Njoo tujuzane ujuzi wa kutafuta sattelite za chaneli bila kubahatisha

Swadakta. Hilo tatizo lipo kwa wengi. Cha kufanya, cheza na lnbf. Uwe unaizungusha kidogo kidogo aidha kuelekea kulia ama kushoto, ukishapata signal tayari. Unazungusha kidogo una search. Zikigoma unaendelea kuzungusha kidogo una search tena. Mpaka uipate. Kqma ni kukia iwe kulia tu, na kama unazunguaha kwenda kushoto iwe kushoto tu. Signal za Channel 10, Tbc na Star tv ziko weak sana kwenye hio satellite.

Sent using Jamii Forums mobile app
star tv walishahama huko 906. kwa dish alilo nalo aongeze lnb nyingine kwa ajili ya nyuzi 75 atapata star tv, akina tv e na clouds kwa signal kuuubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kuelekeza dish kwenye satellite, ukiyafuata dakika 10 nyingi unakua umemaliza, mafundi wetu wengi wanafanya kubahatisha kuzungusha dish hadi kuipata satellite. Ngoja nieleze kwa uzoefu wangu nilionao, unaweza tafuta satellite yoyote ile na kwa muda mfupu kama ukifuata taratibu hizi
  1. Pata footprint(Eneo lote ambalo mawimbi ya satellite husika yanafika) ya satellite. Kuna Website nyingi na tools zinazowezesha hili kwa mfano kwa kutumia Satbeams - World Of Satellites at your fingertips chagua satellite unayoitaka na utaona footprint yake na taarifa zaidi kama inavyoonekata kenye hii picha
    satellite-png.387957
Hapo ni kwa dar es salaam satellite ya Eutelsat 36B ipo nyuzi 36 mashariki (DSTV wanaporusha matangazo). Pia utaona ukubwa wa dishi linalotakiwa ili kupata signal, mfano hapo ni kuanzia 80cm unaipata vizuri tu. mkono wa kushoto kuna taarifa zaidi muhimu. hizi ni elevation angle 80.8 (hii ni kiasi gani dishi linatakiwa linyanyuke), True azimuth 334.2 (ni uelekeo wa dish) na lnb skew 25.6 (Uelekeo wa lnb). Hivyo vitu vi 4 nilivyobold ndiyo muhimu uvijue ukitaka kutafuta satellite yoyote ile.

2. Hatua inayofuata ni kufunga dish pole (ule mlingoti wa kuwekea dishi lenyewe). Hakikisha ile mlingoti umesima wima kwa nyuzi 90 (Ni muhimu sana hili) unaweza pima kwa kutumia kipima pembe au pima maji. Angalia hii picha
hqdefault-jpg.387977
elevati;n

3. Baada ya hapo ni kuweka dish lako sasa kwa kufuata vipimo ulivyopata hapo juu (Elevation, azimuth na lnb skew). Kuweka elevation angle 80.8 tumia alama zilizowekwa kwenye dishi mfano angalia picha hii hapo kuna kuanzia 0 hadi 90. elevation angle hutofautiana kutokana na satellite unayouitafuta, kwa mfano kwa hiyo ya dstv ni 80.8 na Eutelsat 7 (azam wanaporusha matangazo) ni 51.6 hivyo utakweka hapo kwenya hizo alama za dishi. kama dishi lako halina alama hizo unaweza kutumia kipima pembe kama hicho kenye picha hapo juu.
images-png.387978

adjustment-jpg.387981


4. Hatua inayofuata ni kuweka azmuth angle (uelekeo wa dishi kwa kuzungusha kulia au kushoto ukiwa nyuma ya dishi). Kifaa ninachotumika ni compass (dira), hichi kipo hata kwenye smartphone na uelekeze kwenye nyuzi 334.2

5. Katika hatua hii ni kuweka uelekeo wa lnb (Lnb skew angle) ukiangalia pale unapoweka lnb kuna alma pia za kuweka, angalia mfano kwenye picha hii
lnbf-skewing-angle-check-jpg.387986


Ukifuata hatua hizi 5 unapata satellite yoyote unayouitaka ndani ya muda mfupi sana dakika 10 nyingi siyo kubahatisha tu vitu vinaenda kwa vipimo kila kitu kipo kutokana na satellite unayoitaka. satellite zingine signal yake ni weak mfano Nilesat ukisema utafute kwa kuzungusha tu dish kwa kubahatisha unaweza kumaliza siku nzima hujaipata ila ukifuata vipimo vyake unaipata haraka sana.

Unaweza uelewa zaidi kwa kuangalia video hii youtube

View attachment 387957 View attachment 387977 View attachment 387978 View attachment 387981 View attachment 387986

Azimuth, lnb scew,elevation zitafanana maeneo yote?? Inamana nikitumia hiyo lnb scew ,elevation na azimuth nikiwa lindi vipimo vilevile nitatumia nikiwa mwanza? Sio kadri unapo hama position kuna vipimo vina badirika hasa vya uelekeo wa dish ?
 
