Njiani kuelekea Rwanda

Nfumu

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
610
698
wakuu kesho nitakuwa njiani kuelekea Rwanda(kusafisha macho tu and not otherwise) sasa nahitaji kuuliza yafuatayo

1.hotel gani nzuri ya kufikia iliyo cheap kidogo

2.mahali gani naweza badilisha pesa ya kitanzania kuwa ya Rwanda

3.inachukua masaa mangapi kufika Rwanda ukitokea Tanzania

4.je vivutio gani vizuri vinapatikana Rwanda wakati Tanzania havipo
 
Nadhani majibu yako yangejibiwa na google kwa kuanzia.

Utapangaje safari bila kuwa na taarifa muhimu kama hizo? Haupo serious.
 
Swali lako la tatu ndo limeniacha hoi zaidi, unatumia masaa mangapi kufika rwanda ukitokea Tanzaniao_O.

Unaweza tumia hata DK moja tu kuingia Rwanda kutegemeana na wewe ulipo:D:D

Lakini pia Watz hatunaga tabia kujishughulisha kufanya research wenyewe kabla ya kuuliza, mambo mengi yapo so open kwa sasa hv, haina hata haja ya kuuliza, dunia yote ipo kiganjani mwako sasa hv
 
2.Hata Rusumo nadhani utapata
3.Ukitokea Ngara hata saa moja haifiki tayari uko Rwanda,ukitokea Dar ni zaidi ya siku moja,ebu tuambie uko wapi exactly
4.Hata maeneo ya mahuaji ya kimbari, Gisenyi na Kigali kama sijakosea (yaani hapo usiache kwenda uone ni jinsi gani binadamu anaweza kuwa mnyama ndani ya muda mfupi)
 
Mpeni majibu,kama hamjui c mkaushe tu. Mbona wabongo much know sana????!!!!!?
 
wakuu kesho nitakuwa njiani kuelekea Rwanda(kusafisha macho tu and not otherwise) sasa nahitaji kuuliza yafuatayo

1.hotel gani nzuri ya kufikia iliyo cheap kidogo

2.mahali gani naweza badilisha pesa ya kitanzania kuwa ya Rwanda

3.inachukua masaa mangapi kufika Rwanda ukitokea Tanzania

4.je vivutio gani vizuri vinapatikana Rwanda wakati Tanzania havipo
toa maelezo haraka tukusaidie,kuna wenzako wanasubiria michango yetu kwenye majukwaa mengine
 
Hoteli nzuri kabisa na hautajuta ni 'Hotel Rwanda' hii walifikia watu maarufu kama Don Cheadle & Sophie ingawa ni ya gharama nafuu
 
Utatumia dakika tano kama uko hapa mpakani rusumo, ila kuna kwaya ya ambassador unaweza kwenda kupiga nayo picha ni moja ya kivutio ambacho huku kwetu hakuna.
 
Back
Top Bottom