Njia ya maisha yangu ilipofungwa ghafla

Ambiele Kiviele

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Messages
14,482
Likes
26,136
Points
280
Ambiele Kiviele

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2014
14,482 26,136 280
Ni kidonda kikubwa cha hisia, lakini nimemudu kukiponyesha na sasa limebaki kovu tu ambalo halina mauamivu kwangu.

Kidonda hiki cha kihisia kilitokana na mkwaruzo ulioanzia kwenya familia yetu, yaani kwa wazazi wangu. Ndoa ya wazazi wangu haikuwa ndoa imara na wala mtu asingepaswa kuiita ndoa.

Nilizaliwa mwaka 1965 katiaka kijiji cha Segera, mkoani Tanga, kabla ya wazazi wetu hawajahamia Sindeni wilayani Handeni wakati huo, ambako ndiko nyumbani kwa baba yetu.

Mama yetu alikuwa anatokea maeneo ya Mombo mkoani Tanga. Tulizaliwa wawili tu kwa baba na mama, mimi na mdogo wangu wa kike.

Nakumbuka Tangu nikiwa mdogo sana, nilishuhudia mama yangu akiwa anadhalilishwa. Alikuwa anapigwa sana, wakati mwingine alikuwa anavuliwa nguo mbele yetu au hata kutoka nje akikimbia uchi.

Nakumbuka hata nilipokuwa naanza darasa la kwanza kuna siku nilichelewa darasani na mwalimu aliyekuwepo aliniuliza kama nilikuwa naamua ugomvi wa baba nyumbani ndio maan nikachelewa.

Darasa zuima lilicheka na jambo hili sikulisahau kirahaisi. Ni ajabu kwamba hata zamani kulikuwa na waalimu wahuni.

Tukiwa wawili, mimi na mdogo wangu nyumbani, tulikuwa kama wakiwa kabisa. Mama yetu kwa kweli alikuwa mama ambaye ni adimu kumpata kwa ukarimu na uadilifu wake. Sisemi hivyo kwa sababu ni mama yangu , hapana.

Hata jirani na waliomfahamu walijua jambo hilo na kulisema. Nakumbuka kila wakati alipenda sana kutupa moyo kwamba, maisha ni juhudi, uvumilivu na hekima.

Nikiwa darasa la nne mwaka 1975 na mdogo wangu akiwa anaanza la kwanza ndipo jambo baya kabisa lililotugusa na pengine kunifanya hivi nilivyo leo lilipotokea. Ilikuwa ni jumamosi nakumbuka nikiwa nimetokea shambani kuhamia ndege wasiharibu mpunga.

Niliporudi nyumbani hapakuwa na dalili ya kuwepo mtu. Giza lilikuwa limeingia, lakini nyumbani kulikuwa hakujawashwa taa.

Niliingia ndani na kumwita mdogo wangu aliyekuwa akiitwa Selina. Lakini hakukuwa na jibu, wakati nikitaka kutoka nje nilisikia kama sauti ya mtu huko chumbani kwa wazazi wangu.

Niliita 'mama' na nilihisi kama nimeitikiwa. Nilibisha hodi na kuingia chumbani kwa wazazi wangu. Kwa sababu kulikuwa na giza sikuweza kuona vyema madhari ya chumba. Nilitoka na kwenda nje kwenye kibanda kilichokuwa kinatumika kama jiko. Nilichukuwa kiberiti na kurudi chumbani. Niliwasha taa.

Mama yangu alikuwa amelala kitandani akiwa ametapakaa damu usoni. Hakuwa na uwezo wa kuongea kwa sauti ingawa alikuwa akiongea .

Nilimsogelea huku nikiwa nimeogopa sana. Alinyoosha mkono kama vile kuomba nimshike. Nilimshika mkono na alizungumza kwa shida sana. ‘Ni …ba…baba yako, laki….lakini msamehe tu. Mungu…..’ Halafu alinyamaza.

Wakati huo huo watu wawili waliingia ndani. Walikuwa ni wanawake rafiki zake mama. Pamoja nao alikuwepo Selina, ambaye kumbe alitumwa na mama kwenda kuwaita.

Wanawake wale walikwenda moja kwa moja pale kitandani na kumkagua mama hukuwakimsemesha. Lakini bila shaka waligundua kwamba mambo sio shwari. Mmoja alitoka haraka.

Nilitoka na kusimama sebuleni, wakati huo huo tulimwona baba akiwa na katibu kata pamoja na viongozi wengine wa kijiji, wakiingia.

Naye baba alikuwa na jeraha usoni lillokuwa likitoka damu bado. ‘Basi , wakamshambulia hapa, mimi kufika, ndio nikapigwa panga la uso nikadondoka….’

Alisema baba akiashiria kwamba, mama alikuwa ameshambuliwa na watu fulani. Viongozi wale waliingia chumbani kwa wazazi wetu moja kwa moja na huko tulimsikia yule mama aliyebaki mle chumbani akilia.

Ndivyo mama yetu alivyokufa na bila shaka ni mimi na mama na pia mungu ndio tuliojua kwamba, aliyemuuwa alikuwa ni baba na sio hao watu ambao baba aliwasingizia.

Tulianza sasa kuishi maisha magumu sana ambayo siyo rahisi mtu kuamini unaposimuliwa.

Tulikuwa tunakula kwa kubahatisha, shule tulisimama kwa sababu baba alikuwa kama vile anataka kuona tunakufa kama mama yetu……………

Nakumbuka kuna siku alinipiga sana kwa sababu tulichukua unga na kukoroga uji na kutumia sukari yake kidogo iliyokuwa mle nyumbani.

Alinipiga hadi nikapoteza fahamu. Wakati ananipiga alikuwa akiniambia kuwa ataniuwa kama mama. Ukweli ni kwamba ilifika mahali ambapo niliona ni vyema kufanya jambo moja tu, ama kufa au kutoroka.

Lakini nilipofikiria kufa, wazo la mdogo wangu lilinifanya kurudi nyuma. Niliamua kwamba, ingekuwa ni vizuri kwetu kutoroka. Mdogo wangu alikuwa mwerevu na mwenye upendo mkubwa na alinikumbusha mama yetu kila wakati.

Kama baba angekuwa anawaruhusu jirani au wale rafiki mama kutusaidia, huenda tungeishi kwa shida, lakini tungesoma.

Lakini baba alikuwa mbogo kwa mtu yeyote ambaye alikuwa anajaribu kutupa msaada. Tulipanga na mdogo wangu tuondoke pale nyumbani na kwenda kwa dada yetu, mtoto wa mama yetu mkubwa aliyekuwa akiishi Mtibwa ambapo nauli yake ilikuwa ni kama shilingi tano.

Lakini usiku wa kuamkia siku ambayo ilikuwa tuondoke, Selina alianza kujisikia vibaya. Usiku alikuwa amepandwa sana na joto na alikuwa anatetemeka.

Alikuwa na malaria bila shaka. Hali hii ilimuanza kama wiki wiki mbili nyuma, lakini ilikuwa ikiisha baada ya kunywa vidonge vya aspro.

Ilikuwa kama saa sita usiku na baba alikuwa hajarudi. Niliamua kwenda kuwajulisha majirani ili waje watupe msaada. Wakati natoka nilikutana na baba mlangoni.

Aliniuliza nilipokuwa naenda na nilimweleza.
'Kwani umeambiwa mimi sijui kulea, yaani mwanangu akasaidiwe kama manamba, rudi ndani.' Aliniambia na kunipiga kibao.

Nilirudi ndani nikiwa ninalia kwa uchungu na mambo mengi. Baba aliupiga mlango komeo na kuutia kufuli kwa ndani. 'Toka nione, unajifanya kidume sana.'

Hakuja kumwangalia Selina na mimi nilikaa kwenye kitanda cha mdogo wangu hadi asubuhi. Kulipokucha na baba alipoondoka nilikimbia kwa majirani kuwambia kwamba, mdogo wangu alikuwa amezidiwa.

Ukweli ni kwamba wakati huo mdogo wangu alikuwa amezidiwa kupita kiasi.

Jirani walifika kwa woga na kuamua kwenda kwanza kwa katibu kata kutoa taarifa ili baba asiwafanyie vurugu.

Waliporudi tulimchukuwa mdogo wangu hadi kituo cha afya, Alifanyiwa vipimo na kuonekana ana malaria na tatizo la tumbo.

Aliandikiwa dawa.
Inasikitisha sana kusema kwamba Selina alifariki usiku wa siku ile.

Najua hivyo ndivyo ilivyo, kwamba sitakuja kulia kama nilivyolia siku ile. Maishani mwangu naamini sitakuja kum-miss mtu kama nilivyom-miss mdogo wangu mpendwa.

Hata mke wangu siku hizi huwa ninamwambia na anakubali kwamba hata angekuwa yeye ingekuwa hivyo hivyo.

Kifo cha mdogo wangu kimenisumbua kwa miaka mingi hadi mwaka 2001nilipoanza kusoma gazeti la Jitambue, ndipo nilipojifunza kusahau na kujua kwamba kila jambo linakuja kwa sababu maalum na kwa kawaida ni vizuri tu, kama tutapenda iwe hivyo.

Tulimzika mdogo wangu na hakukuwa na matanga. Hakuna jirani ambaye alikuwa tayari kufanya matanga ya kifo cha aina ile.

Usiku wa siku ile ndipo nilipoondoka pale kijijini na nasikitika kusema kwamba, sikurudi tena kijijini hapo hadi nilipokuwa mtu mzima, ambapo nilikwenda kutengeneza kaburi la mama na la mdogo wangu Selina.

Nilifika Mtibwa na kuulizia kiwandani ambapo nilielekezwa. Niliulizia hadi nikafika kwa dada yangu.

