Njiwa mweupe: mjumbe wa amani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
dcc29ed9572314067d70e5350b20ca46--power-animal-peace-dove.jpg
Kwenye maandiko akitajwa kama mnyama mpole, na kwa wakristo wakimtumia kama alama ya roho mtakatifu, njiwa amekuwa akitumika kama alama na ishara ya amani duniani kote kiimani na hata katika mambo ya kidunia kisiasa na hata kwenye kusuluhisha migogoro ya nchi na nchi, vitani nk nk
main-qimg-a8c447dc53631bcfa167bce9e444d250.png

Historia ya njiwa inaanzia mbali, lakini walau ni pale nyakati za Nuhu na gharika. Baada ya mvua ile ya siku 40, na kwa wakati huo technology ilikuwa ya kihenga, Nuhu hakuweza kujua kama maji yameshapungua ama la kukauka juu ya uso wa dunia. Hivyo aliamua kumtuma bwana kunguru akaangalie(hapa kuna dhana mbili 1. Mawasiliano ya binadamu na kiumbemnyama, 2. Kunguru kama ndege mwerevu)
Dhana ya kumtuma ndege arukaye ni kwa ajili ya kuona mbali zaidi. Kunguru alitoka na hakurudi.. (Kunguru hafugiki, haaminiki)
Baada ya Nuhu kuona kimya na kunguru harudi, aliamua kumtuma ndege mwingine na safari hii alimteua hua mweupe(njiwa), huyu alienda na akarudi na jani bichi/la kijani la mzeituni... Ishara ambayo ilionyesha uhai ardhini... Njiwa si kwamba alirudi tu bali alirudi na ushahidi(ishara ya weledi na tafakuri)
Tangu hapo njiwa akaanza kutumiwa kwa ajili ya kupeleka jumbe mbalimbali lakini pia akitumika kama alama na ishara ya amani sehemu mbalimbali duniani
Cha kushangaza zaidi ni matumizi ya jani la mzeituni, mzeituni ni mmea wenye maajabu mengi, na unatumika hata kwenye mambo ya tiba za asili... Mitume na manabii na watu wengine walitumia majani yake kulaki ama kushangilia watu(rejea habari za Bwana Yesu alipoingia Jerusalem)
Je ni kwanini njiwa aliamua kutumia jani la mzeituni na si mti mwingine wowote? Bado tuna mengi ya kuhoji katika ufunuo wa kiroho..... Ni kama vile ulimwengu huu hesabu zake zilishapigwa kitambo Kwahiyo kinachofanyika ni kukokotoa tuu
6a00d83462eb8d69e2010535e4cfce970b-250wi.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 558417Kwenye maandiko akitajwa kama mnyama mpole, na kwa wakristo wakimtumia kama alama ya roho mtakatifu, njiwa amekuwa akitumika kama alama na ishara ya amani duniani kote kiimani na hata katika mambo ya kidunia kisiasa na hata kwenye kusuluhisha migogoro ya nchi na nchi, vitani nk nkView attachment 558418
Historia ya njiwa inaanzia mbali, lakini walau ni pale nyakati za Nuhu na gharika. Baada ya mvua ile ya siku 40, na kwa wakati huo technology ilikuwa ya kihenga, Nuhu hakuweza kujua kama maji yameshapungua ama la kukauka juu ya uso wa dunia. Hivyo aliamua kumtuma bwana kunguru akaangalie(hapa kuna dhana mbili 1. Mawasiliano ya binadamu na kiumbemnyama, 2. Kunguru kama ndege mwerevu)
Dhana ya kumtuma ndege arukaye ni kwa ajili ya kuona mbali zaidi. Kunguru alitoka na hakurudi.. (Kunguru hafugiki, haaminiki)
Baada ya Nuhu kuona kimya na kunguru harudi, aliamua kumtuma ndege mwingine na safari hii alimteua hua mweupe(njiwa), huyu alienda na akarudi na jani bichi/la kijani la mzeituni... Ishara ambayo ilionyesha uhai ardhini... Njiwa si kwamba alirudi tu bali alirudi na ushahidi(ishara ya weledi na tafakuri)
Tangu hapo njiwa akaanza kutumiwa kwa ajili ya kupeleka jumbe mbalimbali lakini pia akitumika kama alama na ishara ya amani sehemu mbalimbali duniani
Cha kushangaza zaidi ni matumizi ya jani la mzeituni, mzeituni ni mmea wenye maajabu mengi, na unatumika hata kwenye mambo ya tiba za asili... Mitume na manabii na watu wengine walitumia majani yake kulaki ama kushangilia watu(rejea habari za Bwana Yesu alipoingia Jerusalem)
Je ni kwanini njiwa aliamua kutumia jani la mzeituni na si mti mwingine wowote? Bado tuna mengi ya kuhoji katika ufunuo wa kiroho..... Ni kama vile ulimwengu huu hesabu zake zilishapigwa kitambo Kwahiyo kinachofanyika ni kukokotoa tuuView attachment 558416

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeupenda uchambuzi wako mkuu, heshima kwako. Huo mzaituni umetajwa pia kwenye kitabu cha waislamu Mwenyezi Mungu akiapia kwa huo mti.
Hata leo hii unatumika kwa tiba mbali mbali hata specialist wanaurecommend kwenye hizo tiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana hapo mwisho kwenye kutafakari kwanini njiwa alirudi na jani la mzeituni na si mti mwingine wowote umenikumbusha jamaa mmoja toka nyanda za juu alikuwa muumini mzuri kanisani ila akawa anatumia mvinyo aina ya ulanzi au bamboo juice....alipoulizwa na wazee wa kanisa kwanini asitengwe kwa maana pombe imezuiliwa alissbabisha vicheko kwa sie wengine tulioshiriki kikao hicho.
Aliwajibu kuwa, kule nchi za mashariki ya kati mvinyo wao wa asili ni uliotokana na zabibu sasa kama hiyo nchi ya ahadi ingekuwa iringa ulanzi ndio ingekuwa divai na ingetumika pale altareni kama kawaida sasa yeye anatumia cha asili ana kosa gani?
Kweli pombe hajjawahi muacha MTU salama.
 
Back
Top Bottom