Njia ya maisha yangu ilipofungwa ghafla

NJIA YA MAISHA YAKO
INAPOFUNGWA GHAFLA,
SEHEMU YA MWISHO

Nilitembea asubuhi hiyo hadi
hospitalini. Nilikwenda upande wa
utawala na kuomba nimwone mama
mkubwa.

Ilikuwa ni vigumu sana
kwa sababu ya watu ambao siku
hizi wanitwa ‘wapambe’ Walikuwa
wananizuia kwa maelezo kwamba
mama mkubwa haonwi hovyo tu.


Wakati tunabishana, kwani nami
nilikuwa mkali nikiwa sijui nilitoa
wapi nguvu hiyo ya kubishana,
alitokea mamammoja mzungu
aliuliz kulikoni, ambap
walimweleza.

Alinisogelea na
kuniambia nimweleze shida yangu.
Sikumwambia kuwa niliota kuhusu
mama mkubwa bali nilimsimulia
kwa kifupi madhila yangu na
kumwambia nilikuwa nataka
msaada w kusoma.

Alinisikiliza sana
na baadae alisemaangepanga
nionane na huyo mama mkubwa.
Saambili baadae nilikuwa ofisini
kwa mama mkubwa.

Alikuwa ni
mama wa kizungu mtu mzima sana,
lakini mjanja na msikivu sana.
Nilizungumza naye kwa kirefu
nikimweleza kia kitu.

Alishindwa
kuvumilia kwani alimwaga chozi.
Hapo nikafanikiwa kupata mfadhili
wa kunisaidia kusoma. Nilikwenda
shuleni na kuendelea na masomo.
Nilikuwa ninaishi chini ya uangalizi
wa mzee mmoja aliyekuwa anaitwa
Alois, ambaye nimeambiw
ameshafariki.

Nilikuwa nikiishi
kwenye chumba kimoja karibu na
wodi ya wagonjwa hapo hospitalini.
Wale ambao bado wapo hospitalini
pale kama watumishi
wanakumbuka, bila shaka.

Nilimaliza darasa la saba na
kuanguka kwa njia ambayo bado ni
mshangao kwangu, hadi leo. Mama
mkubwa alisikitika sana.
Alimwomba Mzee Alois anitafutie
shule nirudie. Nilirudia shule
nyingine ya jirani. Mwaka mwaka
uliofuatia nilifaulu peke yangu
shuleni hapo

Niliendelea na masomo. Bila shaka
huhitaji kujua habari za shule ya
sekondari. Lakini nilimaliza kidato
cha sita mwaka 1987 na kumaliza
masomo ya chuo kikuu nchini
Uholanzi mwaka 1992.

Nilirudi
nchini na kuanza kazim kwenye
kampuni9 moja ya madini kule
shinyanga.


Mwaka 1994 nilikwenda Turiani,
lengo likiw ni kwasalimu wote
ambao nilikuw nafahamiana nao
pamoja na dada yangu. Kwa kweli
nilikuw nimemsamehe dada yangu
yule kutoka ndani kabisa ya moyo
wangu.

Niliamua kwa makusudi
niende nikashukie kwake. Nilipofika
pale nyumbani kwake kulikuwa na
mabadiliko sana.

Ile nyumba
ilikuwa imechakaa karibu kuanguka
na palionyesha ukiwa wa wazi.
Nilibisha hodi na mama mmoja mtu
mzima sana alifumgua mlango
kutokea ndania na kusimama
mlangoni.

Kwa muda sikuweza kumjua. Lakini
htimaye nilijua kuwa ni dada
yangu.
‘Dada shikamoo, habari za siku’
nilimsalimia, lakini yule mama pale
mlangoni alishindwa kujibu na kwa
muda fulani ilionekana kama vile
hakuwa anajua kinachoendelea.

‘Marahaba’ Alijibu, lakini ilikuwa ni
kwa mazoea tu. ‘Nani mwenzangu,
maana na huu uzee nao,’ Alisema
akijichekesha.