Huwezi kuamini kwamba, swali la kwanza aliloniuliza huyo dada yangu ni kama nilikuwa nimekwenda pale kuishi au kusalimu tu.

Nilipomsimulia kisa chote, Alinimbai kuwa pale kwake siyo nyumba ya kutunza watoto yatima.

Alimsimulia mume wake kwamba mama yangu alikuwa mtu mbaya sana. Alieleza kwamba, mimi na marehemu mdogo wangu tulikuwa tumelelewa kwa kudekezwa na hatukuwa watoto wanaoweza kishi na mtu.

Inashangaza kwa sababu, huyu dada yangu mwenyewe nilikuwa najuana naye siku ile, nilikuwa simjui bali kumsikia tu kutoka kwa marehemu mama.

Mumewe alisikiliza maneno yake bila kusema neno. Baadae, huyo shemeji yangu aliniambia tunyooshe miguuili nikakijue kiwanda cha sukari.

Tukiwa njiani alinimbia kwamba haamini kuwa dada yangu , yaani mkewe anasema kweli. Aliniambia kwamba, anachojua ni kwamba atanisaidia hadi nisome na kumaliza masomo yangu.

Ndugu msomaji maelezo ya habari hii yanayofuata ni yenye kuumiza kidogo, kwa sababu, yanaonyesha nyuso nyingi za binadamu na nyuso nyingi za uadilifu na uovu wake.

Nimeona upate pumziko na kutafakari haya ambayo nimekusimulia kwanza, nisije nikakujaza nguvu hasi nyingi zaidi bila sababu.

Usiniambie Nimalizie Hii Stori
 
Patience123

Patience123

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2013
Messages
4,968
Likes
8,183
Points
280
Patience123

Patience123

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2013
4,968 8,183 280
Mhhhh...

Hii story imenijeruhi hisia zangu halafu inanitia hasira...

Namshukuru Mungu aliyeumba kitu "kusahau"

Kuna kina mama wamepitia mahusiano magumu sana, lakini walitabasamu nyuma ya machungu yao ili kuwapa watoto moyo kuwa they are okay..
 
afande kifimbo

afande kifimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2015
Messages
5,827
Likes
2,093
Points
280
Age
48
afande kifimbo

afande kifimbo

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2015
5,827 2,093 280

IMENIGUSA SANA HII NIMEUMIA....UKATILII HUO HYO MZEE KAUOTOA WAPI.....DAH....KWELI WATU WAPETIA SHIDA NA STRESS SIE WNEGINE HAKUNA KITU....BRO MALIZIA JITAHIIDI TUU
 
D

Dirishalangu

Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
33
Likes
12
Points
15
Age
31
D

Dirishalangu

Member
Joined Nov 17, 2016
33 12 15
Pole sana story yako inasikitisha...Jana tu nilikuwa naongea na rafiki yng juu ya kupigwa kwa wanawake mwsho wake huwa wengi wanafariki na nilihisi na mama ako ingekuwa HVO kumbe ni kweli...kuna mambo mwsho wake huwa mbaya la kwanza ni hilo la kupigana. MUNGU azidi kukutia nguvu ni ngumu kusahau ila yakupasa usamehe na usahau
 
House of Commons

House of Commons

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2013
Messages
1,694
Likes
433
Points
180
House of Commons

House of Commons

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2013
1,694 433 180
Kumbe binadam wengi wanashare tabia, hii kitu imenigusa sana. Mama yangu walipigana na baba mwaka 1992 nikiwa form 2, mama katolewa jino moja hiyo siku.

Siku nyingine wakapigana tena, nikasikia kilio kikubwa cha mama, sikuvumilia nilijitosa ndani, nilivowakuta najua mimi...niwaachanisha, ila kuanzia hapo mama akatoka hadi imepita miaka 10 hawako pamoja.

Baba yangu akaanza kunishawishi nimshawishi mama arudi, imenichukua muda mwingine wa miaka 5 nikimshawishi mama waishi pamoja na mama. Hata hivo alikubali kwa masharti magumu sana, ambayo mzee yamemshinda hadi leo, mojawapo ambalo wao walielezana kwa faragha ni " hakuna ushiriki wa ibada ya mwili"...kitu ambacho kati yao hakuna ambaye amesema wazi ila nilielezwa na dada yangu...hayo ni yao mi siingilii

cc Ambiele Kiviele
 
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Messages
11,746
Likes
9,544
Points
280
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2014
11,746 9,544 280
Pole Mkuu,lete hiyo ya pili tupate somo ili tujue kuwa maisha husonga mbele pamoja na magumu tunayopata
 
M

Magimbi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Messages
1,214
Likes
675
Points
280
M

Magimbi

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2011
1,214 675 280
Tunashukuru kwa story nzuri japo ya marudio lakini inatukumbusha mbali sana katika maisha ya ndoa
 
Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044