Aliyoyaongea MAGUFULI Njombe:;
Nitawahudumia watanzania kwaajili ya maendeleo yao na si vyama vyao
Mtu anayehusika na maji hapa aanze kujiandaa mradi utoe maji kabla sijaapishwa...nataka serikali ya vitendo
Watanzania wamechoka ahadi wanataka watendaji Mimi ni mtendaji.. nilikuwa ninatumwa sasa nataka niwatume
Njombe imekuwa mkoa sasa ninawaahidi kuboresha miundombinu...waziri wa ujenzi nitakayemteua kazi yake ya kwanza itakuwa kutengeneza barabara yenu
Matatizo ya Wananjombe ni Mbolea. Natambua na ninaahidi kutatua hilo, niendeleze kazi nzuri za awamu zilizotangulia
Nchi hii sio wote ni wafisadi na wanarushwa ila wapo wachache wala rushwa na mafisadi. .nitawaundia mahakama kutokomeza hili..nafahamu mafisadi hawafurahii hili ila mimi nataka wengi wafurahi na si mafisadi wachache
Kitanda kikiwa na kunguni hukitoi ukatupa bali unatoa kunguni unawaua unalala vzuri kwa starehe, kunguni wameshaanza kutoka..Tafadhal msikutupe ktanda ccm
Zipo nchi kama China walifanya mabadiliko ndani ya chama kwa kuwachoma kunguni wabakize kitanda chao leo hii china ni first word country
Tanzania inahitaji mabadiliko bora na Si bora mabadiliko
Ninawaambia wale wanaosema pipoz power ile power wamempe magufuli...hata wale wa Cuf wanaotoa alama ya ngumi yaani vidole vitano wananipa baraka niwe ŕais watano hata ccm wanaotoa alama ya dole wanamaanisha magufuli ni namba wani
Hakuna aliyezaliwa kupata mateso kila mtu anataka maendeleo mambo ya vyama yanatupotezea muda nataka kuleta mabadilikoyaliyo bora kwa watu wote
Serikali yangu itakuwa ya mawaziri wachache amabao lazima wajipambanue kuhudumia wananchi
Hakutakuwa na karo kuanzia la kwanza mpaka kidato cha nne. Hii siyo siasa mimi ni mtendaji na kwangu ni kazi tu
Tunataka nchi yetu itoke kwenye uchumi wa chini iende kwenye uchumi wa kati
Naomba watanzania tuwe wamoja tumtangulize mungu mbele tusibaguane kwasababu ya dini zetu na vyama vyetu. Tuishi kama ndugu
Tushikamane pamoja kwaajili ya kuleta maendeleo. Tutunze amani yetu maana bila amani hakuna maendeleo
Wanafunzi wa chuo kikuu watapata mikopo bila kugoma na kwa wakati. Nawataka wanafunzi msome hata mimi nmesomea hapa Tanzania. ..ila mkiçhukua mkopo msome kweli
Tutajenga nyumba za walimu na kukidhi madai yao kama ya likizo n.k kwani tunafahamu kero za walimu na tutazibeba vivyohivyo kwa wafanyakazi wengine kama maaskari
Wakati wangu jambazi akija mchape risasi nataka nchi hii iwe na amani wafanya biashara wafanye kazi usku kucha bila bugudha wala uoga
Jeshi la polisi wapate mshahara wa kutosha JWTZ tutajenga nyumba zao
Wafanyakazi wa kawaida tutawaangalia kwa ukaribu na hili ni kwa kukusanya kodi kwa usahihi
Tanzania hii fedha zipo...kuna madini, wanyama pori ..kama wamasai na wasukuma wanavyomchunga ng'ombe ndivyo hivyo wanyama pori wetu watakavyochungwa
Hatutaķi watu wachache wanufaike kwa maliasili nataka tunufaike wote
Emilly: Huyu ndiye John Joseph Pombe Magufuli...unaweza sahau John au Joseph lakini nina imani hamuwezi sahau pombe
Nataka niwafunge Makufuli mafisadi
Wasanii watanzania wamekuwa waganga njaa, ninawaahidi sintowatumia kipndi cha kampeni nitaanzisha mfuko maalum wa wasanii
Waandishi wa habari, wajasiriamal, waendesha bodaboda, mama ntilie nitahakikisha kero zenu zimekwisha hakutakuwa na kukamatwa hovyo wala kodi zisizo rasmi
Tunataka kuijenga Tanzania mpya
Tanzania moja