‘Ni mimi Joseph, mdogo wako
Joseph, mtoto wa mzee Richard
Mbega wa Sindeni.’ Nilisema kwa
kumfafanulia. Nilimwona dada
akijishika vizuri pale mlangoni,
lakini hakuweza.

Alienda chini pole
pole na kukaa kati kati ya mlango.
Kw muda fulani nilijua alikuwa
hajui alipo na kinachoendelea.
Wakati nikiwa najiuliza nifanye
nini mama mwingine aliingia
kutokea huko nyuma ya nyumba.
Nilimtazama lakini sikumfahamu.
Yeye alipiga kelele.

‘Kaka Jose
jamani, kaka Jose,wala siamini…….’
Ilikuwa zamu yangu kushngaana
laijua hilo kwani aliniambia, ‘Ni
mimi mpwa wako Msekwa.’ Nilihisi
kitu kikilipuka huko moyoni na
matumbo yangu yalishikw na
kubana ghafla.

Msekwa, alikuwa ni mama mzima,
amechakaa na kuchoka kabisa. Kati
yetu, yeye angeonekana kuwa
mkubwa sana kuliko mimi. ‘Mungu
wangu nashukuru nimekukuta…’
Halafu tulimsikia dada yangu
akipiga yowe la kilio akidai
kwamba hakuwa anajua alichokuwa
anakifanya.

Akiwa anaongea
Kizigua alisema, ‘Mungu wangu mie
nifanyeje sasa, naumbuka ….’


Nilimbembeleza, ingawa Msekw
alisema nimwache augulie kwa
sababu anastahili.
Baada ya kupumzika, nilijua
kwamba wale wapwa zangu watatu
wengine, aliyekuwa hai ni mmoja tu
wa kike.

Mmoja alifariki kwa
kuajribu kutoa ujauzito na yule wa
kiume alikuwa amefariki kwa
kunywa sana pombe.

Huyu
mwingine alikuwa ameolewa na
kuachwa na alikuwa eneo
linaloitwa Dakawa.

Nilikaa Turiani
siku tatu na nilimwomba Msekwa
tuondoke wote aje Dar ajifunze kozi
yoyote. Hapa ninaposimulia makala
haya, ni muuguzi siku nyingi. Dada
yangu alikataa katakata kuja
kwangu kwa aibu.

Inasikitisha hata hivyo kwamba,
miezi mitatu tu tangu nilipofika
kwake alifariki.

Wanasema kila
wakati alikuwa akijilaumu kwa yale
aliyokuw amenitendeana alianza
kujiambia kwamba, hana sababu ya
kuishi kwa sababu hana maana.


Naamini tunapanda nguvu hasi na
huja kuturudia wenyewe.
Tulienda kuzika na kurejea Dar.
Juhudi yangu yote ilikuwa ni
kumpata yule shemeji yangu, iwe
yuko hai au kaburi lake lilipo ili
angalau nilijengee kama zawadi
yangu kwake.

Lakini juhudi zangu
ziligonga ukuta kwa kadiri
nilivyojitahidi. Nilikwenda hadi
TPC, Moshi lakini sikumpata.
Hata hivyo hatimaye nilimpata
katika mazingira ambayo sitaweza
kuyasimulia hapa.

Naamini kwa simulizi hii, kuna
jambo ambalo umejifunza. Katika
maisha haya tunayoishi ni vyema
tukawa tunapanda mbegu chanya
na sio hasi, kwani kwa kupanda
kwetu mbegu hasi, ndio hatimaye
huturudia mara tatu zaidi ya kile
tulichopanda na maumivu yake
kihisia huwa ni makubwa sana.

Lakini kama tukipanda mbegu
chanya, hakika mavuno yake huwa
makubwa kuliko kawaida, hebu
jaribu uone


Jambo lingine ni kusamehe,
kusamehe ni muhimu kwetu, hata
kama utakuwa umefanyiwa jambo
baya kiasi gani. Kwa kusamehe
kwetu tunakuwa tumejipa nafuu
dhidi ya maumivu ya kihisia pale
tukumbukapo juu ya yale
tuliyotendewa na wenzetu.


