Njia 10 za kupunguza matumizi ya mafuta kwenye gari lako

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,363
11,519
NJIA 10 ZA KUPUNGUZA MATUMIZI YA MAFUTA KWENYE GARI LAKO

1. Hakikisha kuwa unalifanyia gari lako service kwa wakati muafaka.usisubiri mpaka gari ipate tatizo kabisa ndo ubadilishe kifaa husika. Hii ni kwa usalama na kufanya gari lidumu kwa muda mrefu

service.jpg

Kulingana na EPA unapolifanyia gari lako service kila wakati una uhakika wa kuokoa 4% za mafuta, tairi nzuri zilizofungwa vizuri kwa maana ya kuwa ni laini hazibanwi na break au uchafu zinaokoa 3% ya mafuta.

Na unapotumia Oil sahihi kwa gari lako unakoa 2% za matumizi ya mafuta. Hivyo hakikisha gari linatembea kiulaini,na kuchoma mafuta vizur kabisa.wheel alignment ziwe vizuri, filters ziwe safi,spark plug ziwe safi na origin.

2. Punguza uzito usio na lazima. Kama huna sababu ya kuwa na mizigo kwenye boot au gari ushushe kwa kuwa unaongeza matumizi ya mafuta hasa gari inapokuwa inashika mwendo(accelerate) unapopunguza kilo 45 unaokoa 2% ya mafuta. Gari linapokuwa jepesi zaidi na matumiz ya mafuta yanapungua zaidi
magari.jpg

3. tunapofikia kuendesha gari kwa speed ya kuanzia km 45 gari linatumia nguvu kubwa zaid ili kuushinda upepo.hivyo unashauriwa kupandisha vioo juu kiasi flan ili upepo usiingie ndani,usifungue sun roof. Na hapa utaokoa asilimia 1 mpaka 15 ya mafuta.

speed.jpg


4. Unapoanza kushika kasi (ku accelerate) hakikisha unaanza kushika kasi taratibu(kuongeza speed) iwe wastani si ule uendeshaji wa kuchomoka na gari mpaka tair zina slide.

Lakini pia hapa usiongeze sped taratibu sana kwa maana ya kuwa usitumie gear ndogo kwa muda mrefu.ongeza mwendo taratibu kwa mfano unaweza kutumia sekunde 15-20 kufika 80km/h.hii itafanya gari iondoke kwa ulaini huku ikiongeza speed pia kwa ulaini.EPA wanakadiria kuwa uendeshaji mzuri unasaidia kuokoa mafuta kwa 33%.

5. Kuna wale ndugu zangu wanaoendesha gari manual wanapenda sana kuungurumisha gari katika gear ndogo kabla ya kubadili gear. Hapa pia kuna upotevu mkubwa wa mafuta

6. Angalia speed yako. Mara nyingi mileage ina panda kwa speed ya km 64 mpka89/h ukiwa unatumia gear ya juu kabisa katika gari lako. Hii pia huwa inategemeana na aina ya engine,uzito wa gari na drag.

7. Gari za kisasa hazihitaji kuzipasha moto kwa muda mrefu ni kupoteza mafuta. Kama unamsubiria mtu kwa zaidi ya dk 1 ni bora tu kuzima engine, au kama kuna folen na gari hazisogei ni bora pia kuzima gari

8. Ingawa matumiz ya vifaa vya umeme huwa haiepukiki kitu pekee ambacho unapaswa kufikiria katika suala la matumizi ya mafuta ktk gari ni Air Conditioning. Hii inaongeza mzigo au uzito katika engine hivyo inafanya mafuta yatumike zaidi.na hii inaweza kuokoa 10% yamafuta kama hakuna haja sana ya kutumia AC

9. Epuka Traffic Jam: Hii mtu anaweza kuona ni sababu ya kipuuzi, kuwa dar utaepuka vipi traffic jam, inawezekana kias flan . hebu tumia vyema simu yako pengne hata kwa kumuuliza jama yapo aliyetangulia kazini vipi folen ya Ubungo/buguruni/tazara/magomen? Then ukaangalia njia mbadala kukwepa folen. Ile kuzima gari kuwasha au kusimama muda mrefu kwenye folen kunafanya mafuta yatumike zaidi.

jam.jpg


10. Tumia mafuta yasiyochakachuliwa na hii ina maana nunua mafuta kwenye vituo vinavyoaminika achana na cituo vya mafuta vya aina fulan fulan na vinajulikana kwa majina na pia vile vya uchochoron. Nenda kanunue mafuta safi kabisa na pia usishawishike kuchanganya na kitu chochote.

france-fuel_2298290b.jpg


NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI,WAZAZI WANGU NA MKE WANGU NA MTOTO WETU MPENDWA.

Na pia familia yangu kwa kunisupport na kunivumilia wakati nikiandika.

NAWASILISHA, TAYARI KWA KUJADILIWA
 
Swala la kuzima A/C na Kutembea vioo chini si ndio yale yale ya kuongeza mzigo wa upepo ndani? Thanks for the useful thread.
 
Very useful topic...ni vizuri kupandisha vioo wakati was mwendo kasi na kushusha kioo wakati wa foleni na jua sio kali,
Ni vizuri kucheki upepo wa tairi kila wiki,
Kwa wazee wa subaru ni vizuri ukatembea na gari ikiwa kwenye ECO mode, hii inasaidia sana.
 
Useful topic,
La kuongeza ni kubadilisha air cleaner mara kwa mara,kupenda kutumia multgrade oils,kwa wale wanaotumia magari ya petrol yenye distributors wanashauliwa kubadilisha zile waya zinazopeleka umeme kwenye spark plugs baada ya kipindi fulani kwani husababisha plugs zisiwe na ufanisi mkubwa na kwa magari ya kisaza ya coils na highbreed ni kuhakikisha spark plugs zinabadilishwa at least mara moja kwa mwaka,petol filters nazo zatakiwa kubadilisha mara kwa mara.
Nawasilisha.
 
asante kwa kutafsiri kwa kiswahili

hyo makala nmewahi isoma lakini kwa kiingereza
 
Back
Top Bottom