Njia sahihi ya kufanya bei ya mafuta isipande kwa mtumiaji wa mwisho (consumer) ni kupunguza kodi au kuweka Ruzuku?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,958
141,951
Nauliza kwa wataalamu wa mambo ya utawala wa fedha na uchumi kwamba njia sahihi ya kumaintain bei ya mafuta kwa consumer iwe ile ile hata ikipanda huko duniani ni ipi?

Kuweka ruzuku kwenye mafuta?

Au kupunguza kodi kwenye mafuta?

Maendeleo hayana vyama!
 
... shida hiyo ruzuku itatoka wapi wakati mafuta ndio chanzo kikuu?
 
kweli Nchi yetu imeshindwa kuzalisha mafuta ya alizeti, karanga na ufuta?!!

Hawa wasomi wetu Maprofesaa na mainjinia wafani mbalimbali elimu yao inamanufaa gani kwa Taifa?!
au ndio wote wanasubiria tu kuajiriwa na kula mshahara?!
 
Inashindwa kwa sababu ina watu wengi wa aina yako
kweli Nchi yetu imeshindwa kuzalisha mafuta ya alizeti, karanga na ufuta?!!

Hawa wasomi wetu Maprofesaa na mainjinia wafani mbalimbali elimu yao inamanufaa gani kwa Taifa?!
au ndio wote wanasubiria tu kuajiriwa na kula mshahara?!
 
Inategemea ruzuku inatoka wapi, lakini kushusha bei ya mafuta kwa kupunguza tozo au kuweka ruzuku ni karibu kitu kile kile. Ila sasa, kuondoa tozo unaathiri taasisi nyingi kwa kuwa sio tozo zote zinaenda moja kwa moja kwenye mfuko wa serikali kuu. Kwa mfano, ukiondoa toza ya ukarabati wa barabara unakuwa umeathiri utendaji wa TANROADS. Kwa hiyo ni bora kuacha zote ili kutozibana taasisi zinazonufaika na tozo hizo

Na kuondoa tozo itabidi serikali ifidie taasisi zote zinazonufaika na tozo hizo, ambapo administratvely inakuwa very complicated kwa serikali kuwa inagawa fedha kwa kila taasisi inayopokea tozo ya mafuta. Hivyo ruzuku ni njia rahisi zaidi kuliko kuondoa tozo yaani levies, ambayo wewe hapa umeiita kodi.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Sidhani kama upo sahihi,kuna baadhi ya nchi za hapahapa Afrika hazijapandisha bei ya mafuta unataka kuniambia "Tanroad" zao haziathiriki kiutendaji kwa kukosa levy? Hapa tuwe wawazi wale wanaotoa maamuzi ya kupanga bei za mafuta wana ubia na makampuni yanayoingiza mafuta hapa nchini, hiyo ni moja ya hasara zinazopatikana baada ya nchi kulikataa Azimio la Arusha, moja ya kipengele katika hilo Azimio kinazuia viongozi wa nchi kufanya biashara, kwa sasa Hali imekuwa siyo hali, viongozi wanamiliki biashara ni jambo jema lakini lina downside zake, moja wapo ni pale wanapotakiwa kutoa maamuzi nyeti yenye kuleta unafuu kwa wananchi, wanashikwa na kigugumizi inawalazimu watoe maamuzi yanayopendelea maslahi yao binafsi.

Hivi umewahi jiuliza kwanini Tanzania inategemea mafuta ya kupikia toka nje ya nchi wakati ambapo tuna ardhi ya kutosha kulima mazao yenye kutoa mbegu za kukamua mafuta?
 
Back
Top Bottom