Zipo
faida nyingi sana tunazopata pale
tunaposamehe, lakini kubwa zaidi
ni kule kumudu kusahau yale
tuliyotendewa na hivyo kuwaza
mambo mazuri ya yenye tija katika
maisha yetu, badala ya kufikiria
mabaya au kulipiza kisasi dhidi
wale waliotutendea kinyume na
matarajio yetu.


*******MWISHO********


Ndugu wasomaji, habari hii hainihusu mimi
binafsi, bali iliwahi kuandikwa katika gazeti la
jitambue.

Hii ni habari ya kweli kabisa
ambayo ilimpata msomaji wa gazeti la
Jitambue, ambapo kwa hiyari yake aliamua
kuiweka habari ya maisha yake katika gazeti
hilo ili wasomaji wapate kujifunza kupitia
uzoefu wake.

Ukweli ni kwamba, katika gazeti
la Jitambue tulikuwa tukiandika ushuhuda
mbalimbali kutoka kwa wasomaji wetu ambao
walijitolea kuandika historia za maisha yao.

Na mimi nimeona sio vibaya nikizirejea
baadhi ya stori hizo ili wasomaji wa Jukwa hili
nao waweze kujifunza
Nawakumbuka akina Munga Tehenam, Conrad, Sam Makilla, NIck Maila-RIP (alikuwa mwandishi mzuri sana wa makala za Kiswahili kwa Gazeti la Majira.) Nick alini-encourage sana nami kujifunza kuandika story na Makala mbalimbali. RIP wote waliotangulia.
 
Nawakumbuka akina Munga Tehenam, Conrad, Sam Makilla, NIck Maila-RIP (alikuwa mwandishi mzuri sana wa makala za Kiswahili kwa Gazeti la Majira.) Nick alini-encourage sana nami kujifunza kuandika story na Makala mbalimbali. RIP wote waliotangulia.
Wapumzike kwa Aman
 
Pole sana ndg, hapa ndipo ninapoamini wapo waliopitia magumu kuliko tunayoyapitia sisi.
 
Pole sana kiongozi. Umenikumbusha mbali sana. Mimi nikiwa na miezi sita niliacha rasmi kunyonya na hii ni baada ya mama yangu kunichukua na kuniweka pembeni ya barabara kwenye majani marefu akaondoka kurudi kwa wazazi wake maana alichoshwa na vipigo vya baba yangu. Bibi mmoja jiran yetu ndie wakati anakuja kufunga mbuzi wake ndiye aliniona na kuniokota na kunirudisha nyumbani. Hapo mama yangu ameondoka na alikuwa na mimba nyingine. Na haya yote nilielezwa na bibi yangu nilivyomaliza darasa la sana ambae ndiye alinichukua na kunilea. Ni story ndefu lkn basi tu. R.I.P Mama
Dah... Familia nyingi zinapita kwenye misuko suko ya hatari... Poleni wote ambao wazazi wenu walipitia hayo... Binafsi mama yangu alishawahi kupigwa mpk mimba ikaharibika.. Mama aligeuka NGOMA ya baba... Ila nashukuru yeye aliamua kurudi kwao kabla hatari haijamkuta... Ndoa zinamambho
 
Dah... Familia nyingi zinapita kwenye misuko suko ya hatari... Poleni wote ambao wazazi wenu walipitia hayo... Binafsi mama yangu alishawahi kupigwa mpk mimba ikaharibika.. Mama aligeuka NGOMA ya baba... Ila nashukuru yeye aliamua kurudi kwao kabla hatari haijamkuta... Ndoa zinamambho
Asante sana ....pole sana na wewe
 
Mimi sipigi mke wala mtoto hata iweje aisee, namkalisha chini na kumweleza makosa yake na kureason nae. Mke asipochange, ni bora nikamate mchepuko au nibwagane nae.
 
Back
Top Bottom