KAMWENE,hali ya siasa Njombe imezidi kubadilika baada ya uchaguzi mdogo wa vijiji na vitongoji kufanyika tarehe 2.12.2012.Katika moja ya kijiji ambacho CCM ilidhani ingeshinda kwa kishindo kwa kutumia fedha na kanga.Bahati haikuwa yao.Kijiji hicho kinaitwa Igima.Makada wa CCM walipanga kuanza kazi ya kulazimisha ushindi wa mezani saa 7 usiku,kwa bahati nzuri makamanda nao walijua mbinu za kizamani za CCM.Wakaamua kuweka doria na ilipofika saa 7.usiku ndipo shughuli ilipoonza.Mara makada wakatoka kwenye nyumba ya balozi wao.Baada ya kutembea umbali wa m.10 tu walikutana na JU CDM ambapo katibu wa CCM wa kata na makada wenzio walipata kipigo cha mbwa mwizi hadi wakapotea na kesho yake CHADEMA wakashinda kwa kishindo kijiji pamoja na kitongoji.
Ushindi wa CDM umesababisha maumivu makali kwa CCM ambao jana waliamua kwenda polisi na kumfungulia mashtaka mwenyekiti aliyeshinda.Leo mahakamani katika mahakama ya Njombe kila mtuhumiwa alitakiwa kuwa na wadhamini 2.Na kweli wamefanya hivyo.Chaajabu ulipofika muda wa kuwawekea dhamana hakimu bila mishipa ya aibu akasema barua aliyoandika mtendaji wa kijiji cha Igima haina kumbukumbu namba wala simu ya mtendaji aliyeandika barua ya kuwatambua wadhamini.Kitendo hicho kimesababisha mwenyekiti mpya aende lupango(gerezani)hadi jumatatu kitu ambacho kwa kweli kinasikitisha sana.Hivi kweli hakimu anakataa barua eti haina simu ya mtendaji au barua haina ref.nr.Huu kama uhuni ni nini?Mtendaji aliandika barua vizuri na mhuri akagonga,je,hakimu haoni haja ya kuwasaidia wananchi au naye ametumwa na CCM?