewani.

Nakumbuka ilikua ni usiku wa manane, nikiwa kwenye harakati za ushikirikina Uko sehem( sipendi kutaja jina). Nikiwa na mganga akiendelea kufanya mambo ya kishirikina baharini, Ambapo alisema anaita kiumbe( jini) hili anitimizie haja zangu . Kwa akili yangu nilijua tu ni danganya toto, hakuna lolote. Baada ya kama dakika 45 za yule mganga kufanya ushirikina wake. Ghafla akatokea mwanamke mrefu tofauti na urefu wetu wa kawaida wa binadamu alikua baharini anaelea tu, miguu haionekani kwa kweli nilikimbia, Bahati nzuri wale wasaidizi wa mganga wakanikamata kunizuia nisikimbie. Uzuri hakua anatisha wala nini, alikua tu ni mwanamke wa kawaida ingawa alikua na urefu usio na kawaida, na alikua kakasirika sana, alikua analalamika tunamuita sana tuna shida gani.....

2. Niliwahi kushuhudia kwa macho yangu , binadamu akiwa nusu mtu , nusu simba, Ana sura ya kutisha sana , mbaya mfano hakuna, ilibaki kidogo tu nizimie.

3. Binadamu mfupi kama stuli, Ana ndevu nyingi mpaka chini na alikua na mguu mmoja tu , na macho yake yanawaka moto.

4. Mzimu wa mtu maarufu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita.

Hii ndo mikasa ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani, ambayo kiukweli mpaka leo inanipa shida sana, na ilichukua miaka kadhaa mpaka kuweza kukubali hii hali mpaka kufikia kuzoea kidogo. Ila hapa duniani kuna viumbe vya ajabu mno, na kama ukitaka kuviona unaweza.

View attachment 1430585

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ndugu umesema ukiwa na mganga wako baharini aliibuka jini mwanamke mwenye urefu usioelezeka, ukakimbia wasaidizi wa mganga wakakudata. Unaweza niambia ulikimbiaje baharini? Ulikimbia kwa miguu ama mtumbwi ama boti?
 
Sijawahi kushuhudia jambo la kutisha na kuogofya kama hili👇
B0Jj.jpg
 
Ndugu umesema ukiwa na mganga wako baharini aliibuka jini mwanamke mwenye urefu usioelezeka, ukakimbia wasaidizi wa mganga wakakudata. Unaweza niambia ulikimbiaje baharini? Ulikimbia kwa miguu ama mtumbwi ama boti?
Amesema walikuwa baharini, ila hajasema kuwa walikuwa ndani ya maji (think that way, then maswali yako yote yatajibika)

By the way, mleta mada alishatangulia mbele ya haki, thats why nimesaidia kujibu.
 
Maofisini kuna Mambo Sana, miye nilifika ofisini kwa Mara ya Kwanza karibu Kuna msikiti. Ile adhana ya saa saba kichwa kilikuwa kinaniuma mpk natoa machozi.Mzee mmoja hivi wa BC (born before computer) nilikuwa namsaidia kutuma zile risiti kwa email, akaniambia Weeee mtoto nenda kwenu kaage.
Nikamwambia mzee wangu akanifanyia duwa nikawa fresh. Ofisini kuna jamaa alinuna balaa.
Dunia hii kuna watu wana roho za kishetani sana basi tu
 
hili tukio sijui niite ndoto au uhalisia.
nikiwa na miaka 14 mikoani mbeya wilaya ya kyela, kuna siku nimelala usiku nikaota nipo sehemu na mtoto wa jirani yangu na baba yake ambao wanakijiji walikuwa wanawatuhumu kwamba ni wachawi, sina uhakika kuhusu hilo.
basi huko tulipokuwa tulikuwa tunafanya mambo mengi ni kama sherehe hivi, baadae baba wa yule kijana akasema mda umeisha inatubidi turudi nyumbani. Tukaanza kupaa wakati tunakaribia kufika nyumbani ghafla nikawa kama nimeshtuka kutoka usingizini kabla sijaingia ndani, lakini chakushangaza nikiwa bado sijielewi vizuri nikaona ukuta unafunguka na nikaingia kwa kasi ya kama spidi 500 mpaka kitandani. Nilivyofika kitandani akili ndio ikaa sawa, sasa nikawa najiuliza hii ni ndoto au uhalisia sijawahi pata jibu mpaka leo.
Pengine ndio maana umekuwa mjanja wa kijiji, ulienda kuwanga bila kuwa mchawi chief
 
Yaani nimemu admire kwa hilo, nimejifunza kitu kutokana na hio story, wazazi inabidi wawe close na watoto wao kuwahoji na kusikiliza yanayoendelea kwenye maisha ya mtoto
Asilimia kubwa ya sisi huku hili jambo hatufanyi kabisa, sio kwa watoto wetu tu, hata sisi hatukufanyiwa ndio maana tunalipuuzia sana
 
Back
Top Bottom