Kwa wale mafundi wa madish tu,naomba namba yako ya simu hapa yenye akaunti ya whatsapp au PM nikuunge kwenye group kwa lengo la kubadilishana ujuzi tu
 
hilo eneo nililokuelekeza hutakosa, wana vifaa karibia vyote vya madishi.
Mkuu me nahitaji kutumia decoder moja kwa tv mbili tofauti. Niweze kuangalia channels tofauti kwa wakati mmoja. Kuna solutions rahisi kweli?
Nimejaribu kucheck mitandaoni naona Nigeria wana dual tuner receiver. Una uzoefu nazo? Na je zinapatikana bongo?
Thanks
 

Attachments

  • 7B4B8B8A-E70A-4EA7-8C41-A7D6651DEEE1.png
    7B4B8B8A-E70A-4EA7-8C41-A7D6651DEEE1.png
    195.6 KB · Views: 101
Mkuu me nahitaji kutumia decoder moja kwa tv mbili tofauti. Niweze kuangalia channels tofauti kwa wakati mmoja. Kuna solutions rahisi kweli?
Nimejaribu kucheck mitandaoni naona Nigeria wana dual tuner receiver. Una uzoefu nazo? Na je zinapatikana bongo?
Thanks
hata dstv wanazotumia kwenye mabanda ya mpira zipo hivyo, receiver moja inatoa chanell mbili tofauti.

sina uhakika kama zipo ila tembelea hapo msimbazi nyuma ya jengo la simba nina imani utazikuta tu.
 
"...msimbazi nyuma ya jengo la simba nina imani utazikuta tu. ..."
...
Nimepotea sijui!? Ila ukiwa jengo la simba unaelekea polisi kuna jengo lenye handaki nyuma yake ndo kuna duka lina madishi kwa nje na ndani kuna makorokoro mengi ya visimbisi...ila wafanyakazi hawana morali ya kuhudumia... sijui ndo hapo?!
Ila nyuma ya simba, majengo pacha, redstar, ..kama vile sikupata kitu... ila kama una kalink ka location ... itapendeza zaidi!
...
 
Nataka Chanel zote za azam na baadhi ya sports free. Inawezekana?
 
...
Nimepotea sijui!? Ila ukiwa jengo la simba unaelekea polisi kuna jengo lenye handaki nyuma yake ndo kuna duka lina madishi kwa nje na ndani kuna makorokoro mengi ya visimbisi...ila wafanyakazi hawana morali ya kuhudumia... sijui ndo hapo?!
Ila nyuma ya simba, majengo pacha, redstar, ..kama vile sikupata kitu... ila kama una kalink ka location ... itapendeza zaidi!
...
yap hapo kwenye handaki, mtaa wa nyuma ni kama kichochoro hivi (huingii kwenye handaki unapita hilo jengo kwa nyuma)

maduka yapo mengi ila kuna moja kama unakunja kushoto unaliface kwa mbele, jina lake nimelisahau kidogo, mimi hununulia hapo.

hapo madalali wengi inabidi uingie mwenyewe madukani.

ngoja huyu atakusaidia zaidi
Njunwa Wamavoko
 
Habari wanajukwaa!
Naomba kujuzwa kuhusu rcvr bora Kwa sasa itayoniwezesha kupata fta channels za movies, news, na documentaries. Naomba mawazo pia kama strong srt 4922 itanifaa.

Natanguliza shukrani.
 
kama unataka kusearch satelite bila kubahatisha unatakiwa uwe na satelite finder, unaweza kuhunt satelite bila hata kuliangalia hilo dishi. na kama mfuko wako upo vizuri zipo hadi zenye built in tv na receiver ukienda site unabeba tu satelite finder yako yenye ukubwa kama simu huna haja kuhangaika na tv na decoder.
06%E4%BA%A7%E5%93%81%E4%BB%8B%E7%BB%8D1.jpg
Mkuu nitaipataje hii kitu? Na bei yake itakuwa ambayo ni high quality
 
Mkuu Idimi,
Nina receiver ya Hometech 940ii combo na 6ft dish. Jamaa amenifungia NSS 12 at 57°E, ameshindwa kufunga lnb nyingine, lakini kwa receiver hii hakuna updates za software kwa sasa hivyo nashindwa kuangalia sports.

Naweza kupata msaada wa updates au kufunga Intelsat 20 at 68.5°E ili nipate walau Sony, Discovery na HBO?

Msaada tafadhali.
 
Je kuna mtu anayeweza kuset dish kwa kutumia app zilizopo play store? Naomba msaada wa kuzitumia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom