Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,641
- 698,079
Historia ya njiwa inaanzia mbali, lakini walau ni pale nyakati za Nuhu na gharika. Baada ya mvua ile ya siku 40, na kwa wakati huo technology ilikuwa ya kihenga, Nuhu hakuweza kujua kama maji yameshapungua ama la kukauka juu ya uso wa dunia. Hivyo aliamua kumtuma bwana kunguru akaangalie(hapa kuna dhana mbili 1. Mawasiliano ya binadamu na kiumbemnyama, 2. Kunguru kama ndege mwerevu)
Dhana ya kumtuma ndege arukaye ni kwa ajili ya kuona mbali zaidi. Kunguru alitoka na hakurudi.. (Kunguru hafugiki, haaminiki)
Baada ya Nuhu kuona kimya na kunguru harudi, aliamua kumtuma ndege mwingine na safari hii alimteua hua mweupe(njiwa), huyu alienda na akarudi na jani bichi/la kijani la mzeituni... Ishara ambayo ilionyesha uhai ardhini... Njiwa si kwamba alirudi tu bali alirudi na ushahidi(ishara ya weledi na tafakuri)
Tangu hapo njiwa akaanza kutumiwa kwa ajili ya kupeleka jumbe mbalimbali lakini pia akitumika kama alama na ishara ya amani sehemu mbalimbali duniani
Cha kushangaza zaidi ni matumizi ya jani la mzeituni, mzeituni ni mmea wenye maajabu mengi, na unatumika hata kwenye mambo ya tiba za asili... Mitume na manabii na watu wengine walitumia majani yake kulaki ama kushangilia watu(rejea habari za Bwana Yesu alipoingia Jerusalem)
Je ni kwanini njiwa aliamua kutumia jani la mzeituni na si mti mwingine wowote? Bado tuna mengi ya kuhoji katika ufunuo wa kiroho..... Ni kama vile ulimwengu huu hesabu zake zilishapigwa kitambo Kwahiyo kinachofanyika ni kukokotoa tuu
Sent using Jamii Forums mobile app