Njia ya kumtongoza mwanamke akakupenda daima

ulanga2

Member
Nov 21, 2015
23
3
Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.

Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo;

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida
atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye.Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho
baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote. Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua ni vitu ganihasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake, kisha rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana.
 
Last edited by a moderator:
Duh...maandalizi na mbinu kama vile unasubiria interview ya kuomba kazi.

Endeleeni na hiyo mihangaiko mie ntawapata tu kwa mpunga nitakao vuna toka job.
 
Mwanamke mwenye tabia namba 7 naomba ajitokeze tafadhari..Kuna zawadi yake
 
Yani hizi swaga kama hizo mwisho ulikuwa mwaka 2000 asaivi kama huna hela imekula kwako

Kwamfano kuna dada namtongoza mm
Esms zangu hanijibu wala sm zangu hapokei juzi nikamuambia

Nakutakia maisha mema samahani kwa usumbufu

Alicho nijibu
Kabwe mm nina steres nina shida ya milioni 5

Nkamuambia duh toka nzaliwe mwenyewe sijawahi kuishika hiyo hela mm
 
Zote Bla Bla Hizo,Tafuta Mkwanja wa kutosha ,kuwa karibu na wabongo flavor,movie nunua kiwanja mbezi beach jenga ghorofa,nunua range rover sport HSE ,account yako isiwe inapungua 100m utapiga mpaka utawakimbia muulize Rumishael Rummy.
 
Aiseee.....! Theory na praktica ni vitu viwili tofauti.
Hizo labda zinakuwa applied kwa wanawake ambao bado hawajaijua jf.


Alafu kuoendwa daima na mwanamke haitokani na js unavyo mtongoza, jinsi umtongozavyo inakusaidia kukupa jibu la ndio au hapana na kama ni ndio basi the way ulivyomtokea inamsaidia akutreat vp.

Kukupenda daima kama unavyosema ni swala lingine kabisaa. Hapo ni baada ya mahusiano kuanza.

Mpe muda wako, mjali, good sex, na mengineyo....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom