Njia moja ya kutoboa maisha bila kuumiza kichwa au kuiba

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,289
21,482
Napenda sana andiko miradi miepesi kwa mtu wa chini hususani vijana walioko kati ya miaka 20 hadi 35. Wenye uelewa wa uwekezaji na wauaminifu tujaribu hili

Tukipata vijana 100 wanachama, na kila kijana ana uwezo wakutunza sh 50,000 kila mwezi kiasi ambacho ni kinazekana au chini yake kidogo.

Kwa mwezi
50,000 X 100=5,000,000

`kwa mwaka.
5,000,000 X 12= 60,000,000

Kwa miaka mitano(5)
60,000,000 X 5 = 300,000,000

Wekeza hi pesa kwenye 300,000,000 strategic real estate mji inao kua kama kigamboni kibaha au Goba

Kwa mfano mnapata acre 1 ya aridhi kwa 50,000,000 kila heka

300,000,000 /50,000,000 = 6 acres

Kila heka ina viwanja 8 20×30 au 50 X100ft, kwa hiyo mtakua na viwanja 48 plots, zenye kua na njia nzuri

Kila plot ukiiuza 15,000,000, bei ambao ni ndogo sana and fair

15,000,000 X 48 =720,000,000.

Mtapata milioni mia saba na ishirini.(720,000,000) mkogawana kwa wana chama 100 kila mwana chama hupata milioni 72m.

Mtaji unao weza vizuri kua chazo cha kuvunja the vicious cycle of poverty kwenye familia, ebu fikiliani kuhusu hili kwa makini, naomba constractive critism kuhusu hilo.

Ebu tuongane tupambane na umasikini
 
Shida ni kuvumilia kuweka hizo afu hamsini Kwa miaka mitano....Kwanza hata Kama zinawekwa benki, lazima kiwango cha Imani cha muhasibu na signatories kijadiliwe🤣

Halafu watu Mia kwenye issue ya pesa na hizi akili zetu za kimasikini ni watu wengi sana, vurugu lazima ziwepo....hili wazo walau muwe 20 hivi.
 
Ofcoz Mamy K hata me ndio changamoto kubwa ninayoion maana kwanza watu mia hao wote lazima wawe na kipato cha uhakika wa kiwango cha walao 50k kila mwezi kitu ambacho ni ngumu kwa mazingira yetu ila kwa watu 20 at least inawezekana na pia mkiwa waajiriwa wenye kiwango cha mshahara let say 300k per month mnaweza changia fedha yote ambayo ingechangwa na watu mia kwa kila mmoja kutoa 250k lengo likaenda kama lilivyopangwa

Ni wazo zuri sana hili kama mkiwa serious ase
 
Shida ni kuvumilia kuweka hizo afu hamsini Kwa miaka mitano....Kwanza hata Kama zinawekwa benki, lazima kiwango cha Imani cha muhasibu na signatories kijadiliwe

Halafu watu Mia kwenye issue ya pesa na hizi akili zetu za kimasikini ni watu wengi sana, vurugu lazima ziwepo....hili wazo walau muwe 20 hivi.
Nimependa maono yako ni kweli 100people ni wengi ila mnategeneza system kwamba wote mnawajibika kutoa pesa baada ya miaka mitano......miaka mitano sio mingi ni awamu moja tu ya Raisi ila ni uvumilivu wavijana wetu ndo chagamoto.
 
Mpango mzuri sana ila anza na vijana wanaokuzunguka hapo mtaani kwenu....
Unazungumzia hawa vijana wanaokesha kubet, kunywa pombe, kusaka connection za video za ngono, kuwaza kula tunda kimasihara, kushinda instagram na Twitter kutafuta udaku?
Maana hao ndio vijana waliotuzunguka hapa mtaani.
 
Duh unasema ukweli hali ni mbaya sana huku mitaani vijana hawana muelekeo kabisa
 
Back
Top Bottom