Njia moja wapo ya kumfanya mtu kuwa msukule

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,053
Nilikuwa napitia kitabu kimoja kilichoandikwa na mwanadada Alice Werner kiitwacho, MYTHS AND LEGENDS OF THE BANTU, kilichochapishwa mwaka 1932 nchini uholanzi. Lakini ni tafiti tosha kabisa za mwanadada huyu kuhusu mambo gani wabantu wanayaamini na kuyaishi. Alifanya mahojiano na wabantu sehemu za kusini mwa jangwa la Sahara. Na kwakweli wabantu walifunguka kweli kweli Mana kitabu chenyewe ukikimaliza unaweza kujikuta ushakuwa mchawi.

Kwenye tafiti zake alijikita kwenye nini imani na simulizi/hadithi za wabatu kuhusu mambo yafuatavyo;
~Binadamu ametokea wapi, na jinsi gani kifo hutokea.
~Simulizi kuhusu Mungu na miungu
~simulizi kuhusu mbingu na watu waliokufa(roho) ama mizimu
~Story za watu maarufu waliosadikika kuwa nusu miungu, hapa Kuna hadi story ya Fumo Lyongo
~Imani na hadithi kuhusu radi, upinde wa mvua, gharika, na mvua yenyewe
~Waganga, Manabii na WACHAWI
~Na stori nyingine za wanyama Kama Kobe, fisi, sungura nk

Turudi kwenye mada, Msukule ameelezewa kadiri ya makabila tofauti aliyotembelea mwanadada huyo, Kuna kabila la Zulu of South Africa, Lamba of Northern Rhodesia na Yao ambao wanapatikana Tanzania mikoa ya kusini na Msumbiji pia.
Kwa Wayao, Msukule humuita "Ndondocha" wakati Walamba humuita "Tuyewera" na wazulu humwita "Umkovu" na njia za upatikanaji wao ni tofauti kabisa.
Sasa tuone wanyao wao wakimpataje Ndondocha na matumizi yao yalikuwaje;

Kwanza, mtu ambaye amewekwa kwenye shabaha za kuwa Ndondocha anauliwa kichawi na ndugu wa damu kabisa, kaka, mama, mjomba, ila lazima awe ndugu ambaye anafungamana na undugu wa mama. Hapa shangazi haruhusiwi kuua.
Siku ya mazishi au ndani ya siku tatu (isizidi siku tatu) muuaji/mchawi anaenda kaburini usiku akiwa na aidha mkia wa mnyama au pembe ya mnyama iliyokolea dawa za kichawi. Akifika kaburini atalitishia kaburi kwa vifaa hivyo akisema maneno "inuka mama yako amekuamrisha utoke nje" nadhani hapa anatumika "mama" na siyo baba kwakuwa ndiye mwenye unasaba wa kuaminika na ndiyo maana hata wauwaji lazima wawe ndugu za mama siyo akina shangazi.

Baada ya hapo, kaburi linafunuka, na mfu hutokea lakini katika hali isiyoonekana kwa macho ya kawaida. Hapo mchawi humchukua mtu wake Hadi kwenye chumba maalumu alichokitenga nyumbani kwake. Akifika naye maskani, anampiga dawa kali sana ambazo zinamrejeshea uzima wake uliokamilika na badaye anamkata miguu kwenye pingili za magoti.
Toka hapo sasa, Ndondocha atakuwa amekamilika akiwa na upungufu wa akili, viungo na uhai wake upo mikononi mwa boss wake. Atalishwa na mchawi mwenyewe na hataweza kutembea kwenda kokote bila ruhusa ya boss. Na kama akiwa na njaa hutoa sauti kama ya paka, hawezi kuongea. Hutembea kwa kutambaa na mikono na vipande vya miguu iliyosalia.

Kadiri ya mtafiti, anasema aina hii ya Msukule ndiyo yenye nguvu zaidi ya kichawi kuliko Msukule yeyote. Kwanza inampa nguvu kubwa ya kichawi mmiliki, unaweza ukajikuta unaogopeka Kijiji kizima. Kwasababu matumizi makubwa ya misukule aina hii ni kuwauwa maadui. Na wakisababisha kifo, basi usiku kucha watalia Kama paka mtaani na watu wa enzi hizo wakisikia sauti zao Kama za paka wanajua kuwa Leo Kuna mtu atakufa. Na kweli kifo hutokea.

Hupewa dawa maalum za kuwafanya waendelee kuishi.
IMG_20200512_143810.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi mkuu baada ya kumaliza chote mkuu hatuwezi tutest kuwaroga mi-ccm yote mkuu,tuifanye misukule,iwe inasafisha barabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la mtafiti ni moja, maelezo hayajafunguka sana kuelezea mchanganyo wa dawa za kichawi. Kama Ni hirizi hakuna uwazi wa moja kwa moja kwamba hirizi hiyo ina mchanganyo wa nini na nini. Anataja tu vichache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeki-google bila mafanikio
Nalog off
Ni cha mda sana, sidhani Kama kipo in soft copy, Mimi nilipewa Kama zawadi na Padre mmoja wa kikatoliki ambaye alishafariki na alikuwa miongoni mwa mapadre wa Kwanza kabisa weusi hapa bongo. Alikuwa ndugu yetu sasa nikiwa chuo kila nikimtembelea kumsalimia alikuwa na kauli moja kuwa "wewe Msomi nitakupa urithi wa vitabu" akawa ananipa vitabu. Kimoja wapo ni hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ibn
dah ndio umeishia mkuu ama kuna part 2 na kama unawaitaji ili uwatume kazi wanapatikanaje
 
Back
Top Bottom