Njia sahihi ya kupima KISUKARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia sahihi ya kupima KISUKARI

Discussion in 'JF Doctor' started by Oleni, Sep 13, 2012.

 1. O

  Oleni Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa yeyote anayejua naomba anifahamishe ni njia gani sahihi ya kupima kisukari.
  -Kupima pale unapopatwa na dalili au kabla ya dalili? Na ukipima kabla ya dalili unaweza kuonekana?
  -Njia nzuri ni ipi kupima damu au mkojo? Je njia ya kupima damu ni ile ya kutoboa kidole nakuweka damu kwenye kimashine au kuna nyingine. Msaada tafadhali.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kisukari ni muhimu kuwapimwa mara kadhaa, hasa kama una historia ya kisukari kwa familia na/ama una uzito mkubwa.
  Kwa ajili ya monitoring, fasting blood sugar ndio kipimo kizuri. Hii hufanywa asubuhi kabla ya kula chochote. Njia inayotumika haswa ni ya kutumia tone la damu kutoka kidoleni.

  Njia ya kupima mkojo ilikuwa inafanyika zamani. Nadhani imepitwa na wakati, japo haiko conclusive lakini inafaa kuashiria uwepo wa tatizo (watabibu watahusika hapa)
   
 3. O

  Oleni Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuona dalili au hata kabla.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,450
  Likes Received: 5,837
  Trophy Points: 280
  Fika hospitali utapatamuongozo mzuri........mimi ni DIABETIC
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri kupima kabla ya dalili, kwani upimaji hauhitaji gharama sana, na mara baada ya dalili usikate tamaa na kuona umechelewa hivyo kuacha.

  Njia za Upimaji:

  - Damu: Kuna njia mbili za haraka, kupima katika damu
  yaani kupima damu kabla ya kula kitu chochote( Fasting
  Blood Glucose) na ile nyingine ya muda wowote, ,mostly
  masaa mawili baada ya kula(Random Blood Glucose),

  - Upimaji wa njia hiyo hapo juu ni STANDARD, lakini vipimo
  zaidi vya damu Haemoglobin A1c, Haja ndogo (Urine),


  KUMBUKA: Kipimo hufanyika zaidi ya mara moja, kwani inapofanyika mara ya kwanza hukupa kiashiria(clue) inawezekana kuna shida fulani.

  GLUCOMETER, Glucostix, Syringe, Mathylated Spirit ni baadhi ya vifaa vitumikavyo katika kupima.. wakati mwingine unaweza usipate majibu sahihi (False negative, False positive) kutokana na sababu nyingi mfano contamination of blood. n.k
   
 6. O

  Oleni Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri wenu maana mdogo wangu ana dalili hizo kama kubanwa mkojo mara kwa mara, kuwa na numbness mwilini lakin amepimwa hii mara ya tatu anaambiwa ana 4.8, 4.6 na 4.9 halafu wanasema hyo haina matatizo. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba ukoo hauna historia ya kisukari, yeye si mnene na ana umri 18 ila haishi kulalamika ganz, kukojoa, kuchoka, mapigo ya moyo kwenda mbio. Aisee naomba kama kuna maradhi mengine yanaweza sababisha hiz dalili mnijuze maana nachanganyikiwa
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Oleni, ni ngumu sana kuweka dalili(Symptoms) za mgonjwa na kupata kwa uhalisia tatizo ni nini (exact Diagnosis).. kwani kila dalili inaweza kusababishwa na magonjwa mengi... na dalili ukizosema (<18yrs, Absence of familial history of DM doesnt rule out DM) kwani kuna kitu kinaitwa Type I DM/ Juvenile Diabetes Mellitus.

  Ningekushauri, fika katika HOSPITALI yeyote ya karibu ili kujua shida ni nini kama vile Kujua tatizo ni nini, (nini kilichoanza), kwa muda gani, kilikuwa kinaendeleaje, kinapata unafuu kwa kufanyaje, nk...lakini pia vipimo mbali mbali vitaweza kusaidia kujua shida ni nini.
   
 8. O

  Oleni Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru mkuu kwa ushauri wako.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ni muhimu kupima kila wakati kama una risk factors nilizotaja hapo juu:
  Uzito mkubwa (obesity)
  Historia ya kisukari (type 2) kwenye familia
  Kama mwanamke alipata kisukari wakati wa ujauzito (gestational diabetes)
  Kama una dalili

  Kwa huyu mdogo wako, kama huna hakika na maamuzi ya daktari, basi tafuta daktari mwingine umuone na vipimo vyote awape ushauri wa ziada.
  Wakati mwingine ni wasiwasi tu.
   
 10. K

  Kasigi Senior Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vitamin b12 deficiency pia ina hizo dalili kasoro hyo kwenda haja mara kwamara
   
 11. O

  Oleni Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante ntatafuta daktari mwngne. Hivi hii diabetes type 1 kama syo ya kurith, sasa inasababshwa na nin haswa mpaka pancreas kushndwa kutoa insulin, je ni vyakula ama?
   
Loading...