Njia panda, nani ananifaa kati ya hawa?

Njia panda, nani ananifaa kati ya hawa?

Wakati mwingine upendo uliozidi na kumfanya mtu apende kama kipofu huweza kumfanya mtu akafanya uchaguzi usio sahihi katika kuchagua mwenzi wa maisha.

Muasisi wa ndoa nu Mungu na yeye mwenyewe asema mke au mwema atoka kwake, naye ajipatiae mke au mume mwema ajipatia kitu chema. Maadamu wewe umekuja hapa kwa lengo la kupata ushauri wa kukuwezesha kuchagua mume mwema, mimi nakushauri usali na uombe Mungu akuangazie na akuonyeshe mume aliyekuandalia ni yupi. Yeye pekee ndiye anayeweza kukupa jibu sahihi na kukueleza ni nani anayekufaa katika maisha yako na ndio maana hata yeye anasema "Mimi ndio njia ya ukweli na uzima."

Pia wakati unamuomba Mungu akuangazie nakushauri pia utafakari na ujiulize kwanza kama huyo mwanaume unayetaka kuolewa naye anafaa ama vipi. Mwenedo wake na tabia yake ya siku za nyuma ulikuwa wa namna gani? Je maisha yake ni masafi? Je upendo akuonyeshao unatoka moyoni na unaonyesha heshima na tabia njema ama ni upendo wa hivi hivi tu? Je anao mwendendo ambao utakufanya kuwa na furaha? Wewe kama mke utaweza kuwa na furaha uwapo kwake? Je ataruhusu kudumisha tabia yangu na kunipa uhuru ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kufuata matakwa yake? Maswali kama haya yakizingatiwa kwa busara yatakuwa na manufaa sana katika maisha yako yajayo kwako wewe ambaye unataka kuolewa

Kama kuwa na familia yenye furaha na amani, ambayo haitakuwa na udhaifu wala huzuni katika siku za baadae basi naomba ujiulize maswali haya kabla ya kuamua kukubali kuolewa na huyo mwanaume:

  • Je huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
  • Je ana afya njema?
  • Je ana bidii katika kazi?
  • Je msafi wa kimwili na kiroho?
  • Je ni mlevi?
  • Je ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
  • Je anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
  • Je ni mwaminifu?
  • Je ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
  • Je ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
  • Je mpenzi wangu anaye mama?
  • Je tabia ya mama yake ikoje?
  • Je anatambua wajibu wake kwa mamaye?
  • Je anajali upendo na furaha ya mama yake?
  • Ikiwa hajali wala hamheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe?
  • Je harusi itakapokwisha atakuwa na huruma kwa makosa yangu ama atakuwa ananikosoa mara kwa mara huku akiwa mgomvi na mkali?

Katika kuyajibu maswali haya shauku nyingi yaweza kupishia mbali makosa na kasoro za mchumba wako, lakini upendo wa kweli hautaficha neno. Katika kuchagua mwenzi wa maisha, unatakiwa uchague mwanaume mwenye tabia na mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, mwangalifu, mwenye heshima na aliye mwaminifu na mnyofu.

Ikiwa umefanya uchumba na mtu ambaye huelewi vyema tabia yake, usidhani kushika uchumba kutakulazimisha kuchukua kiapo cha ndoa na kuungana na mtu ambaye humpendi na ambaye wala hutamheshimu maishani mwako. Jihadhari sana unapofanya uchumba wenye masharti; lakini hata ukiwa ni uchumba wenye masharti, ni bora mara kumi kuuvunjilia mbali huo uchumba kabla ya kufunga ndoa kuliko kuja kuvunja ndoa baadae kama wengi wafanyavyo.
kati ya Vipengele Na uliyoyaongea Wapo Sawa Wote, Ila kwa uyu wa pili shdah ni ndoa alonayo, Na wa kwanza Mambo mengi
 
Sorry Nimeingilia....Ila mbona ninyi Hamtaki kujitoa kwa wenzenu , Au wao si watoto wa wanaume wenzenu???
Fanya kukumbuka sasa. Mpende mtoto wa mwanamke mwenzio..... mhudumie na umjali. Usimuache na ya kimwili.
 
Sorry Nimeingilia....Ila mbona ninyi Hamtaki kujitoa kwa wenzenu , Au wao si watoto wa wanaume wenzenu???
Uko tayari nijitoe kwako? Piga chini kwanza hayo mamjamaa yako afu njoo kwangu nikupe tulizo la moyo kama mchepuko wangu rasmi.
 
Hakuna anayekufaa hata mmoja kati ya hao
 
Hata mimi simfai? Unanipeperushia ndege wangu mchana kweupe namna hii? Akinipiga chini nahamia kwako!
Hahahaa wewe utakua mchepuko wakati akiendelea kusubiri njia kuu yake
 
Ka vile una pepo la ngono …………mishedede yote hiyo?
 
kati ya Vipengele Na uliyoyaongea Wapo Sawa Wote, Ila kwa uyu wa pili shdah ni ndoa alonayo, Na wa kwanza Mambo mengi

Basi kama wana hayo mapungufu maana yake ni kwamba hawakufai.
 
Nilikaa kama miezi 8 bila kujihusisha Na Mapenz , Na nilivyorudi Akikubadrika kitu

haukukaa hyo miezi nane kujifunza..ulikaa kutegemea atarudi..na huyo aliyeoa sijui alijua udhaifu wako...u are still desperate ...wakate wote...hakuna akufaaye...ila kama wataka wa kutuliza hamu waweza endelea nao no love hapo wanakufanya option tuu.
 
wote wawili hawakufai na hakuna anayekupenda hapo
 
Achana nao wote njoo kwangu tupeane faraja la moyo nipo serious ni pm
Au nicheki kwa namba hii 0777610047
Mkuu usipende kuzagaza namba kiasi hiki! Inaonesha uko desperate sana aise....
 
Aminas naona leo umeamua kuanzisha threads nyingi mno hadi zinanichanganya. Kuna ile moja umeshauriwa utulie na upumzike away from mahusiano. Tulia mama...
 
Back
Top Bottom