Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Freddy Lowassa amejitoa katika kinyang'anyiro cha kuomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli.
Freddy alitoa taarifa ya kujitoa kwa sababu binafsi lakini ndiye aliyetazamiwa kutoa ushindani mkali kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na historia yake ndani ya Jimbo hilo, ambapo alikuwa akishiriki harakati mbalimbali kwa kipindi kirefu wakati baba yake akiwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CCM.
Hali hiyo ya kujitoa kwa Freddy Lowassa, imemwachia Diwani wa Kata ya Lepurko, Yonas Laizer kuongoza kwenye kinyang'anyiro ndani ya CHADEMA, kilichofanyika tarehe 11 Agosti 2018.
Hali hii inatoa nafsi kubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kulirejesha tena mikononi mwake Jimbo hilo baada ya kulipoteza mwaka 2015.