Njoo kesho kwenye interview: Kauli inayokwamisha wengi

Window7

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
4,094
3,020
Unakuta uliomba kazi miezi miwili imepita, basi ukaamua kurudi mkoani kufanya biashara zako.. Mara unapokea simu kisha unaambiwa "Jina lako limechaguliwa miongoni mwa waombaji watakaofanyiwa usaili hapo kesho saa 6 mchana"

badala ya kufurahi unaanza kuwaza kutoka huku mbwinde mpaka Dar es salaam ni masaa 12.. Kwa nini hawatoi taarifa kabla walau hata siku mbili?

Waajiri wa namna hii hua sielewi lengo lao ni nini, na wapo wengi Bongo hii natamani kujua siri yao.. Kwa nini wanapenda njoo kesho?
 
Unakuta uliomba kazi miezi miwili imepita, basi ukaamua kurudi mkoani kufanya biashara zako.. Mara unapokea simu kisha unaambiwa "Jina lako limechaguliwa miingoni mwa waombaji watakaofanyiwa usaili hapo kesho saa 6 mchana"

badala ya kufurahi unaanza kuwaza kutoka huku mbwinde mpaka Dar es salaam ni masaa 12.. Kwa nini hawatoi taarifa kabla walau hata siku mbili?

Waajiri wa namna hii hua sielewi lengo lao ni nini, na wapo wengi Bongo hii natamani kujua siri yao.. Kwa nini wanapenda njoo kesho?
kwa uzoefu wangu mdogo wa masuala ya ajira ... kapuni nyingi au taasisi zinazoheshimika ... haziwezi kukupa 24 hours ujiandae kwa usaili.. ukiona hivyo ujue hizo ni kampuni au vitaasisi vidogo dogo vya uchochoroni.............
 
Ila hiyo ni ishara ya namna ambavyo taasisi husika imejaa uswahili. Taasisi majini hazifanyi hivyo.
 
kwa uzoefu wangu mdogo wa masuala ya ajira ... kapuni nyingi au taasisi zinazoheshimika ... haziwezi kukupa 24 hours ujiandae kwa usaili.. ukiona hivyo ujue hizo ni kampuni au vitaasisi vidogo dogo vya uchochoroni.............
Ulishaomba kazi UN UNICEF UNDP UNHCR? unaombakazi baada ya miaka miwili ndio unapigiwa simu halafu anayekupigia sijui mhidi au mfilipino? kuelewana shughuli, badae wanakwambia uende sijui nairobi, yaani tabu tupu.
 
Mkuu hapo kuna ukweli, wengi tunafanywa chambo kuitwa kwenye interview kurupushi.
Wanaangalia utayari wa mtu. Je wewe ni mtu wa excuses? Do you really need a job? Are you competent enough to show up anytime? Kama wewe ni mtu wa kubahatisha huwezi.... Halafu pia kama Uko mkoa huo Huo why usiende kesho yake? Kama upo mbali unaweza waeleza they are human beings.. Inaweza pia ni sehemu ya interview. Usifeli mapema hivo Kwa kuogopa kusema ukweli
 
kwa uzoefu wangu mdogo wa masuala ya ajira ... kapuni nyingi au taasisi zinazoheshimika ... haziwezi kukupa 24 hours ujiandae kwa usaili.. ukiona hivyo ujue hizo ni kampuni au vitaasisi vidogo dogo vya uchochoroni.............
Kweli kabisa.
 
Dah,umenikumbusha kitu:
Nilifanya interview company flani huko Tanzania mjini (DSM), baada ya interview waliahidi kutuita ndani ya hiyo week, nilisubiri kwa wiki mbili ili niwe karibu na Tanzania mjini mpaka nikakata tamaa.
Nilipoamua kuondoka na kuendelea na ratiba zangu huko kijijini nikapigiwa simu kesho yake niende kwenye interview ya pili saa 3 asubuhi tena nikiwa njiani kwenye bus hata huko kijijini kwetu bado sijafika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom