Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Baada ya Fred kumaliza chuo alirudi kijijini kwao huko Malampaka. Fred alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa na katika elimu yake mjomba wake alisaidia sana.
Mjomba alikuwa na kampuni ya kusindika matunda.
Mjomba alimuomba dada yake, ambae ni mama yake Fred ili aje kuishi mjini kwani ilibidi mjomba ampeleke mke wake India kwenye matibabu ya cancer.
Fred aliachiwa nyumba na gari, pia aliachiwa majukumu machache ofisini na alipewa allowance ya laki nne kwa mwezi.
Fred alitaka wale wote aliosoma nao wajue maisha yake mapya. Aliwatafuta wote na kuanza kula nao bata la mjini. Laki nne kwa mwezi zilianza kuwa ndogo na Fred alimsumbua sana Meneja wa mjomba kumuongezea pesa kila mara.
Fred aliapa hataki tena umasikini, anadate watoto wa kisure tu.
Fred alikutana na Angela aliyetokea Ngara amekuja mjini baada ya kumaliza kidato cha sita na kukosa chuo. Angela amefikia nyumbani kwa Lilian ambae anaishi kwenye nyumba ya wazazi wake. Wazazi wa Lilian wanaishi Machame lakini huja mjini mara chache kwa shughuli za biashara.
Angela baada ya kutafuta kazi kwa muda mrefu aliamua kuwa mdangaji. Na yeye alitafuta wanaume high class. Katika juyaweka vizuri madanga alijitambulisha kama mtoto wa balozi yeye ameamua kuishi bongo hakutaka kumjoin msure huko ughaibuni.
Angela alipokutana na Fred ilikuwa kama mkate na siagi. Siku ambayo Fred alipewa 1.5 milioni na meneja kwa maelezo kuwa azitumie vuzuri mpaka mjomba atakaporudi ndiyo siku Angela alipoomba milioni moja ana shida nayo.
Fred alimpa ile milioni akijua ananyoosha njia kuwa mkwe wa balozi. Angela alipata ujauzito ilibidi ahamie kwa Fred. Kumbe zile pesa Angela alizokuwa anaomba alikuwa anapeleka kwao na mama alikuwa mgonjwa.
Wazee walipoona kimya muda mrefu ndipo walimfuata Angela mjini. Wakianzia nyumbani kwa Lilian ambae nae kumbe alijua baba yake Angela ni ambassador anaona wazee na makubazi wamebeba Ghana must Go.
Lilian I aliwapekeka wageni kwa Fred ambako Angela anaishi na katikati ya introduction ndipo mjomba na mkewe walipoingia kutoka India.
Fred alifukuzwa kwa mjomba kwa upotevu wa pesa na mali nyingi. Angela alimlaani Fred kwa kumharibia future. Walikwenda kujibanza kwa mmoja wa marafiki wa Fred aliyekuwa na chumba kimoja.