Njia panda na wachumba zangu wa muda mrefu

Njia panda na wachumba zangu wa muda mrefu

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
793
Wakuu msaada wa kimawazo, kimsingi nilishawahi kuoa huko siku za nyumba ndoa ya kikatoliki, ila haikudumu kwa muda mrefu tukatengana kidini na kimahakama na ndoa ikaishia hapo ila tulibshatika kupata mtoto mmoja kwenye ndoa.

Katika harakati za kimaisha nikakutana na binti mmoja 2010 ambaye nimefanya nae maisha mpaka sasa niko nae tunaishi kama wanandoa ingawa sijafanya process zozote kumuhalisha na watu mpaka staff wenzangu ndo wanajua mkewangu na sijazaa naye mpaka sasa kutokana na changamoto zake za uzazi.

Kama vile haitoshi 2015 nikakutana na kabinti fulani kanaanza chuo, nilikachulia mzaha lakini baadae nikazama penzini mpaka alipomaliza chuo bado niko naye na sasa anatarajia kunipatia mtoto Mungu akijalia, wote wanafamiana ingawa hawataki kutambuana hasa huyu wa 2010, majuzi nilifanya kaprocess ka utambuzi kwa huyu wa 2015 ili tu kumuheshimisha kwa wazazi wake lakini pia ili kusiwe na zengwe pindi nitakapo muhitaji mtoto wangu akizaliwa.

Muhimu ni kwamba wote nawapenda sana na wao wananipenda sana na kujali familia yangu kwa maana mama na ndugu zangu na wote wananifahamu sana, sasa nataka nifanye maamuzi ya kuhalalisha ndoa Bomani Je ni nani anastahili kuhalalishwa kati ya hao wawili ndugu zangu, kwa sababu siwezi kuoa wote .

Nitashukuru kwa michango yenu ya kimawazo iliotukuka.
 
If you love two people at the same time
Choose the second one
because if you really loved the first
you wouldn't have fallen for the second

JOHNNY DEPP
Mada imefungwa, na huu ndio ukweli. kzba
---
My take.
Huyu wa 2010 utakuwa hujamtendea haki.
Swala hapo ishi nao wote, ikiwa kwa zaidi ya miaka 5 umeweze kuishi nao wote, Je nini kinakuzuia kuendelea kuishi nao sasa kama awali ulivyokuwa ukiishi nao.

Angalia hii video

Kaa nao wote unataka mmoja umuachie nan na kwa nn umuumize mtoto wa watu umemtumia kwa miaka mingap halafu leo hii umuache,pia kuna sehem nimeona umesema wanajuana sasa tatizo lipo wap hapo hakuna tatizo panga zamu ishi nao wote mana wameukubali uke wenza
 
Mada imefungwa, na huu ndio ukweli. kzba
---
My take.
Huyu wa 2010 utakuwa hujamtendea haki.
Swala hapo ishi nao wote, ikiwa kwa zaidi ya miaka 5 umeweze kuishi nao wote, Je nini kinakuzuia kuendelea kuishi nao sasa kama awali ulivyokuwa ukiishi nao.

Angalia hii video

Ni kweli mkuu ila kama umeelewa post yangu , mimi sina nia ya kumuacha yeyote bali natakiwa atleast nihalalishe mmoja ili kuweka kumbukumbu sawa kisheria kumbuka kuna leo na kesho mkuu sisi ni binaadam na tunamwisho wetu, tusije leta taaruki kwa familia.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Kaa nao wote unataka mmoja umuachie nan na kwa nn umuumize mtoto wa watu umemtumia kwa miaka mingap halafu leo hii umuache,pia kuna sehem nimeona umesema wanajua sasa tatizo lipo wap hapo hakuna tatizo panga zangu ishi nao wote
Asante minji nitazingatia hilo

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Asante minji nitazingatia hilo

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
kumbukumbu za nini unazoongelea kwamba ukifa waseme ameacha mke wa ndoa, kama umeweza kuishi nao wote kwa style hiyo endelea nao wote, hakikisha kila mtu ana vitu vyake haviingiliani na mwenzake kwisha. Kuhalalisha kwa mmoja kutaleta majonzi kwa mwingine
 
Mkuu
Umepatwa Na Nini Wewe Mwenyewe?
Yaani Unatengeneza Matatizo Tu Halafu Baadaye Utakuwa Mgeni Wa Nani!!! Ulioa Mkaachana
Ukatafuta Mwingine, Na Mwingine

Nakushauri Wazi Wazi Baadaye Utakuwa Ni Bwana Migogoro, Ulitakiwa Umuoe Huyo Dada Wa Pili
Kama Una Cash Kwenye Haya Maishi Usipate Kiburi Sana Kuamua Mambo Kwa Jeuri

Tembea Vijijini Unakuta Watu Wanaishi Kwenye Nyumba Amani Imetawala Ila Wapo Na Kipato Kidogo
 
kumbukumbu za nini unazoongelea kwamba ukifa waseme ameacha mke wa ndoa, kama umeweza kuishi nao wote kwa style hiyo endelea nao wote, hakikisha kila mtu ana vitu vyake haviingiliani na mwenzake kwisha. Kuhalalisha kwa mmoja kutaleta majonzi kwa mwingine
Nasapoti hii point
 
Mambo mengine ya ajabu yaani wewe ndiye unaowafahamu tabia zao na kila kitu halafu unakuja kwetu sisi ambao hata hatuwafahamu ndo tukuchagulie wa kumuoa ,,,kwa akili hizo hata kuishi na huyo mke utashindwa.
 
Wakuu msaada wa kimawazo, kimsingi nilishawahi kuoa huko siku za nyumba ndoa ya kikatoliki, ila haikudumu kwa muda mrefu tukatengana kidini na kimahakama na ndoa ikaishia hapo ila tulibshatika kupata mtoto mmoja kwenye ndoa, katika harakati za kimaisha nikakutana na binti mmoja 2010 ambae nimefanya nae maisha mpaka sasa niko nae tunaishi kama wanandoa ingawa sijafanya process zozote kumuhalisha na watu mpaka staff wenzangu ndo wanajua mkewangu na sijazaa nae mpaka sasa kutokana na changamoto zake za uzazi, kama vile haitoshi 2015 nikakutana na kabinti fulani kanaanza chuo, nilikachulia mzaha lakini baadae nikazama penzini mpaka alipomaliza chuo bado niko nae na sasa anatarajia kunipatia mtoto Mungu akijalia, wote wanafamiana ingawa hawataki kutambuana hasa huyu wa 2010, majuzi nilifanya kaprocess ka utambuzi kwa huyu wa 2015 ili tu kumuheshimisha kwa wazazi wake lakini pia ili kusiwe na zengwe pindi nitakapo muhitaji mtoto wangu akizaliwa.
Muhimu ni kwamba wote nawapenda sana na wao wananipenda sana na kujali familia yangu kwa maana mama na ndugu zangu na wote wananifahamu sana, sasa nataka nifanye maamuzi ya kuhalalisha ndoa Bomani Je ni nani anastahili kuhalalishwa kati ya hao wawili ndugu zangu, kwa sababu siwezi kuoa wote .

Nitashukuru kwa michango yenu ya kimawazo iliotukuka.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Mkuu najua jibu tayari unalo.

Ila mm nakushauri chukua huyo aliyekuzalia, maana definition ya ndoa ni watoto.

Hapo lazima ufanye maamuzi magumu ya kiume.
 
Back
Top Bottom