Waraka kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Njombe, Bibi Rose Mayemba kwenda kwa Askofu Mwamakula

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
WARAKA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA NJOMBE, BIBI ROSE MAYEMBA KWENDA KWA ASKOFU MWAMAKULA.
Hello Bishop! Heshima yako!
Ninaitwa Rose Mayemba, Mwenyekiti wa CHADEMA Njombe. Leo tarehe 3 Septemba 2020, tumetoka gerezani hapa Njombe ambako tulikwenda kuwasalimia wenzetu, story zao zinatisha sana.Wanasema walipigwa na kuteswa sana huku wakilazimishwa wamtaje Mgombea wa Ubunge Emmanuel Masonga, Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe, Bi Rose Mayemba na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa wamewatuma kufanya mauaji. Wanafuatilia simu zetu zote muda wote kututafutia makosa ya kutuweka ndani.

Walipelekwa kwa Mlinzi wa Amani wakiwa chini ya ulinzi mkali na kutishiwa kuvunjwa miguu kama watakataa kuhusika na mauaji hayo hivyo kila mahali walipohojiwa walilazimika kukubali ili kukwepa maumivu. Leo tulipowaona walikuwa bado wanachechemea huku wakilalamika kwamba uti wa mgongo bado una maumivu makali...

Lakini wanawasalimia sana wanasema wao wako imara. Wanaomba msife moyo. Wanaamini haya ni mapito tu hivyo iko siku yatakwisha.
Aliyekuwa anazungumza na sisi wawili (mimi na Mgombea Ubunge) ni George Sanga ambaye ni mtuhumiwa na pia Mgombea wa Udiwani katika Kata mojawapo na Katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Mjini na alikuwa anawakilisha watuhumiwa wenzake. Lakini waliokuwa wanasikia ni wengi maana tuliingia pia na Mchungaji wa kanisa lake na mkewe na watu wengine wengi...
 
Nadhani ni muda sasa wa kuyaangalia haya mambo kwa jicho la mbali zaidi ili kuwaokoa wenzetu wanaoteswa kwa tuhuma ambazo hawajazifanya..

Siku zote tunasikia tu kuwa sijui wanateswa,mara wanalawitiwa,mara sijui wanaibgizwa chupa nyuma na mateso mengine kibao tgen ndo inakuwa imetoka mwishowe tunasikia wamekufa baada ya mateso makali ss najiuliza hv kweli ubinaadamu umetutoka jumla kiasi kwamba huwa hatuyahisi haya magumu wanayopitia wenzetu???

Tafakari na uanze kuchukua hatua kuanzia sasa..
 
Hakika inasikitisha sana. Na bado kuna mtu kwa utashi wake anaweza kupanga foleni kuchagua utawala huu wa kishetani namna hii?
Nadhani kama unayajua haya kisha unaichagua CCM basi hata shetani mwenyewe anaweza kukushangaa kuwa mapenzi yako kwake ni zaidi ya huba
 
Ccm inawatesa raia wema,kuwasingizia/kuwaammbika kesi kubwa kubwa ili kuwatisha wapiga kura.
Dhambi hii haiwaachi.
Lissu ndani ya siku 100 atawatoa wote na kuwafidia,tuitengeneze Tanzania mpya.
Kura zote kwa Lissu
 
Hakika inasikitisha sana. Na bado kuna mtu kwa utashi wake anaweza kupanga foleni kuchagua utawala huu wa kishetani namna hii?
Nadhani kama unayajua haya kisha unaichagua CCM basi hata shetani mwenyewe anaweza kukushangaa kuwa mapenzi yako kwake ni zaidi ya huba
Mashehe ubwabwa na maaskofu sadaka wataisoma hii?
 
Bado natafakari askofu Kama pengo na yule shehe ubwabwa wa dar tuwafanye Nini?
Kazi ya kuwaadhibu tumwachie Mungu,sisi tutende mema na kuwaletea maendeleo Watanzania.
Lissu alisema" hatawapitisha kwenye maumivu aliyapitia" huu ni utume uliotukuka.Mungu atie mkono wake.
 
Wengi wanaonewa sana hii nchi, na zaidi kama wakiwa wapinzani, binafsi nilivyoiona ile taarifa ya DPP kwamba hao watu wamekiri kuhusika na mauaji sikuamini kabisa.

Huu ni mchezo tu ulioandaliwa kuwaengua hao wagombea wa Chadema - Tunduma ambapo chama kina nguvu sana, mbaya zaidi wametumia mbinu mbaya zaidi kuwaengua kwa kuwabambikia kesi ya mauaji, nasema Mungu alie mkuu wa haki atawalipa wote waliohusika kuwaweka ndani hao watu kwa kadri ya matendo yao, malipo ni hapa hapa duniani.
 
Njbe wamesema watapiga kura hivyo hivyo hata wakiwa gerezani.
 
Hii Ndio serikali ya Magufuli
Katika history ya nchi yetu hatujawahi kupata kiongozi anatesa watu wake hivi
Kwa muda wake amwatesa Sana wapinzani na viongozi wa dini has a waislamu
Kwa miaka mi5 hii kuna watu wengi wametuhumuwa kesi za ugaidi kuliko Afghanistan na Iraq
Huyu mtu katili Sana hata akiongoza miaka Mia mwisho wake upo
 
Back
Top Bottom