Watoto watabaki na bibi au shangazi yao fikiria kama wote hampo duniani watoto watabaki na nani?wewe ni mume wa mke na watoto 2. unaish nje ya nchi, mkeo yupo tanzania sasa mkeo kapata safari ya kikaz kwenda nje ya nchi je utakubali aende ama utakataa? nchi anayokwenda ni tofauti na uliyoko wewe.yeye anakwenda kikazi na wewe uko huko kikazi. wewe kazi yako ni contract ya muda mrefu yeye ni safari ya muda mfupi. nyumban watoto ni wadogo sana ambao kubaki peke yao pasi usimamizi wa mzazi ni ngumu utafanyeje?je wewe mama ama wewe baba mtafanyaje?je unafikiri hela mnazotafuta wewe baba na mama watoto wanazifaidi kwa stail hii ya maisha?
hapo kwenye red umenikumbusha nikiwa binti nilikuwa natamani sana kuna na mama mdogo ambaye sikuwa naye. sasa nilikuwa namsumbua sana mama, yaani hamna hata ndugu ambaye anaweza akawa mama mdogo wangu?yaani mpaka naleta uzi huu wamewaza sana juu ya nini kifanyike manake mke ukoo wake ni mdogo sana wajomba na mamma wadogo hana, mume ndo anandugu ila wako makwao. wadogo wa mke wote wako miji tofauti sana. bibi mzaa baba naye anauguza wazazi wakso hawez kuja huku na kipelekewa wajukuu ni kama kumtesa tu mama wa watu.
Ndio wanawajengea maisha yao, kwani mwanzoni mama alipokuwa anaenda kazini walikuwa wanabaki na nani? cha msingi kabla ya kuondoka kwenda nje kikazi mama anapaswa awaache watoto kwenye mikono salama
Watoto watabaki na bibi au shangazi yao fikiria kama wote hampo duniani watoto watabaki na nani?
safi sana.niyumwiki mlongo wangu
mimi kwa kweli tumewekeana kautaratibu na shem wako,mmoja lazima awepo home ,so hata maswala ya kujiendeleza kielimu kwa kweli yanafanyika kwa utaratibu huo.
Awaachie ndugu asake mihela ili watoto wanufaikekutokuwepo duniani ni tofauti!
Mwachie mdogo au wifi ya/wako wewe kasake mapene kwani unamaliza mwaka?dude how's you? were u successfull? BTW did you meet her expectations?
ishu ni pale unapozisaka wanao wanakosa furaha yao, baadae unakufa bado ni wadogo ndugu wana nyang'anya mpaka viatu na vilemba watoto wanabaki soro si soro kila siku wanafukuzwa na watu wanapokezana kama karata leo kakae kwa huyu kesho kwa huyu so sad aisee.Awaachie ndugu asake mihela ili watoto wanufaike
sisi pia tunajifunza mengi toka kwako mwl. usiache kutuweka sawa tunapopinda.......Duh! @fb umenigusa sana leo ila nimeshajua kosa lilipo si unajua mwl huwa akigundua kosa fasta anarekebisha? So najua wapi panakosa and patarekebika tu. I love jf bse pple like you and snowhite
Hahaha mi napenda mimama yenye miili mikubwa mikubwa yeye ni mwembambambona hujajibu swali? ulimeet expectation za amkatrina?
sisi pia tunajifunza mengi toka kwako mwl. usiache kutuweka sawa tunapopinda.......
kiukweli kila mtu anapenda sana kukaa na watoto wake, hasa sisi akina mama. lakini kuna kipindi inabidi kuna mambo pia yaende. hao hao watoto hata kama unawakumbatia sana lakini huwezi kuwapatia vitu wanavyotaka inakuwa shida. mimi huwa najiwekea kila ninapotoka nje ya watoto wangu lazima nikirudi watamani nisafiri tena ili nikirudi wafurahi. kuna siku mtoto wangu aliniuliza kwani mama utasafiri lini? nikamwuliza umenichoka, akasema hapana, nahitaji kitu fulani..... niliishia kucheka tu.
sasa baba akafanya kosa kasafiri akaagizwa kitu, si unajua wababa, ntanunua airport duty free shop, si walipofika hapo ikawa ni mchaka mchaka hakuna cha kupita shop wala nini. kufika home anaulizwa akasema nimeshindwa kununua, akaambiwa tunajua mummy akisafiri atatuletea maana anakoendaga kuna kila kitu, lol
Watoto watabaki na bibi au shangazi yao fikiria kama wote hampo duniani watoto watabaki na nani?
pole sana. utazoea tu ingawa ni ngumu sanahivi unajua watoto ndo kitu pekee ambacho kiukweli kinakupa furaha ya kweli dunian. ila sasa maisha yanabana sana jjiasi kwamba huwez kukaa nao muda wote pasi kuwatenga ili uwatafutie maisha.binafsi mara nyingi sana nimekuwa nasafiri na wanangu sijawah kuwaacha na hata kama naenda nje basi huwaga kinachonipeleka kinanipa nafasi ya kwenda nao ila sasa inapokuja usafiri uwaache ndo siwez kuamua yaani moyo unauma sana.
lazima kuna atakayekuwepo kutoa msaada. Kama watoto wako ok kiafya, na unasafiri kwa muda mfupi, mimi sioni tatizo liko wapi. Maana maisha yanaendelea hata kwa "forced eviction" ambayo huwa inafanyika bila ridhaa ya mtu. Remember our lives are in the hands of God...
Mbona easy tu unawapeleka kwa mama wakaenjoy na bibi yao,,
Home nimekaa na watoto wa bro for a year, shemeji alikuwa anasoma, na bro yupo nje kikazi watoto wakaletwa kwa bibi yao, yaani mbona tulikoma, bibi na wajukuu kama mayai watoto wakilia tu tunavyofurumushwa ndani kama hatujazaliwa mule, ni katuni tu mda wote... Ukitaka supersport unaambiwa nenda bar
Professional world inachangamoto zake wadau ambazo lazima twende nazo sawa as maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge...