Njombe kusini, ni nyagawa, rose mayemba, fakii lulandala, kazimoto, au emmanuel masonga 2015.

why

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
203
0
SAM_0571.JPG SAM_0562.JPG SAM_0569.JPG fk.jpg fk2.jpg KZ.jpg LA.jpg N A.jpg RM 2.jpg fk.jpg


je kati ya hawa vijana, masonga,lulandala, nyagawa, kazimoto na rose mayemba, nani atanguzruma kupitia chadema 2015. Maoni yenu nani anafaa ni muhimu pia.ni katika jimbo la njombe mjini.
 

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,935
2,000
Why, sijajua ni kwanini umekuja na uchambuzi huu...of course si lazima mtoa mada yeyote humu jukwaani watu wajue kwanini ametoa mada husika. Lakini ni machache ya kuzungumza kwa faida yako na wengine wenye mtazamo kama wako kuhusu Njombe Kusini.
1. Kwsasa si wakati wa kuwajua na kuchambua wataopeperusha bendera ya CHADEMA Njombe Kusini, wakati wa kujenga na kuimarisha Chama katika ngazi ya Kata na Vitongoji hadi Misingi. Ikiwa ni mkazi wa Jimbo hilo unatakiwa kufahamu kuwa kuna vitongoji CCM kimekuwa kama chama cha ukoo.
2. Majina ya wagombea kupitia CHADEMA yatajulikana na kupigiwa kura 2015 na wanachama wenyewe: Yakijumuisha majina yale ya wale walioonyesha nia na kutuma CV zao Makao Makuu pamoja na wale watakaoibuka wakati ukifika huko huko Njombe. Ndipo wanachama watachambua nani anafaa. Kigezo kimojawapo tutawapima katika michango yao kwenye ujenzi wa Chama. Mara nyingi si mara zote, asiyeshiriki ujenzi huwa haumizwi akiambiwa unakiua chama, hufanya anayotaka yeye.
3. Mtindo wa kujitangaza mapema unamfanya muhusika kuwa target nzuri kwenye kuangushwa na CCM. Msifikiri wanalala....muulizeni Nyagawa (Alatanga ) japo kwa ufupi namna propaganda na mbinu chafu dhidi yake zilivyotumiwa na timu ya Makweta (R.I.P.) na ya Deo Sanga (Jah People). Halafu kajifunze zile za Njombe Magharibi.
4. Iko wazi kuwa Deo Mwanyika (yule wa Barrick Gold) anataka kugombea Ubunge kupitia CCM. [Kumbuka 2010 Makinda na waliomuweka Makinda walimwambia zamu yake nu 2015]. Sasa timu yake Mwanyika inakazana sana kupenyeza mamluki na kutaka kujua nani atakuwa tishio kwao. Hivyo vi tisheti wanavyovalishwa vijana wa Njombe sasa na vimisaada uchwara si bure. Kuna karata zinachangwa. Msiwe wepesi wa kuonyesha silaha zenu.

Nafikiri Why umejifunza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom