Elections 2015 Njia nyeupe kwa CCM Jimbo la Monduli: Fred Lowassa ajitoa katika kinyang'anyiro cha Ubunge ndani ya CHADEMA

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Freddy Lowassa amejitoa katika kinyang'anyiro cha kuomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli.

Freddy alitoa taarifa ya kujitoa kwa sababu binafsi lakini ndiye aliyetazamiwa kutoa ushindani mkali kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na historia yake ndani ya Jimbo hilo, ambapo alikuwa akishiriki harakati mbalimbali kwa kipindi kirefu wakati baba yake akiwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CCM.

Hali hiyo ya kujitoa kwa Freddy Lowassa, imemwachia Diwani wa Kata ya Lepurko, Yonas Laizer kuongoza kwenye kinyang'anyiro ndani ya CHADEMA, kilichofanyika tarehe 11 Agosti 2018.

Hali hii inatoa nafsi kubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kulirejesha tena mikononi mwake Jimbo hilo baada ya kulipoteza mwaka 2015.

IMG_6285.JPG

IMG_6285.JPG
 
Kauli ya baba yake ilitosha kuonesha maamuzi aliyoyachakua. Hata hotuba ya mwenyekiti imetoka kuonesha mwelekeo. Lazima jimbo lirudi kwenye chama tawala.
 
Kwa hali ilivyo sasa ni uzwazwa kuingia kwenye uchaguzi ukitegemea kuishinda CCM. Maagizo ya bwana yule ni ushindi kwa CCM no matter what. These days he doesn't take no for an answer na hawa makada wa CCM (ambao ndio maDED na surprisingly haohao ndio "waajiriwa" wa Tume ya Uchaguzi kwenye jimbo husika) wanaogopa sana hizi tenguzi pale wanapotenda haki (soma "wanapokengeuka). Upinzani labda wasubiri mpaka uchaguzi mkuu 2020 maana kila mtu atakuwa anafight kwenye jimbo lake
 
Hapa swala ni moja tu, Lowasa kwa sasa ni mzigo mkubwa pale Chadema anatakiwa arudi alipotoka au astaafu. La sivyo chama kitazidi kudhoofu, he is cancer for them kuanza upya siyo ujinga.
 
hakuna uchaguzi ambao ccm itaacha kuchukua.ni kazi bure kushiriki uchafuzi. Dogo kaona mbali
 
Back
Top Bottom