SoC01 Njombe: Jinsi wananchi wanavyochagiza Maendeleo katika kata ya Makowo

Stories of Change - 2021 Competition

Faith Luvanga

Member
Aug 21, 2018
14
15
Kwa zaidi ya miaka kumi wananchi wa kata ya Makowo iliyopo Mkoani Njombe, wamekuwa wakiishi bila kupata huduma stahiki za Afya kutokana na kukosekana kwa miundombinu rafiki katika kata hiyo.

d852184d-39b5-4d3b-9c35-12816d225019.JPG




Hapo awali wagonjwa hasa akina mama wajawazito na watoto wachanga walikuwa wakifariki kutokana na kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika vituo vya Ikonda na Kibena.

Diwani wa kata hiyo, Pilimini Mgaya, aliweza kuwashawishi wananchi wake waweze kuchangia pesa kwaajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ambapo wananchi waliitikia wito huo na kuanza kuchangishana michango ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ugumu wa matibabu na kuokoa vifo vya wananchi.

Wananchi hao waliweza kuchangia kiasi cha Tsh. Mil.40 na serikali ya kijiji ilitoa eneo na kufanikiwa kuanza ujenzi wa kituo.

IMG_7033.JPG






Diwani hakuishia hapo, aliweza kupeleka taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe na kumueleza adha wanayokumbana nayo na hatua waliyochukua kama kata na vijiji vyake.

Halmashauri ya mji iliwachangia kiasi cha sh. Mil.57 baada ya kupata taarifa hiyo na kuona nguvu walizowekeza wananchi ambapo kituo hicho kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Njombe, Dr. Yesaya Mwasubila, kina viwango vya juu kikiwa na jengo la mama na mtoto, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kufulia, jengo la mionzi, jengo la maabara,jengo la upasuaji na ofisi zake.

Baada ya kituo hicho kukamilika kwa 90% kata hiyo ilipata neema ya kutembelewa na mbunge wa jimbo hilo, Deo Mwanyika ambapo aliwapongeza wananchi na Diwani wao kwa hatua hiyo huku akiushukuru uongozi wa halmashauri ya mji huo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi ambapo aliahidi kufanyia kazi changamoto za vifaa tiba, idadi ya wauguzi na kuboresha miundombinu zaidi ikiwemo Barabara.

Mwanyika aliahidi kuhakikisha anamleta waziri wa TAMISEMI Ummy Mealimu ili aweze kujionea juhudi za wananchi na serikali iweze kuweka mkono wake.
IMG_3136.JPG





Hayawi hayawi yakawa baada ya mwezi mmoja tu Waziri Ummy alitia timu katika kata hiyo na kuahidi kuleta wataalamu wa afya wa kutosha na kuleta vifaa tiba vinavyogharimu Tshs.Mil.300 ili kituo hicho kiweze kufanya kazi pamoja na gari ya kubeba wagonjwa yaani ambulance. Ilikua ni furaha kwa wananchi wa kata hiyo kuona juhudi zao zimezaa matunda na kuona sasa wanakwenda kuondokana na changamoto za kiafya zilizokua zikiwakabili kwa zaidi ya miaka kumi.
IMG_7039.JPG



Kata ya Makowo ina vijiji vitatu na vitongoji sita; Kukamilika kwa kituo hicho cha afya kutasaidia kutatua changamoto za vifo vya akina mama wajawazito na watoto kwani walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma stakihiki, pia kutapunguza adha ya kutunza maiti kwani zahanati zote katika kata hiyo hazina vyumba vya kuhifadhia maiti aidha kutasogeza karibu huduma za upasuaji ambapo zitaokoa gharama na muda ambao wananchi walikua wakitumia kufuata huduma za afya.

Lakini pia kituo hicho hakitatoa huduma kwa kata ya Makowo pekee bali katika kata za jirani ikiwemo Matola, Lugenge na Luponde.






IMG_7031.jpg


IMG_7035.jpg


IMG_7038.JPG
 
Back
Top Bottom