Njombe,siasa hadi mahakamani.aibu kubwa na fedheha kwa learned brothers

lutondwe

Senior Member
Dec 20, 2010
150
195
KAMWENE,hali ya siasa Njombe imezidi kubadilika baada ya uchaguzi mdogo wa vijiji na vitongoji kufanyika tarehe 2.12.2012.Katika moja ya kijiji ambacho CCM ilidhani ingeshinda kwa kishindo kwa kutumia fedha na kanga.Bahati haikuwa yao.Kijiji hicho kinaitwa Igima.Makada wa CCM walipanga kuanza kazi ya kulazimisha ushindi wa mezani saa 7 usiku,kwa bahati nzuri makamanda nao walijua mbinu za kizamani za CCM.Wakaamua kuweka doria na ilipofika saa 7.usiku ndipo shughuli ilipoonza.Mara makada wakatoka kwenye nyumba ya balozi wao.Baada ya kutembea umbali wa m.10 tu walikutana na JU CDM ambapo katibu wa CCM wa kata na makada wenzio walipata kipigo cha mbwa mwizi hadi wakapotea na kesho yake CHADEMA wakashinda kwa kishindo kijiji pamoja na kitongoji.
Ushindi wa CDM umesababisha maumivu makali kwa CCM ambao jana waliamua kwenda polisi na kumfungulia mashtaka mwenyekiti aliyeshinda.Leo mahakamani katika mahakama ya Njombe kila mtuhumiwa alitakiwa kuwa na wadhamini 2.Na kweli wamefanya hivyo.Chaajabu ulipofika muda wa kuwawekea dhamana hakimu bila mishipa ya aibu akasema barua aliyoandika mtendaji wa kijiji cha Igima haina kumbukumbu namba wala simu ya mtendaji aliyeandika barua ya kuwatambua wadhamini.Kitendo hicho kimesababisha mwenyekiti mpya aende lupango(gerezani)hadi jumatatu kitu ambacho kwa kweli kinasikitisha sana.Hivi kweli hakimu anakataa barua eti haina simu ya mtendaji au barua haina ref.nr.Huu kama uhuni ni nini?Mtendaji aliandika barua vizuri na mhuri akagonga,je,hakimu haoni haja ya kuwasaidia wananchi au naye ametumwa na CCM?
 

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,774
2,000
Haki ya mtu haipotei ili mradi ujinga umeanza Mkoani Njombe,Iringa na Mbeya wasogee tu karibu maana apewe support mwenyekiti mpya vinginevyo mchezo utanoga
 

tweve

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
694
195
mwisho wa ccm umeshafika sasa,hii yote ni kutapatapa tu maana mtu anapokaribia kufa lazima anyoshenyoshe miguu hatimae hufa.hizi ndo dalili za ccm kufa
 

msemakwelii

JF-Expert Member
Sep 12, 2011
216
0
Ayaa kwani Mahakama iko chini ya nani, C chini ya CCM wewe ulitegemea nini hapo, Mmeshinda Uenyekiti Kijiji na Kitngoji na Mahakama tena ,
 

nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,956
2,000
Bora waende mahakamani lakini wakiwa tayari wameshashinda, hongera wana igima tupo nyuma yenu..
 

SoNotorious

JF-Expert Member
Sep 11, 2011
2,422
1,195
using the court as tyrannic tool wont help this regime from falling. we are just seeing the last days of this party, its death will be harder and taking some life of the innocent and helpless.
 

Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,428
1,500
hao ndio aina ya mahakim ambao wanapata kazi kwa fadhila anaowapigia kelele Tundu Lissu kila siku ila siku zao zinahesabika hakuna mabaya yasokuwa na mwisho! poleeeni saana ukombozi huambatana na hayo yote
:A S angry:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom